Tuesday, July 17, 2018

TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA PICHA 1.

PICHA 1.

Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.

PICHA 2.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Bw. Faustine Mdesa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna wa Kodi za Ndani Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.

PICHA 3.

Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.

PICHA 4.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo (kushoto) akimwelezea jambo Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na watendaji wengine wa TRA aliofuatana nao kuhusu namna sekta ya utalii nchini inavyochangia pato kubwa kwa Serikali wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna huyo Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)
 ………………………………..

Na Rachel Mkundai, Arusha
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA SHAMBA LA DENGU NA KUZINDUA GHALA LA KUHIFADHIA MAZAO YA WAKULIMA KATIKA KIJIJI CHA BULIGE WILAYANI KAHAMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la dengu lenye ukubwa wa ekari 10, mali ya Bw. Philipo Kapande  (kushoto) katika kijiji cha  Jomu kwenye Halmashauri ya  Msalala Julai 17, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la dengu lenye ukubwa wa ekari 10, mali ya Bw. Philipo Kapande  (wapili kushoto) katika kijiji cha  Jomu kwenye Halmashauri ya  Msalala Julai 17, 2018.  Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la ghala la kuhifadhia mazao ya wakuliama katika kijiji cha  Bulige kwenye Halmashauri ya Msalala Juali 17, 2018. Anayemsaidia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikata utepe kuzindua ghala la kuhifadhia mazao ya wakulima katika kijiji cha Bulige kwenye Halmashauri ya Msalala, Julai 17, 2018.  Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi, Macha, wapili kushoto ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel  Maige na  wanne kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Aza Hilal. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga na wapili kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Elius Kwandikwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TUTAPELEKA MILIONI 300 KUPANUA JENGO LA WAZAZI HOSPITALI YA KITETE TABORA: WAZIRI UMMY

  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iemahidi kupeleka shilingiu milioni 300 kupanua jingo lka wazazi Hospitali ya Rufaa Kitete mkoani Tabora.

Hayo yemesemwa leo Julai 17, 2018 na Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu, (pichani) katika ukurasa wake wa Facebook, ambapo alifanya ziara kwenye hospitali hiyo kufuatilia utoaji wa huduma za afya na kubaini moja ya changamoto kubwa inayoikabili hospitali hiyo ni udogo wa jingo la wazazi.

“ Leo nipo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Kitete kufuatilia utoaji wa huduma za Afya. Changamoto kubwa ni uhaba wa watumishi hasa wauguzi na ufinyu wa Wodi ya Wazazi. Mwezi huu tumepeleka Wauguzi wapya 39 na watumishi wengine 10. Aidha, tunaleta shs 300m kupanua jengo la Wazazi na kukamilisha Chumba cha Upasuaji (Theatre)” Alisema Mhe. Waziri.WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua fao la Ushirika Afya ambalo linawalenga wananchi wanaojishughulisha na kilimo kupitia ushirika.
Amezindua fao hilo jana (Jumatatu, Julai 16, 2018) kwenye mkutano uliofanyika katika

MAJALIWA AMTAMBULISHA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA KWA WANANCHI NA KUWEKA JIWE LA MSINGI LA KITUO CHA AFYA CHA CHELA WILAYANI KAHAMA.


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha  wakati alipoweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Mkuu huyo wa wilaya aliapishwa jana asubuhi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Teklack.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha  wakati alipoweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Mkuu huyo wa wilaya aliapishwa jana asubuhi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Teklack.
 Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha akiwatambulisha viongozi wa wilaya ya Kahama wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasalimia wananchi wa Kijiji cha Chela baada ya kuweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Wanne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kulia ni Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipoweka  jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Watatu kushoto ni  Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na watano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha na watatu kulia ni Mwenyeiiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa. Kushoto ni  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elius Kwandikwa wapili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Kulia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI AKUTANA NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA.


