Thursday, December 31, 2015

NAIBU WAZIRI WA ARDHI ANJELINA MABULA ATEMBELEA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)

1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiwasili Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es salaam huku akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Ndugu Nehemia Mchechu wakati waziri huyo akiwa katika ziara yake ya kujifunza na kusikiliza Changamoto na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na shirika hilo.
2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiuliza jambo kwa mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
3
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
4
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiwa katika kikao na wakuu wa vitengo mbalimbali  wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
5
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC , kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu .
6
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC  Upanga. 
7
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari  hawapo pichani katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC  Upanga. 
8
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu  akijibu baadhi ya maswali yalioulizwa na waandishi wa habari wakati Naibu Waziri Angelina Mabula alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea shirika hilo leo.
9
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Muungano Saguya katikati na kulia ni Yahya Charahani Maafisa kutoka shirika hilo la NHC.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akikabidhi sehemu ya msaada kwa baadhi ya watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi Mlezi wa Watoto na Vijana, Stella Mwambenja wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya watoto wa kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa chakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016 kwa vituo vitatu vya watoto yatima  Dar es Salaam. Kulia ni Mlezi wa Watoto na Vijana wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede, Stella Mwambenja. 
Mmoja wa watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede cha Buguruni Malapa Dar es Salaam akitoa shukrani kwa kampuni ya TTCL baada ya kukabidhiwa msaada huo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Amanda Luhanga (kulia) wakipewa historia fupi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge kwa Ofisa Mfawidhi, Ojuku Mgezi (katikati) kabla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge.
Sehemu ya makazi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge
Sehemu ya msaada ukishushwa kwenye Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas  (kulia) akizungumza na watoto wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Honoratha cha Temeke jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada Mlezi wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Honoratha cha Temeke jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. TTCL imetoa msaada wa mifuko ya Unga, Sukari, Mchele, Maharage na Mafuta ya Kupikia kwa vituo vitatu tofauti vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (katikati)  kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Temeke cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016.

NHIF waianza 2016 kwa kuboresha huduma zao

REN1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Michael Mhando akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam(Hawapo Pichani).
REN2
Mkurugenzi wa Masoko, Elimu kwa Umma na Utafiti Rehani Athumani akiongea na Waandishi  wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu maboresho katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
REN3
Waandishi wa Habari wakifatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na  Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Leo Jijini Dar es salaam
Picha na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
……………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unategemea kuboresha baadhi ya huduma zao ifikapo 2016 ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma hizo kwa wananchi.
Akiyasema hayo leo Jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu Michael Mhando amezitaja baadhi ya huduma ambazo wana mpango wa kuziboresha kwa mwaka 2016  zikiwemo za kuongeza huduma ya matibabu ya moyo kwa kutumia bima ya NHIF,kutoa mikopo ya dawa,kurekebisha mfumo wa ulipaji wa baadhi ya huduma pia kubadili gharama za huduma ambazo zinalipwa kwa watoa huduma ili kuendana na hali halisi ya mfumuko wa bei.
‘’mimi binafsi nimefurahishwa na agizo la Mheshimiwa Rais  kutengeneza maduka ya dawa kila Hospitali ya Mkoa na nitakua tayari kushirikiana nao kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi’’alisema Mhando.
Naye Mkurugenzi wa Masoko, Elimu kwa Umma na Utafiti Rehani Athumani amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili zikiwemo za kukosekana kwa dawa katika hospitali husika pamoja na tabia ya baadhi ya wanachama kugushi baadhi ya nyaraka wakati wa usajili.
Aidha,Bw. Rehani Athumani ametaja hatua itakayochukuliwa ili kudhibiti ubora wa huduma zitolewazo na mfuko huo kuwa ni kufanya ukaguzi wa kushtukiza ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama ‘Medical surveillance’ katika vituo vya matibabu ili kuona ubora wa huduma wanazotoa kwa wananchi.
Katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utahakikisha kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watoa huduma ambao wataongeza bei za huduma kwa wanachama wa mfuko huo na maboresho hayo  hayataathiri kiwango cha michango kinachotolewa na wanachama.

