Kampuni ya uchimbaji wa madini
ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi umekabidhi madawati 4494 yenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 548 kwa ajili ya shule za sekondari
na msingi za mkoa wa Shinyanga.Mwandishi wetu Kadama Malunde,anaripoti.
Akikabidhi madawati hayo,meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema Kampuni yake imekabidhi kiasi hicho cha madawati kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari.
“Mgodi wa Buzwagi unaunga mkono jitihada zinazofanywa na rais wa awamu ya tano,Dkt. John Pombe Magufuli katika kumaliza tatizo la wanafunzi kukaa chini,tumeamua kutekeleza kwa vitendo jitihada hizo” ,alieleza Mwaipopo.
Akipokea madawati hayo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi Zainab Telack ameupongeza mgodi wa Buzwagi kwa mchango wao uliolenga kuunga mkono jitihada za mheshimiwa rais Magufuli, katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanakaa kwenye madawati.
“Nimefarijika sana kuona mnaunga mkono serikali,tulikuwa na upungufu wa madawati lakini kwa msaada huu wa madawati mmesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo”,alisema Telack.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote katika mkoa wa Shinyanga kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wote wanaowaachisha masomo wanafunzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija akishukuru kwa niaba ya halmashauri za mkoa wa Shinyanga, ameupongeza Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada zao mbalimbali katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo katika mkoa wa Shinyanga na hususani wilaya ya Kahama.
Hafla hiyo ya kukabidhi madawati ilifanyika Julai 28,2016 katika Shule ya Msingi Majengo iliyoko wilayani Kahama katika halmashauri ya mji wa Kahama ambapo ilihudhuriwa pia na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga,viongozi wa wilaya ya Kahama,uongozi wa Mgodi wa Buzwagi, walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Majengo.
Akikabidhi madawati hayo,meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema Kampuni yake imekabidhi kiasi hicho cha madawati kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari.
“Mgodi wa Buzwagi unaunga mkono jitihada zinazofanywa na rais wa awamu ya tano,Dkt. John Pombe Magufuli katika kumaliza tatizo la wanafunzi kukaa chini,tumeamua kutekeleza kwa vitendo jitihada hizo” ,alieleza Mwaipopo.
Akipokea madawati hayo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi Zainab Telack ameupongeza mgodi wa Buzwagi kwa mchango wao uliolenga kuunga mkono jitihada za mheshimiwa rais Magufuli, katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanakaa kwenye madawati.
“Nimefarijika sana kuona mnaunga mkono serikali,tulikuwa na upungufu wa madawati lakini kwa msaada huu wa madawati mmesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo”,alisema Telack.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote katika mkoa wa Shinyanga kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wote wanaowaachisha masomo wanafunzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija akishukuru kwa niaba ya halmashauri za mkoa wa Shinyanga, ameupongeza Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada zao mbalimbali katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo katika mkoa wa Shinyanga na hususani wilaya ya Kahama.
Hafla hiyo ya kukabidhi madawati ilifanyika Julai 28,2016 katika Shule ya Msingi Majengo iliyoko wilayani Kahama katika halmashauri ya mji wa Kahama ambapo ilihudhuriwa pia na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga,viongozi wa wilaya ya Kahama,uongozi wa Mgodi wa Buzwagi, walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Majengo.
Radio Maria waiomba Serikali kurekebisha Sheria ya leseni ya redio za jamii
Mwashamu
Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara akikata keki wakati wa sherehe za
kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini
Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, katikati ni Mkurugenzi wa Redio
Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendeleo.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akikata keki wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya
Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam yaliyoanza rasmi tangu
April 26 mwaka huu. Katikati ni Mwashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki
la Mtwara Titus Mdoe,kutoka kulia ni Mhamasishaji Mkuu wa Redio Maria
Tanzania Bi. Veronica Mwita na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Redio
Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendeleo.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Benjamin William Mkapa akisalimiana na Baba Askofu wa Jimbo
Katoliki la Mtwara Mwashamu Askofu Titus Mdoe wakati wa sherehe za
maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es
Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padre. John
Maendeleo.
Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Saalam Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo akizungumza na wadau na marafiki wa Redio Maria Tanzania leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea
kuanzishwa kwa Redio hiyo
Mkurugenzi
wa Redio Maria Tanzania Padre John Maendeleo akizungumza na wadau na
marafiki wa Radio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Rais
wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius Kira akizungumza na wadau na
marafiki wa Radio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akipokea risala kutoka kwa Rais wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius
Kira(Kulia) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya
Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akipeana mkono na baadhi ya marafiki wa Redio Maria Tanzania waliofika
kuchangia Redio hiyo katika harambee iliyofanyika ikiambatana na sherehe
za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Rais wa Redio Maria Tanzania Bw. Humphrey Julius
Kira.
Baadhi ya waumini wa Roman Katoliki wakifurahi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania (RMTZ).
Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Rais wa Redio Maria Tanzania, Humphrey Kira
ameiomba Serikali kurekebisha Sheria ya leseni ya redio za jamii ili
ziweze kuwa na vituo vingi vya kurushia matangazo yake.
Hayo yamesemwa leo na Rais huyo wakati
alipokuwa akisoma risala kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya
miaka 20 ya redio hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Msimbazi Centre,
Jijini Dar es Salaam.
Kira amefafanua kuwa redio za kijamii hasa
zilizojikita katika nyanja za kiimani zinasaidia kufundisha maadili na
kufanya wananchi wakomae kiimani, hivyo angefurahi sana kuona redio za
aina hiyo zinapewa leseni za kurusha matangazo yake nchi nzima.
“Ndugu mgeni rasmi, redio yetu inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufinyu wa sehemu za usikivu
(coverage areas) ambapo tatizo hili linatokana na sheria ya leseni za
redio ambayo hairuhusu redio za aina hiyo kuwa na vituo zaidi ya kumi
nchini nzima, tunaomba serikali itusaidie kuiboresha sheria hii ili
tuongeze vituo vya matangazo ya dini”, alisema Kira.
Rais huyo ameongeza kuwa majimbo yote
yanahitaji kufikiwa na huduma za maombi, hivyo anawashauri wasikilizaji
wote kuendelea kuisikiliza redio hiyo kwa njia ya mitandao ikiwemo simu
za mkononi kwani hivi sasa huduma hiyo inapatika nchi nzima.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu
Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa rai
kwa uongozi wa redio hiyo kutobadilisha maudhui wala kuweka vipindi
visivyokuwa vya dini ili iendelee kuunganisha familia na sio kuzigawa
familia.
“Tunasema kuwa redio Maria ni sauti ya
kikristu nyumbani mwako lakini mimi nasema ni sauti ya Mungu ndani ya
familia kwa kuwa inafanya kazi ya kuunganisha familia, vyombo vingine
vya habari vinafanya kazi kubwa ya kuigawa familia lakini Redio Maria ni
tofauti”, alisema Pengo.
Askofu Pengo amewashukuru wananchi wote
waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo kwa kuwa kufanya hivyo ni njia
moja wapo ya kumuenzi na kumpa heshima Mama Bikira Maria.
Nchini Tanzania, Redio Maria ilianzishwa
Aprili 26 mwaka 1996 katika Jimbo Kuu Katoliki la Songea ikiwa na lengo
la kumsaidia Mama Bikira Maria katika kazi yake ya kumtangaza Yesu
Kristo kwa watu wote. Mpaka sasa ina vituo 10 Tanzania Bara na viwili
Zanzibar.
Rais wa Simba, Aveva akitangaza mkutano kuridhia kufanya mabadiliko
Chanzo Mo Blog
Hatimaye ile
ndoto ya mashabiki wa klabu ya Simba kuona klabu yao ikibadili mfumo
unaotumika sasa wa wanachama ndiyo kuwa wamiliki wa klabu na kuingia
katika mfumo wa kampuni imekamilika.
