Friday, July 29, 2016

Kampuni ya Camel Oil yasema uuzwaji wa kiwanja Manzese ulizingatia taratibu za kisheria index

index 
Mahfudhi Ali Meneja wa Kampuni ya Mafuta ya Camel Oil akizungumza na waandishi kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kuhusu taratibu na sheria uuzwaji wa kiwanja Block A kilichopo Manzese jijini Dar es salaam, Kulia ni Benjamin Sawe Afisa habari Mwandamizi Idara ya Habari Maelezo.
…………………………………………………………………………………………………………………
KAMPUNI ya Camel Oil  imesema uuzwaji wa kiwanja namba 130 kilichoko Block A, Manzese jijini Dar es Salaam ulizingatia taratibu zote za kisheria na kwamba hakuna sehemu iliyoghushi hati za kiwanja hicho kama inavyodaiwa. Baada ya kuona utitiri wa habari za nia ya kupotosha ukweli, Camel Oil wameonelea ni vyema wakaonyesha upande wa pili wa shilingi.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Meneja wa Kampuni hiyo, Mahfoudh Ally, alisema kampuni yake ilifata taratibu zote za kiubinadamu na kisheria katika kuuza kiwanja hicho baada ya mmiliki wa awali, Mzee Mohamed Fakhi kushindwa kulipa deni la Sh bilioni 1.4. Huu ulikuwa uamuzi wa mwisho kabisa baada ya jitihada za muda mrefu, na za msingi zilizogonga mwamba baada ya ahadi hewa nyingi sana kutoka kwa mdeniwa, Mzee Mohammed.
Alisema kabla ya mwaka 2010 kampuni yake ilifanya biashara kwa muda mrefu na Mzee Mohamed  wa Manzese Filling Station kuhusiana na  kuuza  mafuta kwa mkopo kwa makubaliano kwamba Camel Oil ilipwe kila mwisho wa mwezi. Camel Oil iliendelea kukipa kituo hicho mafuta lakini mmiliki wa kituo hicho aliendelea kulimbikiza deni hadi kufikia Sh bilioni 1.6 na mwaka 2012 aliacha kununua mafuta kwenye kampuni hiyo ya Camel bila kutoa taarifa yoyote, na Mzee Mohammed pamoja na mtoto wake wakatokomea kusikofahamika.
“Tulifuatilia kujua kwanini kulikuwa na ukimya wa muda na tulitaka kujua atalipaje deni hilo, baada ya muda kadhaa wa kumtafuta tulimpata na tukakubaliana namna ya kulipa deni hilo. Alitoa hundi ambazo baadhi zilipita na nyingi ziligonga ukuta kwani hakuwa na hela benki. Kwa mara nyingine akatokomea kusikojulikana.  Jitihada za dhati ziliendelea kumtafuta na kumsihi alipe ila palikuwa na kila dalili ya kushindwa kulipa deni. Na tulipoona anashindwa kulipa deni tuliomba kushikilia hati mbili za viwanja vyake kama dhamana,” alisema.
Alisema Mzee Mohamed alikubali mwenyewe kwa maandishi kwamba viwanja vyake vishikiliwe na Camel Oil kama dhamana ya deni hilo analodaiwa, na ushahidi wote wa maandishi upo.