Salamu Za Mwaka Mpya Kutoka Mjengwablog

775ae8d7-3742-4487-9f7d-3decafe88b21
Ndugu zangu,
Imekuwa ni utamaduni wangu kutuma salamu za Mwaka Mpya kwa wajumbe wangu wa Mjengwablog, marafiki zangu kwenye FB na wengine walio ndani na nje ya mitandao ya kijamii.
Nimefanya hivyo tangu mwaka 2006 ilipoanzishwa Mjengwablog. Na mwaka huu naendeleza utamaduni huo.
Ndugu zangu,
Naandika salamu hizi nikiwa hapa Iringa, na nikiwa na mambo mawili ya kuwaeleza; 
Mosi, napenda kuwahakikishia kuwa Mjengwablog/KwanzaJamii itaingia mwaka mpya wa 2016 na kasi zaidi ya mwaka jana. Tutazidisha ubunifu katika kuwaletea huduma mpya na bora zaidi.
Ikumbukwe, Mjengwablog ilikuwa blogu ya kwanza hapa Tanzania kuja na ubunifu wa kuweka kurasa za mbele za magazeti mwaka 2007. Mwaka huu tumekuwa blogu ya kwanza Tanzania kwa kuwa wa kwanza kila alfajiri kuwaletea habari za magazetini zikiwa na uchambuzi wa habari ku 3 ikiwamo uchambuzi wa katuni bora ya siku.
Mwakani tumedhamiria kuunganisha huduma hizo na radio blogging ikiwa na maana ya kufanya chambuzi kwa njia ya radio ya mtandaoni na kuposti ( KwanzaJamii Radio). Mengine mapya ya kiubunifu yako jikoni, yatakuja kwa mwaka ujao, 2016.
Jambo la pili nililotaka kulisema linahusu hali ya mtanziko wa kisiasa Zanzibar. Ni majuzi tu nilikuwa Zanzibar kwa takribani juma moja. Nilitembea Zanzibar mjini na vijijini.
Hakika, sijawahi kupanda boti na kuviacha visiwa vya Zanzibar nikiwa na shaka ya kitakachotokea nyuma baadae. Safari hii niliondoka Zanzibar nikijisikia hivyo. Zanzibar sikuikuta hali njema ya upepo wa kisiasa. Nakumbuka nikiwa kitongoji kimoja pale Jambiani nilioongea na wenyeji walioonyesha shaka kwenye mazungumzo. yao wakati wakiongea nami.
Pale Jambiani niliiona chuki baina ya wenyeji iliyotokana na tofauti za kiitikadi. Chuki iliyoonyeshwa hata kwenye maandishi ya kutani na kwenye milango ya nyumba. Ni chuki iliyoonyeshwa hata kwenye mijadala ya mitandaoni ambayo binafsi niliianzisha kwa madhumuni ya kuamsha fikra na kubadilishana maarifa na uzoefu.
Niliyoiona si Zanzibar niliyoifahamu. Bado naamini, Zanzibar imejaa watu wakarimu na wenye upendo. Suluhu ya Zanzibar itapatikana na Wazanzibar wenyewe na kwa njia ya mazungumzo hadi kufikia muafaka.
Na walio kwenye meza ya mazungumzo wasitangulize maslahi binafsi. Kwenye kujadiliana ili kutatua mgogoro pande husika ziwe tayari kupata na kupoteza. Si vema pia kwenda kwenye meza ya mazungumzo ukihitaji jambo moja tu, kwamba kama ukilikosa ndio mwisho wa dunia.
Na duniani hapa mengine yaliyofutwa, na kama ni kisheria na yakachapwa hata kwenye gazeti la serikali, basi, si rahisi yakarejeshwa kwa wino ule ule. Ni vema ikatangulizwa hekima na busara. Ni vema na ni busara yakawekwa mazingira ya, hatma ya yote, kuwa pande zinazokinzana zote zikaibuka washindi.
Na hakuna namna yeyote ile ya kuvifanya visiwa vikawa tulivu bila ya uwepo wa makubaliano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo viongozi wakuu wa pande zote mbili wafanye kazi ya ziada ya kuwahimiza wananchi wao kuchimba makuburi marefu ya kuzizika chuki zao baina ya wao kwa wao. Chuki zilizojengeka kwenye misingi ya ubaguzi. Na sote tunajua dhambi ya ubaguzi, ni kama dhambi ya mwanadamu kuonja nyama ya mwanadamu mwenzake, hawezi kuacha.
Ni iwekwe wazi, kuwa suala la Muungano wetu halipaswi kuwa mjadala tena kama uwepo au usiwepo, bali ni kwa namna gani tutauimarisha.
Maana, daima utabaki kuwa ukweli, kuwa jambo la Zanzibar ni letu Bara, na kinyume chake.
Na tuwe tayari kupambana hadi risasi ya mwisho, na nguvu zote hasi, za ndani na nje ya mipaka yetu, zinazotaka kututenganisha kwa misingi ya Uzanzibar, Upemba, Ubara na hata udini.
Ni imani yangu, kama ilivyotokea huko nyuma, kuwa Zanzibar imeweza kuvuka mitihani migumu na ikasimama tena.
Naziona ishara za tumaini jipya la Zanzibar linalokuja. Kwamba viongozi wakuu wa CCM na CUF Zanzibar watazishinda nguvu hasi na zinazochagizwa na wahafidhina wa pande zote mbili, hivyo, kupata formula mpya ya kuvivusha visiwa vya Zanzibar na Pemba kutoka kwenye mtanzuko wa kisiasa uliopo sasa.
Mungu Ibariki Tanzania na Heri Ya Mwaka Mpya.
Maggid Mjengwa,
Iringa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Atoa Risala ya Kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2016