Hilo limethibitishwa na Rais wa Simba, Evans Aveva katika
mkutano mkuu wa Simba ambao ulikuwa unafunga msimu wa 2015/2016 kwa
kutolewa taarifa na kuweka mipango mipya kwa msimu ujao.
Hatua hiyo imekuja baada ya mmoja wa mashabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa makampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji “MO” kutangaza nia ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 na kutoa Bilioni 20 kwa ajili ya kuisaidia Simba kurudi katika makali yake ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri, kocha mzuri, kujenga kiwanja, kuweka vituo vya kukuzia vipaji vya Simba na vingine vingi.
Kutokana na jambo hilo, mashabiki wa Simba walionekana kuvutiwa na mipango ya MO na hivyo kuandamana katika ofisi za klabu na kushinikiza uongozi kukubaliana na MO ili kununua hisa na kuanza kuwekeza ili Simba irudi katika makali ya kushinda mataji.
Ipo hapa video ikimuonyesha Rais wa Simba, Evans Aveva akitangaza mkutano wa Simba kuridhia kufanya mabadiliko.
Hatua hiyo imekuja baada ya mmoja wa mashabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa makampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji “MO” kutangaza nia ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 na kutoa Bilioni 20 kwa ajili ya kuisaidia Simba kurudi katika makali yake ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri, kocha mzuri, kujenga kiwanja, kuweka vituo vya kukuzia vipaji vya Simba na vingine vingi.
Kutokana na jambo hilo, mashabiki wa Simba walionekana kuvutiwa na mipango ya MO na hivyo kuandamana katika ofisi za klabu na kushinikiza uongozi kukubaliana na MO ili kununua hisa na kuanza kuwekeza ili Simba irudi katika makali ya kushinda mataji.
Ipo hapa video ikimuonyesha Rais wa Simba, Evans Aveva akitangaza mkutano wa Simba kuridhia kufanya mabadiliko.
BOHARI LATEKETEA KWA MOTO SINZA LEGO JIJINI DAR JIONI HII
Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa
Bohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili. Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
Bohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili. Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
Bohari linalosadikiwa kuhifadhi vipuri vya magari likiwa
linateketea kwa moto jioni hii Sinza Lego jijini Dar es salaam ambapo
juhudi za kuzima moto zinaendelea japokuwa kazi ya kuzima imekuwa ngumu
kutokana na aina ya vipuri vinavyohifadhiwa katika ghala hilo kuwa aina
ya mipira na mafuta ya vilainishi vya vipuri.
Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo
Mbele
ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto , hapa
wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto
huo
Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua
JAMES LEMBELI NILITOKA CCM KWA SABABU RUSHWA ILIKUWA IMETAMALAKI, UKIHITAJI NIKUSAIDIE NIKO TAYARI
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwenyekiti wa CCM na Mhe
Dk John Pombe Joseph Magufuli akiwa meshikana mikono na Mhe Lembeli
huku akiongozana naye , Lembeli Amesema yuko tayari kurudi CCM wakati
wowote akihitajika kurudi ili kumasidia Rais “Nilitoka CCM kwa sababu
Ruswa ilitamalaki” Lembeli amezungumza hayo mchana wa leo katika
mkutano mkubwa wa hadhara huko mjini Kahama.
Rais Dk. John Pombe Magufuli
akizungumza katika mkutano huo amemwambia Lembeli “Rudi kundini kadiri
utakavyoguswa ili tuijenge nchi kwa sababu huko uliko huwezi kujenga
nchi.
SERIKALI KURASIMISHA MAKAZI HOLELA JIJINI DAR ES SALAAM.
Diwani
Kata ya Kimara Mhe. Pascal Manota akihamasisha wananchi wa Mtaa wa
Mavurunza Kata ya Kimara kushirikiana na Wataalam wa masuala ya Ardhi
ili kuruhu upimaji wa maeneo yao walipofanya mkutano wa uhamasishaji juu
ya Urasimishaji wa Makazi holela.
Kaimu
Mkurugenzi Urasimishaji Makazi holela Bi. Bertha Mlonda akielezea faida
za urasimishaji katika mkutano wa Uhamasishaji kwa wanachi wa Kata ya
kimara mtaa wa Mavurunza.
Badhi
ya wakazi wa Mtaa wa Mavurunza waliohudhuria mkutano wa Uhamasishaji
kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela, wakiwasikiliza viongozi wa
Serikali za Mitaa (Hawako pichani) pamoja na wataalam kutoka Sekta ya
Ardhi walipokuwa wakitoa elimu kwa wakazi hao.
Hamza
Khatibu, Mkazi wa Mtaa wa Mavurunza akiuliza swali kwa viongozi wa
Serikali za Mitaa na wataalam wa Sekta ya Ardhi walipokuwa katika
mkutano kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela.
Alama
inayotenganisha kiwanja kimoja na kingine inayowekwa na wataalam wa
upimaji kutoka Wizara ya Ardhi, wakishirikia na wataalam kutoka Manispaa
ya Kinondoni.
Wataalam
kutoka Wizara ya Ardhi na Manispaa ya Kinondoni wakiandaa ramani za
maeneo ambayo tayari yamefikiwa kwa ajili ya kupimwa na kurasimisha
makazi holela katika Kata ya Kimara, Mtaa wa Kilungule B.
……………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
imeanza kupima viwanja zaidi ya 25,000 kwa wakazi wa kata za Kimara na
Saranga zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kurasimisha
makazi holela.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti Kaimu mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela Bi.
Bertha Mlonda amesema, Uendelezaji Miji ni kwa mujibu wa Sheria ya
MipangoMiji na una faida nyingi kwa wanachi. Alisisitiza kwamba,
Maendeleo ya sehemu yeyote hutokana na miundombinu ya sehemu husika
pamoja na huduma za kijamii zinazopatika.
Mlonda
amewaasa wananchi haswa wa Kata za Kimara na Saranga kutoa ushirikiano
kwa wataalam ambao wameanza kupima maeneo yao ili kuondokana na tatizo
la Makazi Holela kwa wakazi hao kwani upimaji huo utabadilisha taswira
na hadhi ya maeneo yao.
Kwa
sasa Urasimishaji umeanzia katika Kata za Kimara na Saranga, baada ya
hapo yatafuata maeneo yote yenye sifa za urasimishaji katika jiji la Dar
es Salaam, na mikoa yote ya Tanzania. Zoezi hili litakuwa likitekelezwa
kwa awamu kulingana na maeneo yatakavyobainishwa.
RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MKUTANO TINDE, ISAKA NA KAHAMA MKOANI SHINYANGA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa
wakazi wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea Nzega mkoa Tabora.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza jukwaani wimbo
wa kwaya ya Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala
Shinyanga kabla ya Kuhutubia mamia ya wakazi Kahama mkoani Shinyanga.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa
zamani wa Kahama James Lembeli mara baada ya kuwasalimia wananchi
waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais katika viwanja hivyo vya Kahama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Isaka mkoani Shinyanga.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na
Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa Chadema
mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na
Wanakwaya wa Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala
Shinyanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano Kahama mjini mkoani
Shinyanga.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada
ya kuoneshwa picha na kijana mmoja aliyeishika picha hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Tinde mkoani Sinyanga.
PICHA NA IKULU
DK MNDOLWA AIBUKA KIDEDEA GOLF LUGALO
Dk
Edmund Mndolwa mshindi wa Jumla kwa mwezi July baada ya kuibuka na
Ushindi wa Mikwaju ya Jumla (Gross) 87 katika mashindano yaliyofanyika
jana katika Viwanja vya Golf Lugalo Jijini Dar es salaam.
Dk Edmund Mndolwa mshindi wa Jumla kwa mwezi July baada ya kuibuka na
Ushindi wa Mikwaju ya Jumla (Gross) 87 akipiga mkwaju wa mwisho katika
mashindano yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Golf Lugalo Jijini Dar
es salaam.