77 million newborns globally not breastfed within first hour of life – UNICEF

maniza 
77 million newborns – or 1 in 2 – are not put to the breast within an hour of birth, depriving them of the essential nutrients, antibodies and skin-to-skin contact with their mother that protect them from disease and death, UNICEF said.
“Making babies wait too long for the first critical contact with their mother outside the womb decreases the newborn’s chances of survival, limits milk supply and reduces the chances of exclusive breastfeeding,” said France Bégin, UNICEF Senior Nutrition Adviser. “If all babies are fed nothing but breastmilk from the moment they are born until they are six months old, over 800,000 lives would be saved every year.”
Globally, progress in getting more newborns breastfed within the first hour of life has been slow over the past 15 years, UNICEF data show. In sub-Saharan Africa, for example, where under five mortality rates are the highest worldwide, early breastfeeding rates increased by just 10 percentage points since 2000 in East and Southern Africa but have remained unchanged in West and Central Africa.
In Tanzania, only 1 out 2 children aged 0-23 months benefit from early initiation of breastfeeding, according to the 2014 Tanzania National Nutrition Survey (TNNS 2014). In some regions, the level is even lower at less than 25 per cent, including in Tabora, Geita, Shinyanga, Rukwa and Katavi regions in the Mainland.
The longer breastfeeding is delayed, the higher the risk of death in the first month of life. Delaying breastfeeding by 2-23 hours after birth increases the risk of dying in the first 28 days of life by 40 per cent. Delaying it by 24 hours or more increases that risk to 80 per cent.
“Breastmilk is a baby’s first vaccine, the first and best protection they have against illness and disease,” said France Bégin. “With newborns accounting for nearly half of all deaths of children under five, early breastfeeding can make the difference between life and death.”
UNICEF Representative in Tanzania, Maniza Zaman, said, “For many different reasons, including cultural norms and lack of knowledge, women in Tanzania are not receiving the support they need to start breastfeeding immediately after the baby is born. Giving babies other liquids or foods may be another reason early breastfeeding is delayed. We have to intensify our efforts so that many more Tanzanian children, and their mothers, benefit from optimal breastfeeding practices.”
Moreover, around the world only 43 per cent of infants under six months old are exclusively breastfed. Babies who are not breastfed at all are 14 times more likely to die than those who are fed only breastmilk.
In Tanzania, less than 41 per cent of children under six months old were exclusively breastfed in 2014. In some areas, like Ruvuma and Tanga in mainland Tanzania, the figure is as low as 25 per cent.  In Zanzibar, 20 per cent of children were exclusively breastfed, with Pemba, as low as 10 per cent (NNS, 2014).
But any amount of breastmilk reduces a child’s risk of death. Babies who received no breastmilk at all are seven times more likely to die from infections than those who received at least some breastmilk in their first six months of life.
Tanzania has an opportunity to further highlight the need for more efforts in good breastfeeding practices. From 1-7, World Breastfeeding Week, will be celebrated in mainland Tanzania, along with the national Farmers’ Day known as “Nane Nane”. Activities will include televised roundtable discussions as well as health and nutrition talks with mothers in in health facilities and in communities. In Zanzibar, the theme will be “breastfeeding, a key to sustainable development”. The focus will be on addressing social norms that contribute to poor breastfeeding practices.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki watekeleza agizo la Rais kwa kuchangia Madawati.

index 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi  Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimkabidhi  hundi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya makabidhiano  madawati  ikiwa ni fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais Mhe. John Magufuli  mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam . Picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO
……………………………………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es salaam
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamechangia kiasi cha Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari nchini.
Akikabidhi mchango huo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya watumishi wa wizara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi  Augustine Mahiga amesema kuwa watumishi hao wametoa fedha hizo kwa shule ya msingi Chamazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.
Balozi Mahiga amesema Wizara yake iliwahamasisha watumishi wake walio makao makuu na wale walio kwenye balozi mbalimbali nje ya nchi kuchangia zoezi hilo la upatikanaji wa madawati.
“Ili kufanisha upatikanaji wa fedha hizi Wizara yangu iliwahamasisha watumishi wake wote walio Makao makuu na wale walio katika balozi zetu duniani kote,  wito huu uliitikiwa kwa ari na hamasa kubwa na kufanikisha kukusanya kiasi cha Shilingi 100,176,825.52 za kitanzania”alisisitiza Balozi Mahiga
Waziri Mahiga aliongeza kuwa mara baada ya kukusanya fedha hizo watumishi wa Wizara hiyo waliamua kumpatia aliyekuwa Mtumishi wa Wizara ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kiasi cha shilingi Milioni 15 kwa ajili ya ununuzi wa madawati katika Wilaya yake.
Aidha, amesema kiasi fedha zilizobaki zaidi ya shilingi milioni 85 zilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa  kwa ajili ya mchango wa utengenezaji wa madawati ya shule ya Msingi Chamazi iliyoko Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
 
Waziri Mahiga aliongeza kuwa mbali na wizara yake kuwa na majukumu mbalimbali bado inalo jukumu la kuhakikisha inaitangaza Tanzania ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.

ZIARA YA WAZIRI MBARAWA MWABEPANDE

rw1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Afisa Uhusiano wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bi. Edna John wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
rw2 
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga  akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
rw3 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga  wakati alipokagua  ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
rw4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga  wakati alipokagua  ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
rw5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua baadhi ya miundombinu iliyopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za wafanyakazi zilizopo Bunju B jijini Dar es salaam.
rw6 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
rw7 
Meneja Mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania Arch.Humphrey Killo akifafanua mchoro wa ramani ya ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam katika barabara ya Sam Nujoma,wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga .
rw8 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga  wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
rw9 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga  wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
rw10Muonekano wa awali wa ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
rw11Muonekano wa nyumba za wafanyakazi nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA BENJAMINI SAWE-MAELEZO