4efab04e-03f8-4760-9e14-104ccf23e617
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitowa Salamu za kuukaribisha Mwaka Mpya 2016 kwa Wananchi wa Zanzibar Ikulu Zanzibar leo 31/12/2015.(Picha na Ikulu Zanzibar) 

WAZIRI UMMY MWALIMU AKUTANA NA WADAU WA TIBA ASILI

ee69e1f3-7fab-4193-9f44-01f8f971e7df
WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO, UMMY MWALIMU AKUTANA NA WADAU WA TIBA ASILI,LEO OFISINI KWAKE NA KUJADILIANA MAMBO MBALIMBALI HATA HIVYO WIKI IJAYO WATATOA TAMKO KUHUSIANA NA MAJADILIANO HAYO.

TAARIFA KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU

6a94a7d0-e50d-49e2-aa9b-07a9bcaa97c5

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA BARUA PEPE ZA KAWAIDA KATIKA MAWASILIANO YAKE.

aj2
Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
aj3
Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi leo jijini Dar es salaam.
aj4
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) kuhusu utendaji wa Wakala hiyo leo wakati wa  ziara ya kikazi ya Mhe. Angella Kairuki katika Ofisi za Wakala hiyo leo jijini Dar es salaam.
aj5
Mkurugenzi wa Uratibu wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Benjamin Dotto akitoa ufafanuzi kwa Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam.
aj7
Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) akitembelea maeneo mbalimbali ya Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao leo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
aje1
Waziri  Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza na Watendaji na baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
 …………………………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam.
Serikali imepiga marufuku matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali  kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA Serikalini.
 “Sasa kuna watumishi 7000 wanaotumia anwani za Barua  pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu”  Amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye mawasiliano binafsi.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia  mitandao mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia Barua Pepe za Serikali.
Mhe. Kairuki amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za  umma zinaunganishwa na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano.
“Katika hili ninatoa siku 60 muhakikishe kuwa mnakamilisha kwa Taasisi zilizobaki ili kwa wale watakaopuuzia hatua zianze kuchukuliwa” Ameeleza Mhe. Angella.
Aidha, ametoa wito kwa watendaji wa Wakala hiyo kuweka mpango  wa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa kitaaluma watumishi waliopo kazini  kwa kujenga utaratibu wa kuwarithisha uzoefu watumishi ili kuendelea kuimarisha ufanisi na utendaji wa Wakala hiyo.
Mhe. Kairuki amewataka kuwa wabunifu katika kuanzisha mifumo mipya ya TEHAMA  ili kuimarisha dhana ya Serikali mtandao  ili kupunguza gharama hadi kufikia asilimia 5 ya fedha zinazotumika kuendeshea masuala mbalimbali ambayo yangefanywa kupitia matumizi ya TEHAMA.
Akizungumzia kuhusu ununuzi wa vifaa vya TEHAMA serikalini ameitaka Wakala hiyo kutoa ushauri ili kudhibiti mianya ya ubadhirifu na matumizi mabaya  ya fedha katika kununulia vifaa hivyo kwa gharama kubwa wakati vinaweza kupatikana kwa bei ya kawaida.
“katika hili Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika katika upotevu wa mapato muhakikise mnazisaidia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika masuala ya ununuzi wa mifumo na vifaa vya TEHAMA ili mifumo inayonunuliwa iwe na manufaa kwa wananchi na thamani halisi ya fedha”  
Amesema Serikali itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kupitia mtandao ili wananchi waweze kupata huduma hizo  mahali walipo kwa gharama nafuu na kutoa wito kwa watumishi wa Wakala ya Serikali mtandao (e-Gov)  kuwa wabunifu katika kutengeneza programu mbalimbali na mifumo salama itakayowasaidia wananchi kupata huduma.
Aidha, katika hatua nyingine ameitaka e-Gov kuendelelea kujenga uwezo katika kudhibiti dharura na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika matumizi ya TEHAMA na kuitaka Wakala hiyo iendelee kulifanyia kazi suala la kuwezesha mifumo ya Serikali kuzungumza kati ya taasisi moja hadi nyingine ili huduma zote  ziweze kupatikana katika eneo moja  na kuondoa urudufu wa mifumo iliyopo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Gov) Dkt. Jabiri Bakari akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala hiyo amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali toka kuanzishwa kwake Julai 11, 2012 imeendelea kupata ufanisi katika uimarishaji wa Serikali Mtandao.
Amesema kuwa Wakala hiyo inaendelea kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinawafikia wananchi kupitia mtandao mahali walipo na kuhakikisha kuwa inafanikisha lengo la huduma zote za Serikali kupatikana chini ya dirisha moja.
Aidha amesema kuwa Wakala ya Serikali Mtandao itaendelea kuhakikisha kuwa usimamizi wa viwango vya matumizi ya TEHAMA katika Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali vinazingatiwa.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI ASISITIZA UTENDAJI KAZI WENYE TIJA