Mshindi
wa kwanza kwa Wanawake Victoria Elias Akijiweka sawa huku Mwezie Chiku
Elias akimshuhudia wakati wakimenyana katika mashindano ya Kila mwisho
wa mwezi katika Klabu ya Lugalo ya Nmb Monthly Mug.
Mshindi
wa kwanza kwa Wanawake Victoria Elias Akijiweka sawa kupiga mpira wa
Mwisho wakati wakimenyana katika mashindano ya Kila mwisho wa mwezi
katika Klabu ya Lugalo ya Nmb Monthly Mug.
Afisa
wa Habari kutoka JWTZ Luteni Selemani Semunyu akitoa Zawadi kwa
Mshindi wa Kwanza kwa Watoto (Junior) Zuwena Hamisi mara baada ya
Kumalizika mashindano ya mwezi July (Monthly Mug )yaliyofanyika jana
katika Viwanja vya Golf Lugalo Jijini Dar es salaam.
Wachezaji
Golf Chipukizi wakijiweka sawa wakati wa mashindano ya kila mwisho wa
Mwezi ambapoi kwa mwezi July yalifanyika jana katika Viwanja vya Golf
Lugalo Jijini Dar es salaam.
(Picha na Selemani Semunyu).
FREEMAN MBOWE AJIPELEKA POLISI LEO
Mwenyekiti
wa Chama Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe akiongozana na baadhi ya
Wajumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa, John Mnyika, Mkiti wa Baraza la
Wazee Hashimu Issa Juma na Mwanasheria Mkuu wa Chama Tundu Lissu,
wakiwasili Kituo Kikuu cha Polisi (Central) Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, ambapo Mwenyekiti Mbowe ameitikia wito wa jeshi hilo kupitia wa
ZCO Wambura wa kumhitaji afike hapo leo.
NANI KASEMA SIASA NI UADUI, HEBU ANGALIA WENYEWE WANAVYOPIGA STORI
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa
CCM Taifa Mh. Nape Nnauye na Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa
Chama cha CHADEMA wakijadiliana jambo wakati alipokutana katika shughuli
ya kuaga mwanahabari Mpiga Picha Marehemu Joseph Senga aliyefaiki
mwishoni mwa wiki hii Nchini India alikokuwa akitibiwa maradhi ya moyo
shughuli hizo za kuaga mwili wa Marehemu Joseph Senga zimefanyika Sinza
na mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda wilayani Kwimba mkoani Mwanza
kwa mazishi.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa
CCM Taifa Mh. Nape Nnauye akizungumza na Mh. Edward Lowasa Waziri Mkuu
wa Zamzni na kada wa CHADEMA katikati kushoto ni Kada mwingine wa
CHADEMA Ndugu Khamis Mngeja.
BFA YAPATA VIONGOZI WAPYA WA MIAKA MINNE IJAYO
Mwenyekiti
mpya wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Bagamoyo(BFA) Alhaj Abdul
Sharif ,wa katikati kati ya waliokaa ,akiwa na viongozi wenzake wa chama
hicho ,waliochaguliwa mapema mwishoni mwa wiki iliyopita.(Picha na
Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti
mpya wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Bagamoyo(BFA)alhaj Abdul
Sharif ,akizungumza na wajumbe wa chama hicho baada ya uchaguzi wa chama
hicho ambapo kilipata viongozi wapya watakaoongoza kwa miaka minne
ijayo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
CHAMA
cha mpira wa miguu ,wilayani Bagamoyo,mkoa wa Pwani,( BFA) kimechagua
viongozi wapya wa chama hicho wataokingoza katika kipindi cha miaka
minne .
Uchaguzi huo umefanyika kihalali ,kwa mujibu wa sheria ambao ulihudhuliwa na wajumbe 91.
Katika
uchaguzi huo alhaj AbdulZahoro Sharifu alichaguliwa kuwa mwenyekiti kwa
kipindi kitakachoishia mwaka 2020 kwa kupata kura 77.
Alhaj
Sharif alipata ushindi huo kwa kupata kura hizo dhidi ya mpinzani wake
Kitomu Yona aliyepata kura 11 huku nafasi ya makamu mwenyekiti
alichaguliwa Shaabani Makelele ambae hakuwa na mpinzani.
Nafasi
ya katibu mkuu imenyakuliwa na John Fransis Bolizozo “Boli Kubwa”
aliyejipatia kura 81 na kumwacha mbali mgombea mwenzie kwenye nafasi
hiyo Yona Mkawa aliyejinyakulia kura 4.
Katibu
msaidizi alishinda Jitihada Omary kwa kura zote kutokana na kuwa peke
yake ,mhazini alichaguliwa Ornjurie Marigwa ambae hakuwa na mpinzani
msaidizi ikienda kwa Salumu Kanuti aliyejikusanyia kura 88.
Mjumbe
mkutano mkuu wa mkoa alichaguliwa kipa wa zamani wa nyota nyekundu na
kocha mzawa hapa nchini Shekhe Abdallah aliyepata kura 45 dhidi ya kura
43 alizopata Mzee Minjoli.
Nafasi
ya mwakilishi wa vilabu akichaguliwa Jabir Omary aliyeshinda kwa kura
46 akimwacha mgombea mwenzake Ally Jakaya aliyepata kura 44.
Wajumbe
kamati ya utendaji na kura zao katika mabano waliochaguliwa ni
Ramadhani Mape (77), Rajabu Maliki (80), Maneno Kidobe (68), Shabani
Masimbi (69) na Peter Nyambasi (39).
Katika
uchaguzi huo uliongozwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wilaya
Mwinyi Akida, mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shaabani Kangale
“Machokodo” na diwani wa kata ya Kiwangwa Hussein Malota Kwaga.
Baada
ya kutangaza matokeo hayo Akida aliwataka viongozi hao kuhakikisha
wanawatumikia ipasavyo wana-Bagamoyo ili mpira uchezwe maeneo yote.
Alieleza
kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kukidhi kiu ya wana michezo ambao kwa
muda mrefu hususan ukanda wa Chalinze na maeneo mengine wilayani humo
ambao wamekosa fursa hiyo.
Nae
mwenyekiti mpya wa BFA ,Abdul Sharif, alitoa rai kwa viongozi wengine
wa chama hicho kuhakikisha kila mmoja anajitoa kwa hali na mali ili
kuinua sekta ya michezo wilayani humo.
Alhaj
Sharif aliahidi kupatikana kwa timu itakayocheza ligi kuu ya Vodacom
Tanzania Bara katika kipindi cha miaka minne ambacho watakiongoza.
KWA HERI MPIGANAJI JOSEPH SENGA, MUNGU AIWEKE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI
Wapiga
picha wakibeba jeneza la marehemu Joseph Senga aliyekuwa mpiga picha wa
gazeti la Tanzania Daima ili kuliweka kwenye tayari kwa safari ya
kwenda Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kwa mazishi wanaoongoza mbele
katikati ni Rafiki yake Mkubwa Deus Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la
Mtanzania aliyeshika Msalaba , kulia aliyeshika Shada la maua ni John
Bukuku mpigapicha na Mkurugenzi wa Blog ya Fullshangwe na kushoto
aliyeshika picha ya marehemu ni Joachim Mushi mpiga picha na Mkurugenzi
wa Mtandao wa The Habari akiwa pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mablogger
Tanzania TBN wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Sinza jijini
Dar es salaam.
Deus
Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania kulia Mpiga Picha Loveness
aliyekuwa mfanyakazi mwenzake na marehemu kwenye kampuni ya Free Media
inayoendesha gazeti la Tanzania Daima na Mpiga Picha Halima Kambi kutoka
Guardian wakiwa wamebeba mashada ya maua na msalama.