 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, (Kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye.
NA MWANDISHI WA JESHI LA ZIMAMOTO
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Phaustine Kasike mapema leo asubuhi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.
Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.
Vilevile Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.
“Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO KATI YA VYAMA VYA SIASA VYA AFRIKA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) JIJINI DAR ES SALAAM.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

  Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

 
Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika mkutano huo wa viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika na Chama hicho cha CPC jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally akihutubia katika mkutano huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)

MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE YAUNGA MKONO UJENZI WA VIWANDA NCHINI


  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhandisi Ramo Makani akiuliza swali kwa mwakilishi wa kampuni ya simu ya Vodacom (hayupo pichani) waliojenga mnara kwenye eneo la kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Morogoro wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Selemani Kakoso na wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi wa Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye.
NA WUUM, MOROGORO
KAMATI ya Bunge ya Miundombinu imeanza ziara ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wote kwenye maeneo mbali mbali nchini ambapo wamekagua uwepo wa mawasiliano hayo kwenye eneo la kijiji cha Mkulazi kilichopo tarafa ya Ngerengere mkoa wa Morogoro ambapo Serikali imedhamiria kuwekeza na kujenga kiwanda cha sukari.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Selemani Kakoso akiongoza wajumbe wa Kamati yake, wamefika kwenye eneo hilo la uwekezaji na kudhibitisha uwepo wa mawasiliano. Kakoso ameushukuru Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kutekeleza azma ya Serikali ya kupeleka mawasiliano ambapo hamna mawasiliano na imewezesha nia ya Serikali ya kuwekeza kwenye viwanda.
Kakoso amewataka wananchi waitumie nafasi hii vizuri, minara inahitaji ulinzi ili rasilimali iliyowekwa iweze kufanya kazi muda wote. “Wananchi watambue mradi ni mali yao,” Kakoso amesema. Ameishukuru na kuipongeza UCSAF kwa kufanya kazi ya kufikisha huduma za mawasiliano kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara kama haya ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano. Amefafanua kuwa eneo hili lina wakazi wachache lakini UCSAF imefikisha huduma za mawasiliano. Pia tumeshuhudia eneo hili lina wanafunzi wanasoma, nashauri UCSAF muwapatie vifaa vya TEHAMA ili kuwawezesha kusoma vizuri zaidi.
Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa Serikali iliilekeza Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuwekeza na kujenga kiwanda cha sukari katika eneo la Mkulazi lililopo Kata ya Mkulazi, tarafa ya Ngerengere mkoa wa Morogoro. Nditiye ameishukuru Kampuni ya simu ya Vodacom kwa kushirikiana na UCSAF kujenga mnara na kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi ambapo amekuta mawasiliano kweli yapo. “Mawasiliano ni uchumi na ni usalama”, Nditiye amesema. “UCSAF imefanya kazi kubwa sana, huku hakuna kampuni yeyote inaweza kujitokeza peke yake kuja kuwekeza mawasiliano kwenye eneo kama hili bila kupata ruzuku ya Serikali,” amesema Nditiye.  Ameongeza kuwa, uwepo wa mnara huu utawawezesha wawekezaji kuwasiliana ndani na hata nje ya nchi.
Katibu Mtendaji wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga amesema kuwa Mkulazi ni eneo ni jipya la uwekezaji ambapo linafanyiwa uwekezaji na mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF na NSSF na wamepewa eneo hilo na Serikali kujenga kiwanda cha sukari tangu mwaka 2016 ambapo walifika UCSAF na kuiomba ijenge na kufikisha huduma za mawasiliano kwenye eneo hilo kwa kuwa hapakuwa na mawasiliano ya aina yoyote. Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa upande wa viwanda na uwekezaji wa  kujenga viwanda, “sisi tulipokea ombi hilo na kuwasiliana na kampuni za simu ambapo Vodacom walikubali na walichukua ruzuku na kujenga mnara huo,” amesema Ulanga.
Amefafanua kuwa UCSAF tuliipatia Vodacom shilingi milioni 140 za kujenga mnara huo ambapo nao wenyewe Vodacom waliongeza fedha zao kwa kuwa ujenzi wa mnara huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 300.  Mnara huu umeanza kufanya kazi tangu miezi miwili iliyopita ha hadi sasa una miezi minne tangu ulipoanza kujengwa.
Ulanga ameongeza kuwa tayari UCSAF imeshapokea maombi kutoka kwa wajenzi wa Stigglers Gorge  ya kufikisha na kuboresha mawasiliano kwenye maeneo yao ya makambi  ili kuwawezesha kupata huduma za mawasiliano wakati wa ujenzi wa mradi huo ili waweze kuwasiliana.
Mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom kutoka Makao Makuu ya kampuni hiyo iliyopo Dar es Salaam Mhandisi wa Mawasiliano na Mipango Bwana David Mbogela amesema kuwa eneo hilo halikuwa na mawasiliano ya aina yoyote hapo awali ambapo wao wamejenga mnara huo kwa kushirikiana na UCSAF. Ameongeza kuwa mnara huo unatumia nishati ya umeme wa jua na jenereta ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata mawasiliano wakati wote kwa kuwa hakuna chanzo kingine cha nishati ya umeme.
Naye mwanakiji wa kijiji cha Mkulazi aishie maeneo hayo Bwana Naize Omary Uzuri  ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa kuwawezesha kupata huduma za mawasiliano kwa kuwa katika kijiji chao tangu huduma za mawasiliano zianze kutumika nchini, kijiji chao hakijawahi kupata huduma hiyo.
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara yao ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwenye eneo la kiwanda cha sukari lililopo kijiji cha Mkulazi, Morogoro. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Selemani Kakoso na wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga


Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga akiongea na waandishi wa habari kuhusu ufikishaji wa huduma za mawasiliano kwenye eneo la kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Morogoro wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (wanaomsikiliza). Anayesikiliza kwa makini wa tatu kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete

MAPOKEZI YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA MAKAO MAKUU YA JESHI HILO LEO


PIX%2B2
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akipokea salamu ya heshima kutoka kwa Gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili ya mapokezi yake Makao Makuu ya Jeshi hilo.
PIX1
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike akipokea saluti kutoka kwa Kamishna wa Utawala wa Magereza, Gaston Sanga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini, Dar es Salaam, leo Julai 16, 2018.
PIX%2B3
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza.
PIX%2B4
Kamishna Jenerali mstaafu, Dkt. Juma Malewa(suti nyeusi) akimkaribisha Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Phaustine Kasike mara baada ya kumaliza kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na maofisa na askari wa Jeshi la Magereza.
PIX%2B5
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini wakifanya mahojiano maalum na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike mara baada ya mapokezi Makao Makuu ya Jeshi hilo.
PIX%2B6
Kamishna Jenerali mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(suti nyeusi) akifurahia jambo pamoja na Kamishna Jenerali mpya wa Magereza Phaustine Kasike wakiongozana kuelekea katika mazungumzo maalum na Maofisa, askari na watumishi raia wa Jeshi hilo Makao Makuu ya Magereza.
PIX%2B7
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Maafisa, askari na watumishi raia wa Jeshi hilo.
PIX%2B8
Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza, Maafisa, Askari na watumishi raia wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali mpya wa Jeshi hilo(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI NA STL GROUP


 Balozi Seif akimsisitiza jambo Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Amand Group iliyo chini ya Taasisi ya STL Group  Bwana Nadas Simhoni aliyeuongozi ujumbe wa viongozi wanne wa Kampuni hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
(katikati), akizungumza na uongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kitaalamu inayosimamia Makampuni  Sita yanayojihusisha na masuala ya Miundombinu, Afya, Elimu, Biashara, Umeme na Mawasiliano ya Kisasa ya STL Group huko Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

