Tuesday, July 17, 2018

TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA PICHA 1.

PICHA 1.

Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.

PICHA 2.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Bw. Faustine Mdesa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna wa Kodi za Ndani Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.

PICHA 3.

Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.

PICHA 4.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo (kushoto) akimwelezea jambo Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na watendaji wengine wa TRA aliofuatana nao kuhusu namna sekta ya utalii nchini inavyochangia pato kubwa kwa Serikali wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna huyo Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)
 ………………………………..

Na Rachel Mkundai, Arusha
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA SHAMBA LA DENGU NA KUZINDUA GHALA LA KUHIFADHIA MAZAO YA WAKULIMA KATIKA KIJIJI CHA BULIGE WILAYANI KAHAMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la dengu lenye ukubwa wa ekari 10, mali ya Bw. Philipo Kapande  (kushoto) katika kijiji cha  Jomu kwenye Halmashauri ya  Msalala Julai 17, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la dengu lenye ukubwa wa ekari 10, mali ya Bw. Philipo Kapande  (wapili kushoto) katika kijiji cha  Jomu kwenye Halmashauri ya  Msalala Julai 17, 2018.  Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la ghala la kuhifadhia mazao ya wakuliama katika kijiji cha  Bulige kwenye Halmashauri ya Msalala Juali 17, 2018. Anayemsaidia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikata utepe kuzindua ghala la kuhifadhia mazao ya wakulima katika kijiji cha Bulige kwenye Halmashauri ya Msalala, Julai 17, 2018.  Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi, Macha, wapili kushoto ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel  Maige na  wanne kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Aza Hilal. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga na wapili kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Elius Kwandikwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TUTAPELEKA MILIONI 300 KUPANUA JENGO LA WAZAZI HOSPITALI YA KITETE TABORA: WAZIRI UMMY

  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iemahidi kupeleka shilingiu milioni 300 kupanua jingo lka wazazi Hospitali ya Rufaa Kitete mkoani Tabora.

Hayo yemesemwa leo Julai 17, 2018 na Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu, (pichani) katika ukurasa wake wa Facebook, ambapo alifanya ziara kwenye hospitali hiyo kufuatilia utoaji wa huduma za afya na kubaini moja ya changamoto kubwa inayoikabili hospitali hiyo ni udogo wa jingo la wazazi.

“ Leo nipo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Kitete kufuatilia utoaji wa huduma za Afya. Changamoto kubwa ni uhaba wa watumishi hasa wauguzi na ufinyu wa Wodi ya Wazazi. Mwezi huu tumepeleka Wauguzi wapya 39 na watumishi wengine 10. Aidha, tunaleta shs 300m kupanua jengo la Wazazi na kukamilisha Chumba cha Upasuaji (Theatre)” Alisema Mhe. Waziri.WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua fao la Ushirika Afya ambalo linawalenga wananchi wanaojishughulisha na kilimo kupitia ushirika.
Amezindua fao hilo jana (Jumatatu, Julai 16, 2018) kwenye mkutano uliofanyika katika

MAJALIWA AMTAMBULISHA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA KWA WANANCHI NA KUWEKA JIWE LA MSINGI LA KITUO CHA AFYA CHA CHELA WILAYANI KAHAMA.


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha  wakati alipoweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Mkuu huyo wa wilaya aliapishwa jana asubuhi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Teklack.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha  wakati alipoweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Mkuu huyo wa wilaya aliapishwa jana asubuhi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Teklack.
 Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha akiwatambulisha viongozi wa wilaya ya Kahama wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasalimia wananchi wa Kijiji cha Chela baada ya kuweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Wanne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kulia ni Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipoweka  jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Watatu kushoto ni  Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na watano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha na watatu kulia ni Mwenyeiiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa. Kushoto ni  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elius Kwandikwa wapili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Kulia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI AKUTANA NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA.


 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, (Kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye.
NA MWANDISHI WA JESHI LA ZIMAMOTO
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Phaustine Kasike mapema leo asubuhi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.
Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.
Vilevile Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.
“Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO KATI YA VYAMA VYA SIASA VYA AFRIKA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) JIJINI DAR ES SALAAM.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

  Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

 
Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika mkutano huo wa viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika na Chama hicho cha CPC jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally akihutubia katika mkutano huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)