Deus
Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania akiaga mwili wa marehemu
Joseph Senga na kushoto ni Mpiga Picha mkongwe Juma Dihule.
Carthubert Kajuna Mpiga Picha na Mkurugenzi wa Blogu ya Habari na Matukio akiaga mwili wa marehemu Joseph Senga.
Mpiga Picha wa Gazeti la Habari leo Robert Okanda akiaga mwili wa marememu.
Mpiga picha Muhidin Sufiani akitoa hesgima zake za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
Baadhi ya wapiga picha wakijadiliana mambo kadhaa.
Mpiga Picha wa Jambo Leo Dotto Mwaibale akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
Waziri Mkuu wa zamani Edward
Lowasa akiongozana na Nape Nnauye Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
Waziri Mkuu wa Zamani Edward
Lowasa akijadiliana jambo na Nape Nnauye Waziri wa Habari , Utamaduni ,
Sanaa na Michezo wakati walipoongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa
mwanahabari Marehemu Joseph Senga
MKUU WA WILAYA YA ILALA AUNGANA NA WATENDAJI WAKE KUSAMBAZA MAPIPA YA KUWEKEA TAKA BARABARA YA KIVUKONI DSM
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akiongozana na Edward Mpogolo
Katibu Tawala wa wilaya hiyo wakati walipoongoza zoezi la kusambaza
mapipa ya kuwekea takataka kwenye barabara ya Kivukoni jijini Dar es
salaam kwa ajili ya udhibiti wa utupaji wa taka hovyo.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema katikati akiongozana na Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala Bw.Msongela Palela kushoto pamoja na Edward
Mpogolo Katibu Tawala wa wilaya hiyo weka mapipa ya kuhifadhia takataka
katika barabara ya Kivukoni jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akiongozana akimuelekeza jambo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala juu ya mpangilio wa uwekaji wa mapipa ya
kuhifadhia takataka kwenye barabara ya Kivukoni jijini Dar es salaam
jana.
KOKA:AWAASA WALIMU WAKUU NA WATENDAJI KUTUNZA MADAWATI YA MISAADA
MBUNGE
wa jimbo la Mji wa Kibaha,Silvestry Koka wa kushoto akikabidhi madawati
537 yenye thamani ya zaidi ya mil. 37 yaliyotolewa na serikali ikiwa ni
mgao wa wabunge nchini kwenye sehemu ya posho zao,kwa afisa elimu wa
halmashauri ya Mji huo ,Maajabu Mkanyemka aliyemwakilisha mkurugenzi wa
halmashauri hiyo Jennifer Omolo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MBUNGE
wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka ,amewataka walimu wakuu wa
shule za msingi na watendaji wa mitaa na kata katika halmashauri ya Mji
huo, kusimamia na kuhakikisha wanayatunza madawati mapya yanayotolewa na
wadau mbalimbali ili kuondoa tatizo la ubaha wa madawati mashuleni.
Amesema mwalimu mkuu ama mtendaji ambae atazembea kusimamia suala hilo basi atawajibishwa .
Koka
aliyasema hayo ,wakati akikabidhi madawati 537 yenye thamani ya zaidi
ya mil. 37 yaliyotolewa na serikali ikiwa ni mgao wa wabunge nchini
kwenye sehemu ya posho zao .
Alieleza
kuwa serikali haitakuwa tayari kuona madawati yanayotolewa na
wahisani,wadau na yale yaliyotengenezwa na wadau hayafuatiliwi wala
kupewa matunzo.
“Ni
wajibu wa kila mtendaji,walimu na wanafunzi wenyewe kuwa wasimamizi
kutokana na fedha zilizotumika ni kodi za wananchi hivyo lazima zilindwe
kwa faida ya watoto hao “alisema Koka.
Aidha
Koka alisema awali wanafunzi walikuwa wanapata shida na kero wakati wa
kusoma ambapo wengine walikuwa wakikaa chini na kuchafuka kwa vumbi na
kuandikia chini hivyo kushindwa kupata elimu yao kwenye mazingira yasiyo
bora.
Alisema
serikali ya awamu ya tano chini ya rais John Magufuli ,iliona iweke
mkakati madhubuti wa kuchangia madawati na viti na meza katika shule za
msingi na sekondari ili kuondoa kero ya upungufu uliokuwepo miaka ya
nyuma.
Koka
alisema kuwa ni jambo la lazima na sio hiari kwa walimu wakuu kuwa moja
ya wakaguzi na wasimamizi wakuu wa madawati hayo ili hata kama yatakuwa
yameharibika kidogo yatengenezwe na si kuyaacha hadi yaharibike .
Nae
mwakilisha wa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha Jennifer
Omolo,afisa elimu wa halmashauri ya Mji huo,Maajabu Mkanyemka alisema
kabla ya agizo la rais kulikuwa na mahitaji ya madawati 9,162.
Alieleza hadi kufikia June 30 walikuwa tayari wametengeneza na kukarabati madawati 6,979 hivyo kwasasa wana upungufu wa 2,183.
Maajabu
alisema hadi sasa madawati yaliyopatikana ni 2,500 kati ya mapungufu
ya 2,183 huku 572 yakiwa yanatengenezwa na mara yatakapokamilika
kutakuwa na ziada ya madawati 312 hivyo kutarajia tatizo la madawati
kubaki historia mjini hapo.
Alisema katika upande wa shule za
sekondari mahitaji ya meza yalikuwa 7,032 vilivyopo ni 6,041 na kubakia
na upungufu wa meza 991 huku viti walivyokarabati na kutengeza ni viti
6,099 kukiwa na upungufu wa viti 933 hadi sasa.
TBL Group family day 2016 yafana vilivyo
Mkurugenzi
Rasiriamali watu wa TBL Group David Magesa (kushoto) akimkabidhi Mercy
Maliwa zawadi kwa kuibuka mshindi wa shindano la mpango wa AfyaKwanza ,
wakati wa wa Siku ya wafanyakazi wa kampuni hiyo (Family Day)
iliyofanyika kwenye viunga vya hoteli ya Fun City Kigamboni jijini Dar
es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakisafishwa kucha za miguu pamoja na kupakwa rangi kwenye burudani za siku ya familia
Wototo wa wafanyakazi walicheza michezo mbalimbali
Watoto wakiweza kujibu maswali ya ufahamu na kujishindia zawadi
Zoezi la Afya Kwanza lilitekelezwa kwa vitendo
Baadhi ya wafanyakazi na famÃlia zao wakipata misosi
Baadhi ya wafanyakazi na famÃlia zao wakipata misosi
Wana msondo wakimwaga burudani kwa wafanyakazi wa TBL Group
Msanii maarufu wa vichekesho Joti alikuwepo kumwaga burudani
Burudani tele za muziki zilikuwepo
NAIBU WAZIRI MPINA AZITAKA RADIO ZA JAMII KUHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
(katikati) akiangalia samaki katika soko ya wilaya ya Masasi akiwa
katika ziara yake ya usafi na ukaguzi wa mazingira mjini Masasi, (kilia)
ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bw. Selemani Mzee.
Aliyeinama
katikati akikusanya uchafu ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika zoezi la usafi
wa mazingira Wilayani Masasi mwishoni mwa wiki.
Bw.
Benjamini Elias (kulia) Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Masasi
akitoa taarifa na maelezo ya hali ya usafi wa soko la mji wa Masasi kwa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina
(kushoto), wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira mjini Masasi.
(PICHA NA EVELYN MKOKOI)
……………………………………………………………………………………………
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amezitaka
Radio za jamii kuhamasisha usafiri wa mazingira nchini. Naibu Waziri
Mpina ametoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki siku ya usafi kitaifa,
mwishoni mwa wiki wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Akitolea Mfano wa Radio Pride FM
ya Mjini Mtwara yenye kupatikana katika frequencies 87.8 mjini Mtwara,
ambayo imeanzisha kampeni ya usafi katika mkoa wa mtwara na wilaya zake
kwa kufanya vipindi vya moja kwa moja na kutembelea wilaya za mkoa huo
kufanya usafi wa mazingira kwa vitendo.