JH1
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya 2016. Baraza hilo limefanyika Desemba 31, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
JH2
Askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza wakati akitoa hotuba yake kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2016.
JH3
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa timamu kumpokea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akiwasili tayari kwa kulihutubia Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2016.
JH4
Maafisa ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba fupi aliyoitoa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
…………………………………………………………………………………………………
Na Lucas Mboje, Dar es Salaam
WATUMISHI wa Jeshi la Magereza wametakiwa kuzingatia utendaji kazi wenye tija mahala pa kazi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea(Business as usual).
Rai hiyo imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja wakati akizungumza kwenye Baraza la kufunga Mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka mpya 2016 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini, Dar es Salaam.
Jenerali Minja amewaagiza Watumishi wote wa Jeshi hilo kuhakikisha kuwa wanawajibika kwenye maeneo yao ya kazi ili kufikia ufanisi uliotarajiwa pamoja na kutumia vizuri rasilimali za Ofisi kwa manufaa yaliyokusudiwa.
“Utekelezaji wenu wa kazi za kila siku lazima uwe na tija na uendane sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ili kufikia ufanisi unaotarajiwa”. Alisema Jenerali Minja.
Aidha Jenerali Minja amezungumzia baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa Mwaka 2015 ambayo ni pamoja na kukamilika kwa Sera ya Taifa ya Magereza ambayo italiwezesha Jeshi hilo kutekeleza mpango wake wa Maboresho ya maeneo mbalimbali, kusainiwa kwa Mkataba  na Kampuni ya Poly Teknology ya China itakayojenga nyumba 9,500 za Makazi ya Maafisa na Askari, kusainiwa kwa Mkataba wa Magari 9,05 na Kampuni ya Ashok Leyland ambapo magari hayo yanatarajiwa kupokelea mapema mwakani.
Mafanikio mengine ni pamoja na Usajili wa kudumu wa Chuo cha Urekebishaji ambapo Chuo hicho kitatoa elimu stahiki ya Urekebishaji itakayotambulika ndani na nje ya Nchi, Jeshi la Magereza limepeleka Maafisa wake kwenye shughuli za Ulinzi wa Amani kwenye nchi mbalimbali zenye migogoro, Jeshi limeingia ubia na Wawekezaji mbalimbali katika miradi ya Kilimo, uchimbaji madini ya chokaa, ujenzi wa maduka makubwa(shopping Malls) katika Mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro ambapo miradi hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa Jeshi.
Vilevile Jeshi limefanikiwa kuandaa Maandiko mbalimbali ikiwemo andiko la kujitosheleza kwa chakula na miradi minane ambayo miradi hiyo ikiwezeshwa inaweza kuongeza thamani za mali zinazozalishwa na Jeshi hilo.
Aidha Jenerali Minja alieleza changamoto mbalimbali ambazo Jeshi hilo linakabilianazo ambazo ni ufinyu wa bajeti, uhaba na uchakavu wa vyombo vya usafiri, ukosefu wa zana za kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa hivyo kuathiri Uzalishaji, tatizo la miundombinu ya magereza na msongamano magerezani hali inayopelekea kwa kiasi fulani kuathiri utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja ametoa Salaam za kheri ya Mwaka mpya 2016 kwa Watumishi wote wa Jeshi hilo na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotawala uendeshaji wa Jeshi la Magereza.

TAARIFA MUHIMU KWA UMMA KUTOKA UTUMISHI

LO1 
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inawatahadharisha wateja na wananchi wote kujihadhari na watu wanaotumia jina la ofisi kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kujitambulisha kuwa ni watumishi wa ofisi hii. Imebainika miongoni mwa wanaotapeli anatumia jina la James Josephat na kujifanya ni mtumishi wa masijala. Namba ya simu inayotumika kutapeli ni namba 0657 888 277. Ofisi haina mtumishi mwenye jina hilo, na huduma za ofisi hazitolewi kwa ada ya aina yoyote. Ofisi inawatahadharisha wadau na wananchi kuzingatia taratibu zilizopo na kuelewa huduma hazitolewi kwa malipo ya aina yoyote. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Kny: Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

POLISI ARUSHA YASHTUKIA “DILI”