Clinton: Trump hawezi kutatua matatizo Marekani

cli1 
Bi Clinton amesema Wamarekani wenyewe ndio wanaoweza kusuluhisha matatizo yao.
…………………………………………………………………………………………………………
Hillary Clinton amekubali rasmi kuwa mgombezi wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, huku akisema wakati wa kupambana na mpinzani wake sasa umeanza rasmi.
Alitoa wito kwa wanachama wote wa Democratic kuungana naye huku akimkebehi mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump, katika madai yake kuwa ni yeye pekee anayeweza kuyasuluhisha matatizo ya Marekani.
Alisema kuwa Wamarekani hufanya kazi kwa pamoja kyatatua yote yanayonufaisha taifa.
Awali, bintiye Chelsea Clinton alikuwa ametoa hotuba na kumsifu sana mamake. Alisema ni mwanamke ambaye huwa hasahau anawapigania akina nani.
“Watu huniuliza kila wakati, huwa anawezaje kufanya haya? … ni kwa sababu huwa hawasahau watu anaowatetea,” amesema.
“Najua kwa moyo wangu wote kwamba mamangu atatufanya tujionee fahari.”

KATIBU MKUU AFYA ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE YA KIBIRIZI MKOANI KIGOMA

kif1 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi.
kif2 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi, Katikati ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Bw. Moses Msuluzya.
kif3 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kwa ajili ya ziara ya kikazi.
kif4 
Afisa Mfawishi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma Bw. Ladius Mushi akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuhusu Makazi hayo na namna wanavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Wazee hao wanakuwa katika mazingira salama.
kif5 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongozwa na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kukagua baadhi ya majengo wanayoishi wazee hao ili kuona namna ya kuyaboresha kadiri inavyowezekana wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi hayo.
kif6 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongozwa na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kukagua baadhi ya majengo wanayoishi wazee hao ili kuona namna ya kuyaboresha kadiri inavyowezekana wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi hayo.
kif7 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma
kif8 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akitoa Zawadi ya Sabuni kwa viongozi wa wazee wa Makazi ya Kibirizi Katibu Makazi hayo Bi. Veronica Nyaga  na Mwenyekiti Bw.Hamisi Sabuni
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

waziri mwakyembe akutana na viongozi wa WILDAF

k1 
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema mazingira ya kisiasa na kijamii yaliyopo nchini sasa ni mazuri kuliko kipindi chochote nyuma kwa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF) kufanikisha kampeni yake ya muda mrefu ya kuondoa sheria zote kandamizi kwa wanawake katika masuala ya mirathi.
k2 
Akiongea na viongozi wa WILDAF wakiongozwa na mpigania haki za akina mama na mwanasiasa mkongwe nchini, Bi.Tabitha Siwale jijini Dar es Salaam leo, Dk. Mwakyembe amesema WILDAF washindwe wenyewe kwani kuna mabadiliko chanya makubwa nchini ya fikra kuhusu haki za akina mama.
Waziri Mwakyembe  amewahimiza WILDAF kupeleka mapendekezo ya mabadiliko ya sheria mbalimbali hasa zile za mirathi wizarani mapema iwezekanavyo ili kazi ya kuondoa mapungufu kwenye sheria hizo ikamilishwe.

PROPERTY INTERNATIONAL WADHAMINI TAMASHA LA UZINDUZI WA KITABU CHA SAFARI YA SOKA NCHINI, WATANI WA JADI YANGA, SIMBA, MABALOZI KUUMANA

 Mkurugenzi wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya Wachezaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Machinga’, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa Tamasha hilo, Bahari Camari.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya Wachezaji wa zamani wa Simba, Moses Mkandawile, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa Tamasha hilo, Bahari Camari.
 Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kulia) amkimkabidhi Tisheti Kipa wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, zitakazotumika kufanyia mazoezi siku ya Tamasha. (wa pili kushoto) Katikati ni Afisa Habari wa Property, Saleh na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada.
 Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed, akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wachezaji wa zamani wa Vilabu vya Yanga na Simba, kuhusu Tamasha la jumamosi katika Uwanja wa Uhuru.
Na Ripota wa Sufianimafoto Blog,Dar
KAMPUNI ya Property International Ltd imedhamini bonanza la
uzinduzi wa kitabu cha soka cha Safari ya Soka la Tanzania litakalofanyika
Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 
Katika bonanza hilo la uzinduzi wa kitabu hicho litaambatana
na maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya uhuru wa Algeria, ambalo litahudhuriwa na Waziri wa
Habari Michezo na Utamaduni, Nape Nauye ambaye ataongozana na Waziri wa Mambo
ya Ndani Mwigulu Nchemba.
Katika Bonanza hilo pia kutakuwa na mechi kadhaa ikiwemo maveterani wa
timu za Simba na Yanga, mechi za vyombo vya habari pamoja na mabalozi wa nchi
mbalimbali nchini Tanzania wataungana na kucheza na maveterani wa Simba na
Yanga. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