Kwa Upande wake Bw. JUma Andrea
Manager uzalishaji wa kituo hicho cha Radio, alisema kuwa lengo kubwa la
kituo hicho kuhamasiha usafi ni kuunga mkono agizo la Mhe. Rais kwa
kuwaweka pamoja wananchi, kuweka muamko na hamasa ili kujenga tabia ya
kupenda usafi na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea
mfano ugonjwa wa homa ya matumbo na kipindipindu.
Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa
Mtwara katika majumuisho ya ziara yake Wilayani Masasi, Naibu Waziri
Mpina aliwataka viongozi wa mkoa huo kuunda sheria ndogondogo za
mazingira zitakazo watoza faini wananchi waharibifu wa mazingira mkoani
humo, na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na hali ya wananchi
ili waweze kujifunza na kujijengea tabia ya usafi.
“Nimeona kuwa uchomaji moto
misitu ovyo hapa kwenu umekithiri, uchomaji moto taka nao siyo njia
nzuri ya uondoshwaji wa taka,hiyo kuwe na miondombinu rafiki kwa
uondoshwaji wa taka, na kiongozi wa mkoa ambae hatakuwa tayari
kushughulikia usafi wa mazingira na yeye awe tayari kushughulikiwa
alisisitiza.”
Ziara ya Naibu Waziri Mpina
Mkoani Mtwara ni muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa viwanda
na usafi wa mazingira iliyohusisha pia ukaguzi wa machinjio ya mji wa
Masasi.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI ATEMBELEA MAENEO YA HIFADHI YA MISITU NA WANYAMAPORI YENYE MIGOGORO MBALIMBALI MKOANI TABORA
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akisaini kitabu cha
wageni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo alifanya ziara ya
kikazi ya siku nne na kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi ya Hifadhi
ya Misitu na Wanyamapori yenye migogoro. Maeneo hayo ni Hifadhi ya
Msitu wa Wembere (Wilaya ya Igunga), Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Isawima (Wilaya ya Kaliua), Eneo la Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole
(Wilaya ya Skonge), Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi (Wilaya ya Skonge)
na Msitu wa hifadhi wa Ilomero (Wilaya ya Nzega).
Naibu
Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani akizungumza na baadhi ya wananchi
waliovamia Msitu wa Hifadhi wa Wembere Wilayani Igunga hivi karibuni.
Aliwataka wananchi hao kutii sheria za nchi na kusubiri maelekezo ya
Serikali ambapo aliwaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga na
Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kukusanya taarifa mbalimbali
zinazohusu hifadhi hiyo na vijiji jirani ambapo zitatumika kumaliza
mgogoro huo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi
wa waliovamia Msitu wa Wembere na kuweka makazi, Wilayani Igunga hivi
karibuni. Alitoa maelekezo mbali kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya
na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania kwa ajili ya kukabili changamoto
zilizopo katika hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya ya Igunga pamoja na viongozi wengine kutoka Mamlaka ya
Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto)
akikagua maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Isawima Wilayani Kaliua hivi
karibuni. Hifadhi hiyo ambayo imetengwa na vijiji 11 kwa ajili ya
kuanzishwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima umevamiwa na
wananchi kutoka maeneo ya nje ya vijiji hivyo na kuweka makazi, mifugo
na kilimo jambo lililoikwamisha jumuiya hiyo kupewa kibali cha
kurasimishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii. Eng. Makani
alitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya ya Kaliua na Halmashauri kutumia
mamlaka ya kisheria
waliyo nayo kuwahamisha wavamizi hao ili jumuiya hiyo iweze kuanzishwa.
waliyo nayo kuwahamisha wavamizi hao ili jumuiya hiyo iweze kuanzishwa.
RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NZEGA MKOANI TABORA.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Mkoani Tabora Mhashamu
Paulo Ruzoka mara baada ya Kuwasili Nzega mkoani Tabora jana kwa ajili
ya ziara ya kikazi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Tabora Al-Haji Ramadhani Rashid
katika viwanja vya Stendi ya Nzega kabla ya kuhutubia mamia ya wakazi
wa Nzega.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
mamia ya wananchi katika viwanja vya Stendi ya Nzega wa mkoani Tabora
jana.
PICHA NA IKULU
Wadau wa Sanaa nchini wahamasishwa kudhamini na kufadhili Mashindano ya Urembo bila ubaguzi.
Miss
Dar Indian Ocean aliyemaliza muda wake, Camilla John (katikati)
akimvisha skafu Mshindi wa Mashindano ya Miss Tanzania Indian Ocean 2016
Jackline Kimambo (kushoto) mara baada ya kuibuka mshindi katika
mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Miss
Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo (aliyekaa katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na warembo wenzie ambaye ni Mshindi wa pili na wa
tatu mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30
Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkuregenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Bw. Francis Songoro (kulia) akimpongeza Miss Tanzania
Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo kwa kuibuka mshindi wa mashindano
hayo baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai,
2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Miss
Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kumalizika kwa mashindano hayo
yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni
jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………..
Na. Benedict Liwenga-WHUSM.
Wadau
wanaojishughulisha na masuala ya Sanaa nchini wamehamishwa kujitokeza
kwa wingi katika kusaidia maendeleo ya Sanaa kwa kudhamini na kufadhili
mashindano ya urembo bila kubagua.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.
Francis Songoro wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Mhe. Anastazia Wambura ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi
katika Mashindano ya Miss Tanzania Indian Ocean 2016 yaliyofanyika
katika Ukumbi wa MRC uliopo Mikocheni jijini hapa.
Akiwasilisha
hotuba hiyo, Songoro amesema kwamba kazi inayofanywa na wadau wa sanaa
ni hatua ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni ambayo inasisitiza
jamii na wakuzaji sanaa kuendeleza ubunifu katika kazi za kiutamaduni.
Ameeleza
kuwa, Serikali kupitia Wizara yake inathamini na kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na wadau hao hasa katika kukuza na kuviendeleza vipaji vya
vijana nchini, hivyo amewapongeza wadau hao kwa moyo wao wa kujitoa na
kuwataka kuendeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997
katika Sura ya 9 kifungu cha 9:5:8 ambacho kinasisitiza na kuhimiza
watu binafsi pamoja na Mashirika kuwekeza rasilimali katika sekta ya
utamaduni.
‘’Maonyesho
haya ni ishara tosha kuwa sanaa ni kazi, ajira, biashara na burudani,
hivyo kipekee nawapongeza sana’’, alisema Songoro.
Aliongeza
kuwa, Warembo ambao wameshiriki katika mashindano hayo wanautangaza
utalii wa ndani na nje ya nchi na kwa kufanya hivyo wanaiwakilisha vyema
Tanzania Duniani katika mashindano ya Miss World na pia kukuza uchumi
wa nchi.
Aidha,
amewataka warembo ambao hawakubahatika kuibuka washindi katika
mashindano hayo kutokata tamaa, bali waitumie fursa hiyo hususani ya
elimu waliyoipata wakiwa kambini kwa kuisadia jamii inayowazunguka na
kuwa wanawake wa mfano wa kuigwa katika kujitambua na kujiamini.
‘’Mtambue
kwamba, siyo wote mtakaoibuka washindi na kuendelea mbele katika
mashindano haya, niwaombe wale ambao hamtashinda msivunjike moyo, bali
mkaitumie elimu mliyoipata na yale ambayo mmejifunza mkiwa kambini kwa
kuisaidia jamii inayowazunguka na muwe wanawake wa mfano wa kuigwa’’,
alisema Songoro.
