Akizungumza katka mgahawa huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara
ya Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif, alisema kuwa lengo la kampeni hiyo
ni kuwahamasisha wateja wa Benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi
na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu. “Pamoja na punguzo la
asilimia kumi kwa malipo yao, wateja wetu pia watapata nafasi ya
kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fulana, vikombe na nyingine vingi.
Meneja wa Bar ya Tips Beach Kidimbwi, Bi Joan Pascal, alisema kuwa wateja wao wamefurahia sana kampeni hiyo kwani ni mwanzo mpya wa kuachana na utamaduni wa kutumia fedha taslimu kufanya malipo.
Meneja wa Bar ya Tips Beach Kidimbwi, Bi Joan Pascal, alisema kuwa wateja wao wamefurahia sana kampeni hiyo kwani ni mwanzo mpya wa kuachana na utamaduni wa kutumia fedha taslimu kufanya malipo.
Afisa
Mauzo wa Benki ya CRDB, Francis Mgani (kushoto), akimkabidhi zawadi ya
fulana, Patrick Michael, baada ya kufanya malipo kwa kutumia
TemboCardvisa wakati wa mwendelezo wa kampeni ya “Chanja, Lipa, Sepa”
ya kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na
kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu. Kampeni hiyo hiyo
ilifanyika katika Mgahawa wa Beach Kidimbwi uliopo Mbezi Beach, jijini
Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Wakala FahariHuduma, Nasra Abdallah (kulia), akitoa huduma kwa mmoja wa watu waliofika katika Bar ya Beach Kidimbwi.
Mteja akifungua akaunti Mpya ya Benki ya CRDB.
Afisa
wa Benki ya CRDB, Bi. Rehema, akimpa zawadi mteja wa benki hiyo baada
ya kufungua akaunti Mpya wakati wa mwendelezo wa Kampeni ya “Chanja, Lipa, Sepa” ya kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu.
Mteja
wa Benki ya CRDB, akifanya malipo kwa kutumia TemboCardvisa wakati wa
mwendelezo wa kampeni ya ‘Chanja, Lipa, Sepa’ ya kuhamasisha wateja wa
benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa
kutembea na fedha taslimu, iliyofanyika Mbezi Beach jijini Dar es
Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Huduma za
Uwakala CRDB, Fadhil Mollel.
No comments :
Post a Comment