NA OMPR, ZANZIBAR
UONGOZI wa Taasisi ya Kimataifa ya Kitaalamu inayosimamia makampuni  sita yanayojihusisha na masuala ya Miundombinu,

TUMIA HII YA MWANZO IMEKOSEWA; WAZALISHAJI DAWA KUTOKA NCHI 25 WAKUTANA NA BOHARI YA DAWA (MSD) JIJINI DAR ES SALAAM


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika Mkutano ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD), uliowakutanisha  na wazalishaji wa dawa na vifaa tiba kutoka ndani na nje ya nchi uliofanyika leo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam ambapo wazalishaji zaidi ya 
130 kutoka nchi 25 walihudhuria.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu akizungumza.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante ole Gabriel, akizungumza katika mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa MSD wakifuatilia  mkutano huo.
Wafanyakazi wa MSD wakiwa katika mkutano huo.
Wazalishaji dawa na vifaa tiba wakiwa kwenye mkutano.
Wafanyakazi wa MSD, wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mwakilishi wa Wazalishaji wa ndani, kutoka Kiwanda cha Prince Phermaceutical,Hetal Vitalan, akizungumza.
Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Abdul Mwanja akizungumza.
 Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa MSD, Sako Mwakalobo, akizungumza.
 Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza  wa  Mamlaka ya  Chakula na Dawa (TFDA), Adonis Bitegeko, akizungumza.
Wazalishaji dawa  wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Na Dotto Mwaibale
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Mpoki Ulisubisya, amesema uwezo wa Bohari ya Dawa (MSD), umeongeza na kupanua wigo wa uwekazaji na uzalishaji wa dawa nchini.
Akizungumza kwenye Mkutano wa pili wa mwaka wa MSD na wazalishaji na washitiri wa dawa na vifaa tiba zaidi ya 130 kutoka nchi 25, Dkt. Mpoki amesisitiza kuwa, MSD niya kiwango cha kimataifa hivyo milango iko wazi kwa wawekezaji wa dawa na vifaa tiba kuja kuwekeza nchini.
Aliongeza kuwa mkutano huo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na kujadili namna yakufanya manunuzi,utekelezaji wamikataba na uimarishaji wa uwekezaji katika sekta ya afya.
“Tunaitikia wito wa serikali wa kuhakikisha wawekezaji wa ndani wanapewa kipaumbele, hivyo mkutano huu wakiutendaji,utaijengea uwezo MSD na kuongeza ushirikiano kati yake na wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba kwa kujua mahitaji aliyopo na kuwashauri soko tulilonalo ndani na njeya nchi ilikupanua wigo wautendaji,”alisema.
Aidha alisisitiza  kuwa  uwezo wa MSD katika usambazaji wa dawa na vifaa tiba umekua na  ndio sababu ya kukidhi viwango vya kimataifa, huku  mwaka wa fedha uliopita wakiwa wameweza  kutumia dola milioni 700 kwa ajili ya kufanya manunuzi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel, alisema utendaji wa MSD meboresha huduma za afya nchini na uhusiano wa karibu kati ya wizara yake na sekta ya afya nikichocheo muhimu cha uchumi nchini.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu, alisema hatua ya bohari kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, imewawezesha kupanua wigo wa huduma na  kuwa karibu na wafanyabiashara na wawekezaji 160 alioingia nao mikataba, hivyo mkutano huo utawajengea uwezo na kuongeza ushindani kwa wazalishajihao.
Aidha, kwa upande wake mwakilishi wa wazalishaji wa ndani, kutoka kiwanda cha Prince Phermaceutical,HetalVitalan, lisema uimarishaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba  hapa nchini,umesaidia fedha inayotengwa na serikali katika bajeti ya dawa  kuweza kukuza uchumi wa ndani,kuongeza ajira kwa watanzania  na kupanua wigo waukusanyaji wa kodi kwa viwanda vya ndani.