Katika
mashindano hayo, Mshindi wa Kwanza aliyeibuka na kunyakua taji hilo ni
Jackline Kimambo ambaye alipatikana kati ya tano bora na kuvikwa taji
la Miss Tanzania Indian Ocean 2016 na Mshindi wa pili ni Regina Ndimbo
huku wengine waliobaki kwenye tano bora wamepata fursa ya kuingia katika
mashindano ya Miss Kinondoni.
Shindano
hilo lilihusisha jumla ya washiriki wapatao 20 ambapo mmoja kati yao
ndiyo aliyeibuka mshindi na lilidhaminiwa na wadau mbalimbali wakiwemo
Mikocheni Resort Centre, Mlimani TV, Channel Ten, Darling, Helmic,
Tanzania Breast Cancer Foundation, Magic FM, Jozi Lounge, Kiss Printers
pamoja na NTS.
JPM AKOSHWA NA DC WA IGUNGA JOHN MWAIPOPO, AAMURU STENDI YA BASI NA SOKO VIANZE KAZI JUMATATU
Rais
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga
Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na
Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara
mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana
mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya
basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo
limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu
badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na
kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani
ambako nako pia wana sehemu za Biashara.
Rais Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe
John Mwaipopo wakati akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria
na Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa
hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
Mkuu
wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt.
Magufuli kuhusiana na Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru
huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. Rais ameitaka SUMATRA
ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi Jumatatu. Pia ameiagiza
halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu
za biashara bila kuzitumia katika soko jipya wathibitiwe mara moja.
Wananchi
wa Igunga wanalipuka kwa furaha na Mzee huyu anatoa noti ya shilingi
10,000/- akitaka kumtuza Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua
changamoto za Stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri
wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo
Jumamosi Julai 30, 2016
Rais
Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele
wa grade One kutoka uongozi wa wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake
wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
PICHA NA IKULU
SINAI MISSIONS INTERNATIONAL (SMI) YAFANYA MKUTANO WAKE MKUU WA MWAKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA
Mgeni
rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Bishop Dr
Kameta (katikati) akizungumza na wanachama wa Shirika la kidini
linalotoa huduma kwa makanisa na mashirika yanayofanya kazi ya kueneza
injili ulimwenguni lijulikanalo kama SINAI MISSIONS INTERNATIONAL(SMI)
wakati wa mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika jijini Dar es Salaam Lengo
la mkutano huo ilikuwa ni kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila
huduma chini ya mwavuli wa SMI. kulia ni Rais wa shirika hilo
Ing.Bishop Piter M.Sanga.na kushoto Katibu Mkuu anaemaliza muda wake
Bishop Pite W.Chinyama kutoka Zambia.na Mweka Hazina anayemaliza muda
wake Msh Raphael Muhagama kutoka Tanzania.
Wajumbe wa Mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wakifuatilia mada mbalimbali.
Viongozi
wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio wakati wa mkutano mkuu wa mwaka
kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa
SMI.
Wajumbe wa mkutano wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio.
Wajumbe
wa mkutano mkuu wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio wakati wa mkutano
mkuu wa mwaka kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini
ya mwavuli wa SMI.
Mgeni
Rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Bishop Dr Kameta
(kushoto), pamoja na Mtafisiri ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirika la
MSI, Bishop Gilibert Biyengo.wakihutubia Mkutano Mkuu wa Mwaka.
Mgeni
rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekosite, Bishop Dr Kameta
(kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa
SINAI MISSIONS INTERNATIONAL(SMI) uliofanyika jijini Dar es Salaam
kwaajili ya kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya
mwavuli wa SMI.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
MAKOCHA TANZANIA WAANZA KUIVA
Makocha
20 wa Tanzania wanaofanya kozi ya Leseni A kutoka Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF), wamemaliza kozi hiyo hatua ya kwanza na kusema,
“Tumenolewa na sasa tumeiva vya kutosha,” amesema mmoja wa wanafunzi
hao, Wilfred Kidao leo saa Julai 30, 2016 wakati Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Kidao amesema japo kozi hiyo
ilikuwa hatua ya kwanza ‘Module 1’ kwa sasa wameiva kiasi kwamba
watakapomaliza Novemba, mwaka huu wana uhakika wa kupeleka vyeti vyao
sehemu yoyote duniani kuomba kazi na kushinda kwa kuwa wameiva vilivyo.
Wakufunzi wa kozi hiyo walitokea CAF, Sunday Kayuni na Salum Madadi
ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.
Baada ya kusikiliza kauli hiyo ya
Kidao, Rais wa TFF Jamal Malinzi moja kwa moja akawasisitiza makocha
hao kufanya kazi kwa juhudi na kuwaeleza kuwa hatua waliyofikia ni kubwa
kwa kuwa baadhi ya makocha kutoka nje hawana vyeti na kukosa sifa ya
kufundisha timu kubwa ikiwamo timu za mataifa ngazi mbalimbali.
Rais Malinzi alitaka makocha hao
kuangazia mpira wa miguu kwa wavulana wengi wakiwa wanatokea katika
mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel pamoja na soko
la wasichana ambalo kwa sasa linashika chati kila kona ya dunia.
Naye, Makamu wa Rais wa TFF,
Wallace Karia alimpongeza Rais Malinzi kwa namna anavyoratibu na
kuzikubali kozi mbalimbali za waamuzi na makocha. “Kwa muda mrefu au
tuseme kwa miaka mingi hakujafanyika kozi nyingi kama kipindi cha
uongozi wako ukisaidiana na mimi pamoja na kamati nzima ya utendaji
pamoja na sekretarieti.”
“Fanyeni utafiti ninyi makocha.
Utaona kuwa sehemu kubwa nchi za Afrika zimefanikiwa kwa kutumia makocha
wazawa. Leo ninyi ni makocha wa ngazi ya juu kabisa hivyo mna uwezo wa
kufanya vema na kusaidia timu zetu na timu za taifa,” alisisitiza Karia.
MKWASA AAHIRISHA KAMBI TAIFA STARS
Kutokana
na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka
kuandaa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu
Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa
kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu,
imefahamika.
Wachezaji ambao Mkwasa amewaita
wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi
ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC.
Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa
anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya
kirafiki wa klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania
Bara (Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi
Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda
Nigeria.
Taifa Stars ina mchezo na jijini
Lagos, Nigeria Septemba 2, 2016 ambao ni wa kukamilisha ratiba katika
kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad kujitoa. Wachezaji
ambao Mkwasa aliwaita mapema wiki hii ni:
Makipa:
Deogratius Munishi
Aishi Manula
Benny Kakolanya
Mebeki:
Kelvin Yondani
Aggrey Morris
Oscar Joshua
Mohamed Husein ‘Tshabalala’
Juma Abdul
Erasto Nyoni
Viungo:
Himid Mao
Mohamed Ibrahim
Shiza Kichuya
Jonas Mkude
Ibrahim Jeba
Mwinyi Kazimoto
Farid Mussa
Juma Mahadhi
Hassan Kabunda
Washambuliaji:
Simon Msuva
Joseph Mahundi
Jamal Mnyate
Ibrahim Ajib
John Bocco
Jeremia Juma
MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAWASILI DAR, KUAGWA JUMAPILI VIWANJA VYA SINZA-UZURI
Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili
Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa
Othmani
Michuzi,(kulia). wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa
Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na
marehemu Senga
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili
Mbunge
wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri
Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel
Nderumaki wakati wakisubiri mwaili wa marehemu Senga kuwasili
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta
jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena,
wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa
mpiga picha mkuu wa gazeti hilo
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo
Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka
RAIS DKT. MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA YAKE KATIKA WILAYA ZA IGUNGA NA NZEGA MKOANI TABORA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na mamia ya wakazi wa Igunga mkoani Tabora katika ziara yake ya kikazi
katika Mkoa huo wa Tabora.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani
hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani
hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani
hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani
hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Ndugu
Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea
Nzega Mkoani Tabora.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wakazi wa Ziba Wilayani Igunga mkoani Tabora hawaonekani
pichani wakati akielekea Nzega Mkoani Tabora.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
wabunge wa Mkoa wa Singida wakati akiwahutubia wakazi wa Misigiri Mkoani
Singida wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wakazi wa Misigiri Mkoani Singida. PICHA NA IKULU
AfDB YAAHIDI KUENDELEA KUIPIGA JEKI TANZANIA KUKUZA UCHUMI WAKE
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) akiwa kwenye
majadiliano na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
Dkt. Frannie Leutier (katikati) na Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi.