US1
Askari wa Jeshi la Polisi wa wilaya ya Arusha na vikosi vingine wakiwa wanamsikiliza Afisa Masoko wa URA SACCOS toka makao makuu  Mkaguzi wa Polisi Shabani Jumbe alipokuwa anatoa elimu hiyo katika ukumbi wa bwalo la Polisi uliopo jijini hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
US2
Mmoja wa wanachama cha Ura saccos CPL Ezekiel akiuliza swali lililokuwa linamtatiza kwa muda mferu ambalo baadae lilijibiwa vizuri na Afisa Masoko huyo toka makao makuu (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
US3
Mkuu wa kituo kikuu cha Polisi Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Thomas Mareko akitoa ufafanuzi kwa askari waliohudhuria kikao hicho juu ya Ura Saccos kulia kwake ni Mkaguzi wa Polisi shabani Jumbe ambaye pia ni Afisa Masoko wa chama hicho. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
US4
Baadhi ya askari wakiwa wanajaza fomu za Ura Saccos kwa ajili ya kujiunga na chama hicho mara baada ya kupata elimu iliyoeleweka toka kwa Afisa Masoko toka Makao makuu Mkaguzi wa Polisi Shabani Jumbe. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 ………………………………………………………………………………………………………………
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Ikiwa tunauaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 masaa machache yajao baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa wanaonekana kufurahia baada ya wengi wao kupata elimu ya Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo Ura Saccos iliyokuwa inatolewa na Afisa Masoko na uelimishaji wa Chama hicho toka Makao Makuu Mkaguzi wa Polisi Shabani Jumbe.
Elimu hiyo iliyotolewa na Afisa Masoko huyo, iliwafanya askari zaidi ya 100 wabadilishe mawazo ya kujitoa kwenye Chama hicho na badala yake walichukua fomu za kujiunga na Chama hicho kwa ambao hawakuwa wanachama na kwa wale ambao walikuwa wanachama waliamua kuongeza kiwango cha makato kwa asilimia 50 hadi 90 huku wengine wakiendelea kupiga simu kwa msimamizi wa Ura Saccos mkoa wa Arusha PC Said wakitaka fomu za kujiunga na Chama hicho.
Awali akitoa elimu hiyo katika wilaya za Arumeru, Monduli, Longido na Arusha mjini, Afisa Masoko huyo  alisema tatizo kubwa lililokuwepo ni ufinyu wa elimu kwa wanachama na wasio wanachama na kufafanua kwamba wameamua kutoka ofisini na kuwafuata mikoani kwa lengo la kuwaelimisha ili waone umuhimu wake.
Alisema wanachama wengi walikuwa hawajui sababu zinazosababisha kupata mikopo midogo ndani ya Chama hicho kwamba zinatokana na kiasi cha Akiba wanazoweka kwa mwaka kuwa ni kidogo huku akisema wengi wao wanaweka elfu kumi kwa mwezi.
“Sasa mfano utakuta mwanachama anaweka Tsh. 10,000/= Kwa mwezi ndani ya mwaka mmoja anajikuta ana Tsh 120,000/= alafu baada ya miaka mitatu anaomba mkopo hivi unafikiri utapata kiasi gani”? Alihoji Afisa Masoko huyo Shabani Jumbe ambaye pia ni Mkaguzi wa Polisi.