NEMC YAPEWA MWEZI MMOJA KUKAMILISHA RIPOTI YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KATIKA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA MTWARA

2 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina akipata Maelezo kuhusu uchataji wa taka unaofanywa na kiwanda cha SBS kutoka kwa  Bw. Joseph meneja uendeshaji wa kiwanda hicho.
3 
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kulia Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw.  Khatibu Kazungu  kushoto ni  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda wakigagua DAMPO jipya la kisasa la Mjini Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira.
1 
DAMPO la kisasa la Mjini Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira lililojengwa kwa hisani ya benki ya Dunia kwa thamani ya shilingi bilioni 8.8, mara DAMPO hilo litakapoanza kutumika litakuwa na uwezo wa kutengeza nishati mbadala.
(Picha na Evelyn Mkokoi)
………………………………………………………………………………………………
Baraza la taifa na Hifadhi ya Mzingira NEMC limepewa mwezi mmoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kupima Vumbi, Moshi na Maji yanayotoka katika kiwanda cha kuchakata taka cha SBS kilichopo katika maeneo ya Mangamba Mjini Mtwara ili kujirisha kama vina madhara kwa mazingira na viumbe hai.
Naibu Waziri Mpina akiwa katika muendelezo wa Ziara yake ya kukagua mazingira na kuangalia utekelezaji wa sheria ya mazingira kwa wenye viwanda nchini amelitaka baraza hilo kufanya kazi zake kwa umakini na kutokukubali majibu ya vipimo toka kwa mwenyekezaji bila NEMC pia kufanya vipimo na kupata majibu sahihi kutokana na sababu kuwa wananchi wamekuwa wakilalamika mara kwa mara juu ya uchafuzi wa mazingira unaofanywa na wenye viwanda jinsi unavyo hatarisha maisha yao na mazingira kwa ujumla.
Katika Ziara Hiyo ya Mjini Mtwara, Naibu Waziri Mpina Pia alitembelea DAMPO la kisasa la mjini hapo lilijengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia lenye thamani ya shilingi Bilioni 8.8 na kuwapongeza wana Mtwara kwa kupata Dampo la kisasa ambalo ni Rafiki wa Mazingira, na kuwashauri waratibu wa mradi huo na uongozi wa mkoa wa Mtwara kuanza kutumia DAMPO hilo ambapo taka zitakazowekwa katika DAMPO hilo la kisasa, pia zinaweza kutumika kutengeneza nishati mbadala.
Awali, akitoa taarifa ya Mazingira ya Mkoa wa Mtwara, katibu Tawala wa Mkoa huo Bwana Afred Luanda, alisema kuwa Mkoa unakabiliana na changamoto mbali mbali za kimazingira ikiwa ni pamoja na uvuvi haramu wa kutumia mabomu, ukataji miti ovyo kwa matumizi ya kuni na mkaa, vifaa vya uondoshaji taka pamoja na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Ziara Ya naibu Waziri Mpina Mkoani Mtwara leo ilihusisha pia kutembelea bandari ya mtwara ili kujionea utekelezaji wa sheria ya mazingira katika uingizwaji wa viwatilifu na kemikali hatarishi kwa mazingira zinazoingizwa  kupitia bandari hiyo.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AAHIDI KUKOMESHA UFANYAJI KAZI WA MAZOEA

Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha(CD),Athuman Juma akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo juu ya mipango kamambe ya kukomesha wavamizi wa maeneo ya wazi ambayo yametambuliwa kuwa ni viwanja 52.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha(CD),Athuman Juma akizungumza namna jinsi walivyojipana kukusanya mapato kwanjia za kieletroniki na mashine za EFD’s kuhakikisha mapato hayapotei.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania,Eliya Mbonea akiuliza swali.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha(CD),Athuman Juma akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo

Waandishi wa habari wakiwa makini kuchukua taarifa hiyo

Waandishi wa habari wakiwa makini kuchukua taarifa hiyo

Afisa Habari Mwandamizi wa Jiji la Arusha,Nteghenjwa Hoseah akizungumza jambo baada ya mkutano huo.

No comments :

Post a Comment