Tonia Kandiero.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akifafanua jambo mbele ya
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie
Leutier, kulia kwa Dkt. Leutier, ni Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi.
Tonia Kandiero na watendaji wa Wizara.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, akitoa ufafanuzi kuhusu
vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano kwa Makamu wa Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie Leutier (Hayupo pichani).
Mwakilishi
mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero (wa kwanza kushoto) akitoa
ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango. Kutoka
kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB )
Dkt. Frannie Leutier, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (anayeandika)
Makamu
wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie Leutier
akitoa ufafanuzi wa namna ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo
ambapo benki hiyo imewekeza Dola za Marekani Bilioni 2 hadi sasa nchini
Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Makamu wa Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie Leutier.
Makamu
wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie Leutier
akisoma jambo kwenye kompyuta ndogo wakati akieleza jambo kwa Mhe.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipomtembelea na
kufanya mazungumzo naye ofisini kwake Jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………………………
Na Benny Mwaipaja,MoFP
Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leautier,
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo ameishukuru Benki hiyo kuwa
mojawapo ya mashirika ya kimataifa yanayoisaidia Tanzania katika sekta
mbalimbali za maendeleo.
Benki hiyo imewekeza hapa nchini
kiasi cha dola Bilioni 2 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 4.4 kama
ruzuku na mikopo yenye riba nafuu ili kuendeleza sekta mbalimbali
ikiwemo barabara, elimu, kilimo, nishati ya umeme, na viwanda.
Katika mazungumzo hayo Mhe. Dkt.
Mpango, ameelezea kufurahishwa kwake na Dira ya AfDB ambayo inafanana na
vipaumbele vya serikali, kupitia Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo
wa miaka mitano ambao umelenga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda
ifikapo mwaka 2025.
Dira ya Benki hiyo imejikita
katika malengo matano ambayo ni kuwekeza katika nishati ya umeme,
uzalishaji wa chakula, kuendeleza viwanda, kuiunganisha Afrika kwa
mtandao wa barabara na kuboresha maisha ya watu.
Mhe. Dkt. Mpango, amesema kuwa
uwekezaji katika sekta hizo utasaidia mpango mkubwa wa uboreshaji wa
miundombinu kama vile kujenga viwanda kwa kuhusisha sekta ya umma na
binafsi-PPP, umeme wa kutosha kuendesha viwanda, barabara ambazo
zitaunganisha nchi zote za Afrika.
“AfDB wametusaidia sana katika
ujenzi wa barabara nyingi nchini Tanzania ikiwemo barabara ya kutoka
Tanga kwenda Horohoro, ambayo imerahisisha usafiri wa kwenda nchini
Kenya. Barabara nyingine zitajengwa kutoka mpakani Kagera kupitia
Kigoma kwenda Katavi, Dodoma hadi Iringa. Hili ni jambo kubwa” Alisema
Dkt. Mpango
Dkt. Mpango amemweleza Makamu
huyo wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Frannie
Leautier juu ya mpango wa serikali wa kuimarisha sekta ya usafirishaji
ikiwemo kujenga Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (standard gauge)
ambapo kiasi cha shilingi Trilioni 16 kinahitajika kukamilisha mradi
huo.
Ameeleza kuwa tayari serikali
imetenga kiasi cha shilingi Trilioni 1 katika bajeti yake ya mwaka huu
2016/2017 kwaajili ya kuanza kutekeleza mradi huo mkubwa unaohusisha
njia ya reli yenye urefu wa kilometa 2,190.
Ameitaja Sekta nyingine ya
kipaumbele kuwa ni kilimo kwaajili ya kuzalisha chakula kwa wingi
kwaajii ya kutosheleza matumizi ya ndani na ziada yake kuuzwa nje ya
nchi huku ikitiliwa mkazo uzalishai wa malighafi zitakazotumika katika
viwanda.
Katika mazungumzo hayo Waziri wa
Fedha na Mipango alimpongeza Dkt. Leautier, ambaye ni raia wa Tanzania,
kwa kupata nafasi ya Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
AfDB, kuwa ni faraja na kielelezo kizuri kwa akina mama wa Kitanzania
kuwa wanaweza.
Kwa upande wa Makamu wa Rais wa
AfDB Dkt. Frannie Leautier Dkt. Leautier, ambaye aliambatana na
Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo hapa nchini, Bi. Tonia Kandiero, amesema
kuwa AfDB imesaidia na itaendelea kusaidia miradi mingi ya maendeleo
hapa nchini ikiwemo ya barabara, elimu, kilimo, afya, sekta ya umeme ili
Tanzania iwe na umeme wa kutosha kuendesha viwanda.
“Kwa kufanya hayo uchumi wa nchi
utaimarika, vijana watapata ajira, wananchi watakuwa na maisha bora,
chakula kitazalishwa cha kutosha na kingine kuuzwa nje ya bara la
Afrika, Viwanda vitasaidia sana kiumarisha uchumi wa nchi kwani bila
viwanda ni vigumu sana kuendelea” alisema Dkt. Leautier
Ameahidi kuwa Benki yake
itaendelea kusaidia kuinua sekta ya kilimo kupitia Benki ya Maendeleo ya
Kilimo kwa kutoa mkopo wenye masharti nafuu ili kuwawezesha wakulima
wakubwa, wa kati na wadogo kupata fursa ya mikopo hiyo itakayosaidia
uzalishaji wa mazao.
Dkt. Leautier amesema kuwa
atawasilisha kwenye bodi ya benki hiyo wazo la Tanzania kutaka kupigwa
jeki katika ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa kwa kuwa
mradi huo utakuwa na manufaa makubwa si tu kwa Tanzania, bali kwa nchi
zote zinazoizunguka zikiwemo zile ambazo hazina bahari.
“Mradi huo ukikamilika utasaidia
pia kunusuru barabara ambazo zimekuwa zikiharibika kutokana na
kupitishwa mizigo mingi mizito ambayo ingefaa kusafirishwa kwa njia ya
reli ili kuzifanya barabara hizo zidumu muda mrefu” aliongeza
Benki ya Maendeleo ya Afrika
AfDB, kupitia mfuko wake wa Maendeleo-African Development Fund (ADF),
imeahidi kutoa kiasi cha Dola Milioni 200, sawa na shilingi 433.6 bln,
kama ruzuku na mkopo wenye masharti nafuu kwenye Mfuko Mkuu wa Bajeti
wa serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018
Imetolewa
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Fedha na Mipango
JUMUIYA YA KANGA MATERNITY TRUST YA ZANZIBAR YAFANYA SEMINA KWA WATAFITI WAZALENDO
Daktari
bingwa. Tarek Meguid wa wodi ya Wazazi Mnazimmoja Hospitali akitoa
tarifa ya pili ya watafiti wazalendo kuhusu wajawazito na watoto katika
Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust iliyofanyika Tembo Hotel
Mjini Zanzibar.
Dkt.
wa Maradhi ya Saratani Mnazimmoja Hospital Salama Uledi Mwita akitoa
taarifa ya hali yaugonjwa wa Saratani ulivyo sasa Zanzibar katika Semina
ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust.