Alisema Chama hicho kwa sasa kimeweka utaratibu wa kumwekea Mwanachama 3% kwa kila laki tano ambayo atakuwa ameweka akiba ndani ya chama hicho ambayo inaitwa riba juu ya Akiba.
Akitoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa Mwanachama kutoa Akiba yake ndani ya siku 90 na si chini ya hapo alisema hii inatokana na idadi ya wanachama wanaochukua mikopo kuwa kubwa lakini pia inatoa fursa ya kukusanya madeni toka kwa wanachama wengine waliokopa.
“Wanachama wengi wanashindwa kutofautisha kati ya Akiba na Amana ambapo kwenye Amana mwanachama anaweza kutoa fedha yake wakati wowote na haina notisi ya siku 90 lakini kwenye Akiba utaratibu wetu ni siku 90 lakini pia karibu askari 21,000 kwa mwezi wanachangia Tsh 10,000 hali ambayo inakwamisha uwezo wa chama kukua na kusababisha kushindwa kutoa mikopo mikubwa kwa wanachama”. Alisema Afisa Masoko huyo.
Alisema mbali na kuweka akiba kwenye chama hicho lakini pia wanachama wanatakiwa wawe wananunua hisa zaidi ya zile za msingi ambazo ni 20 lakini tu zisizidi 20% ya hisa zote za chama hicho ili kuondokana na hali ya uchangiaji tu bali pia wawe wamiliki wa sehemu ya chama na mwisho wa mwaka kupata gawio.
Alisema uwepo wa Chama hicho ambacho kwa sasa kina wanachama wanaokadiriwa 34,000 kimesaidia kuweka usimamizi wa nidhamu ya fedha Kwani ni watu wachache wenye uthubutu wa kuwa na utamaduni wa kuweka Akiba kila mwezi na kuongeza kwamba mpaka sasa toka mwaka 2007 kimetoa mikopo kwa wanachama wake kiasi cha Tsh. 82.3 bilioni.
Naye Mkuu wa kituo kikuu cha Polisi cha Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Thomas Mareko ambaye kitaaluma ni Mhasibu aliwataka askari kuongeza viwango vya akiba zao hali ambayo itawasaidia kupata mikopo mikubwa na pia kunufaika na riba ya aslimia tatu ya kila mwezi kwa watakaoweka kuanzia Tsh. 500,000/=.
Alisema awali askari walikuwa na wasiwasi juu ya Chama hicho lakini baada ya elimu walielewa hivyo aliwataka wachangamkie fursa hiyo ya kupata mikopo yenye riba nafuu.
Kwa upande wao baadhi ya askari waliopata elimu hiyo kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa huu walisema wameweza kubadilishwa mawazo yao ya kutaka kujitoa kwenye chama hicho na hivyo wameamua kuongeza akiba hali ambayo itasaidia kuinua uchumi wao siku za usoni.
“Nashukuru sana kwa Inpekta Shabani Jumbe kutoa elimu hii binafsi nimeifurahia na kuongeza ufahamu kwa upande wangu hali iliyonipa hamasa ya kuchukua fomu na kuongeza akiba yangu toka 10% hadi 50% kwa mwezi”. Alisema Asia Matauka ambaye ni Mkaguzi wa Polisi na kushauri kwamba wajenge matawi katika mikoa yote.
“Baada ya kupata elimu nimegundua kwamba Chama hiki cha ushirika ni chama muhimu sana kwa askari na mimi nimeamua kuongeza akiba yangu toka elfu 10 hadi elfu 80 kwa mwezi” .Alisema D/C Anzelim toka wilaya ya longido.

