Hilo limethibitishwa na Rais wa Simba, Evans Aveva katika mkutano mkuu wa Simba ambao ulikuwa unafunga msimu wa 2015/2016 kwa kutolewa taarifa na kuweka mipango mipya kwa msimu ujao.
Hatua hiyo imekuja baada ya mmoja wa mashabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa makampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji “MO” kutangaza nia ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 na kutoa Bilioni 20 kwa ajili ya kuisaidia Simba kurudi katika makali yake ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri, kocha mzuri, kujenga kiwanja, kuweka vituo vya kukuzia vipaji vya Simba na vingine vingi.
Kutokana na jambo hilo, mashabiki wa Simba walionekana kuvutiwa na mipango ya MO na hivyo kuandamana katika ofisi za klabu na kushinikiza uongozi kukubaliana na MO ili kununua hisa na kuanza kuwekeza ili Simba irudi katika makali ya kushinda mataji.
Ipo hapa video ikimuonyesha Rais wa Simba, Evans Aveva akitangaza mkutano wa Simba kuridhia kufanya mabadiliko.