Madaktari
bingwa wa Hospitali ya Mnazimmoja, (kulia) Dkt. Tarek Meguid na
(kushoto) Dkt. Msafiri Marijani wakiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kanga
Maternity Trust (KMT) wakatikati Dk. Mohammed Hafidh wakifuatilia
uwasilishwaji wa Tafiti za ndani kwa madaktari wazalendo.
Dkt.
Sanaa S. Said Phisician (Internal medicine) Mnazimmoja Hospital
akiuliza swaali kwa watafiti wazalendo (hawapo pichani) katika Semina
iliyofanyika Tembo Hotel Mjini Zanzibar.
Dkt.
Msafiri Marijani akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa kuhusu
ugonjwa wa Saratani (kushoto) Dkt. Salama Uledi Mwita ambae amewasilisha
tafiti ya ugonjwa wa Saratani ulivyo Zanzibar.
Dkt.
Mdhamin wa Kijiji cha Watoto (S.O.S) Zanzibar Abdulla Mohammed Hassan
akimkabidhi Certificate Dkt. Natasha Hussein kwa niaba ya Jumuiya ya
Kanga Maternity Trust kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Baadhi ya walikwa katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.
Naibu Waziri wa Habari afungua mashindano ya Brazuka Kibenki
Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura akikagua timu wa wachezaji wa Diamond Trust Bank (DTB) wakati wa
mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mratibu wa mashindano hayo kutoka
Barclays Bi. Nasikia Berya
Mchezaji
kutoka timu ya Barclays akijaribu kuzuia mpira kutoka kwa mchezaji wa
timu ya DTB wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu
kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura akizungumza na wanamichezo kutoka mabenki mbalimbali (hawapo
pichani) wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu
kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura akimkabidhi naodha wa timu ya DTB ngao ya hisani kwa kuwafunga
mabao matatu kwa moja timu ya Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa
mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Afisa Michezo Bw. Rashid Mijuza.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na
wachezaji kutoka Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya
kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam
Waamuzi
wa michezo ya Brazuka kibenki katika picha ya pamoja wakati wa mechi ya
ufunguzi wa mashindano ya kibenki leo Jijini Dar es Salaam.Picha na
Genofeva Matemu – WHUSM
………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali kupitia sera ya
Maendeleo ya Michezo inasisitiza wananchi na jamii kwa ujumla kushiriki
katika michezo ili kujenga afya, kuunganisha watu toka makundi
mbalimbali bila ubaguzi wa kidini, kisiasa, wala kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa
ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Kibenki maarufu kama Brazuka katika
viwanja vya Gymkhana leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Wambura ameeleza kuwa ni
muhimu kwa wafanyakazi kujumuika kwa pamoja katika michezo ili
kuboresha afya na kuimarisha uhusiano baina yao.
“Michezo ni kitu kizuri kwani
husaidia katika kuimarisha na kulinda afya zetu hivyo ni vyema kila
mmoja wetu kushiriki katika michezo ili kuwa nguvu ya kutekeleza
majukumu yetu ya kila siku” alisema Mhe. Wambura.
Vilevile alitoa shukrani kwa
wakuu wote wa mabenki kwa ushirikiano wao wa kuwaleta pamoja
wafanyakazi wa benki ili kufahamiana na kuimarisha ushirikiano baina yao
.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa
Benki ya Barclays Bw. Aron Luhanga amesema kuwa dhumuni la mashindano
hayo ni kuendeleza mahusiano baina ya benki kwa kufahamiana na
kuimarisha afya na fikra zao.
“mashindano haya ni kwa ajili ya
kufahamiana na kuimarisha urafiki kwa wafanyakazi wa sekta ya benki kwa
kufanya sekta ya kibenki kuwa sehemu bora ya shughuli za kiuchumi
nchini” alisema Bw.Luhanga.
Mashindano hayo ya Brazuka
kibenki yanaratibiwa na benki ya Barclays na ni mara ya pili
kufanyika nchini ambapo mwaka jana benki ya Diamond Trust (DTB) iliibuka
mshindi hivyo kushiriki katika ufunguzi wa michuano hiyo mwaka huu.
Benki zinazoshiriki mashindano
hayo ni 18 ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania, NMB, Stanbic, KCB, Exim, Citi
Benki, Commrcial Bank of Africa (BOA),CRDB, Letshego, Eco Bwnki, Akiba,
Diamond Trust Benki, Bank of India, Banc ABC,Azania na Twiga Bancorp.
BABATI WATAKIWA KUJIUNG ANA CHF ILIYOBORESHWA
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza na wananchi wa Tarafa
ya Goroa Wilayani Babati, juu ya kaya zao kujiunga na mfuko wa afya ya
jamii iliyoboreshwa (CHF).
Wananchi
wa Kata ya Duru Tarafa ya Goroa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara,
wakimsikilimza Mkuu wa Mkoa huo Dk Joel Bendera wakati wakiwaeleza
umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Raymond Mushi akizungumza na
viongozi wa Tarafa ya Goroa juu ya mikakati yake ya kuhakikisha jamii
inajiunga na CHF iliyoboreshwa.
Na Mwandishi Wetu
MKUU
wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera amesema atawachukulia hatua kali
viongozi wa ngazi ya Vijiji, Kata, na Tarafa za Wilaya ya Babati,
watakaozembea zoezi la kuhamasisha kaya zijiunga na mfuko wa afya ya
jamii ulioboreshwa (ICHF).
Dk
Bendera aliyasema hayo mbele ya mkuu wa Wilaya hiyo Raymond Mushi,
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Hamis Malinga, wakati
akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Goroa, alipotembelea kuhamasisha
kaya kujiunga na mfuko huo.
Hata
hivyo, amewaagiza viongozi hao kuhakikisha hadi mwezi Desemba mwaka huu
kaya 40,642 zinajiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (CHF)
hivyo kufikia asilimia 50 ya kaya zilizopo kwenye wilaya hiyo.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo ya Babati ina kaya
81,284 hivyo viongozi wa wilaya hiyo wahakikishe hadi mwezi Desemba wawe
wamefanikisha nusu ya kaya zijiunge na mfuko huo.
“Suala
la kupatiwa matibabu pindi mtu akiugua halina mjadala hivyo viongozi wa
ngazi tofauti kwenye wilaya hii ya Babati, wanapaswa kufuatilia ili
kaya hizo zijiunge na mfuko huo ambao una manufaa kwao,” alisema Dk
Bendera.
Alisema
viongozi wote wa eneo hilo wanapaswa kuhakikisha jamii inajiunga na
mfuko huo kwani ni ukombozi wao kwenye sekta ya afya na siku wakistaafu
wananchi watawakumbuka kwa kusababisha mabadiliko ya huduma hizo.
Hata
hivyo, Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) mkoani
humo, Isaya Shekifu alisema mpango wa CHF ulioboreshwa utawawezesha kila
kaya ya watu sita baba, mama na watoto wanne ambao hawajafikisha miaka
18 kupata matibabu kwa gharama ya sh30,000 katika mwaka mzima.
Shekifu
alisema bima ya afya ni muhimu kwa sababu siyo kila mtu anapopata
ugonjwa ana uwezo wa kugharamia matibabu na nchi zilizoendelea
zimefanikiwa kupunguza vifo visivyo na lazima kwa kuhakikisha watu
wanajiunga na mfuko.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati
Hamis Malinga akizungumza mbele ya Dk Bendera, alisema wamejipanga
kikamilifu kuhakikisha kuwa wananchi wa eneo hilo wanajiunga kwa wingi
na mfuko huo.
Malinga
alisema kupitia timu waliyonayo kuanzia ngazi ya vijiji, kata na
tarafa, watatimiza majukumu yao kwa kupeana mrejesho kila mwezi ili
kutambua wamefikia hatua gani na wanatarajia hadi mwezi Desemba
watafanikisha suala hilo.
No comments :
Post a Comment