TAHADHARI YA JESHI LA POLISI KUHUSU MKESHA WA MWAKA MPYA

BUL
Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha  mwaka mpya wa  2016, wananchi hutumia muda huo kwenda  katika nyumba za ibada ama kusherekea katika maeneo mbalimbali ya starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo  vinavyohatarisha usalama wa raia mali zao.
Jeshi la Polisi nchini, limejipanga vizuri katika mikoa yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kwamba vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza  hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mkesha wa mwaka mpya vinadhibitiwa. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Aidha,  Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara. Simu za polisi endapo mwananchi atakuwa na taarifa ni 111 au 112.
 Pia,  Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabar
ani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Vilevile, wananchi kuacha tabia ya kuchoma matairi barabani pamoja na kupiga mafataki. Aidha, yeyote atakayefanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Nawatakieni watanzania wote kheri ya mwaka mpya.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.        

MKUTANO WA TUME YA PAMOJA YA FEDHA (JFC) WAFANYIKA LEO OFISI YA MAKAMU WA RAIS

ua1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba (mbele), akitafakari jambo wakati wa kikao cha kujadili changamoto na utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) jijini Dar es Salaam leo,  kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Abdulrahaman Jumbe. (Picha na OMR)
ua2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) katika Mkutano wa kujadili changamoto na utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo. (Picha na OMR)

Benki ya maendeleo ya kilimo kuanzisha ofisi za kanda

tab1
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Benki, Bibi Neema Christina John (aliyevaa miwani) wakati wa uhakiki wa fomu zilizojazwa na moja kati ya vikundi vilivyofanikiwa kupata mkopo kutoka Benki hiyo.
tab2
Mwanasheria mwandamizi wa TADB, Bibi Salome Masenga (Kulia) akimuelekeza mmoja wa wanakikundi waliopata mikopo kutoka Benki hiyo.
tab6
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bw. Kasunga (Kulia).
tab7 tab10
Picha ya pamoja
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu, Iringa
Benki mpya ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema hadi kufikia miaka mitano ijayo itakuwa imefungua ofisi sita za kikanda zenye lengo la kuwahudumia wakulima nchi kote.
Mikakati hiyo iliwekwa bayana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa, katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Bibi Kurwijila alisema kuwa TADB inalenga kutelekeza kwa vitendo Maelekezo ya Serikali ya kupunguza changamoto zinazowakabili wakulima nchi kote.
Aliongeza kuwa kwa sasa Benki inalenga kusambaa nchi nzima kwa kuanzisha Ofisi za Kikanda ndani ya miaka mitano ijayo.
“Tunalenga kuwafikia wakulima wote nchini kadri siku zinavyoendelea kwenda na kutegemea mtaji unavyoongezeka ama upatikanaji wa fedha toka vyanzo mbali mbali ili kuweza kuwawezesha kumudu shughuli zao za kilimo,” alisema.
Aliongeza kuwa Benki inaleenga kuwajengea uwezo na kuanzisha Programu Maalumu ya Vijana wajihusishao na shughuli za Kilimo cha kibiashara na kushirikiana na wadau wengine kuhuisha shughuli za umwagiliaji na miradi ya kisasa ya umwagiliaji.
Malengo mengine ni kutafuta fedha toka vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha Wakulima katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye mazao ya Kilimo na kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na Minne (14) ya Mwanzo na kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia kuwaunganisha Wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kwamba Benki yake imedhamiria kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini ili kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Bw. Samkyi alisema TABD imejizatiti kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mapinduzi ya kilimo kwa kuongeza tija na upatikanaji wa mikopo ya riba nafuu maalum kwa sekta ya kilimo, kama njia ya kuleta Mapinduzi yenye tija kwa wakulima nchini.
“Benki imejipanga kutoa mikopo yenye riba nafuu katika muda mfupi, wa kati na mrefu kwa Wakulima wadogo wadogo,  wa kati na wakubwa, hususan kuziba pengo la upatikanaji wa fedha za kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani katika tasnia za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu (ufugaji nyuki),” alisema Bw. Samkyi.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba kwa kuanzia walengwa wakuu wa TADB ni wakulima wadogo wadogo, hatahivyo, hata wale wakulima wa kati na wakubwa watahudumiwa.
Bw. Samkyi imejidhatiti katika kufanya tathmini ya kina katika mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi kwa minajili ya kuongeza thamani na ushindani kwenye masoko.
“Sera ya TADB ni kutathmini mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi, na ambayo utatuzi wake utaongeza tija na uwezo wa ushindani kwenye masoko, na hivyo kukuza uchumi wa walio wengi na kupunguza umaskini,” aliongeza.
Katika hafla hiyo, jumla ya vikundi nane (8) vyenye jumla ya wakulima wadogo wadogo 857, vilimiza vigezo na kupewa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja.
Kwa mujibu wa Bw. Samkyi kabla ya kutoa mikopo hiyo, benki iliwatembelea na kutoa elimu kwa wakulima jinsi ya kuimarisha vikundi vyao, ambapo jumla ya vikundi 89 vyenye jumla ya wanakikundi 21,526 vilifikiwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mama Amina Masenza amewaasa Wakulima wote nchini kutumia vizuri mikopo wanayopewa ili kuweza kutimiza malengo yao binafsi na ya Serikali katika kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania.
Mama Masenza alisema kuwa wakulima wakitumia mikopo waliyopewa kwa malengo husika watafika mbali na kuweza kuchagiza mikakati ya Benki hiyo katika kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kilimo kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
“Naamini, wakati Benki ya Maendeleo ya Kilimo itapoanza kufanya tathmini ya mikopo hii iweze kuona matunda ya uwekezaji wake hasa kwa nyie ambao mmeweza kubahatika kupata fursa ya awali kabili kunufaika na huduma za TADB,” aliwasihi.
Mama Masenza aliwaomba  wakulima hao kuwa Mfano Bora na wanaojitambua vilivyo, hasa nia ya kutoka katika kiwango fulani cha maisha kwenda katika hatua nyingine za juu zaidi kimaisha kwa kuongeza kipato na ubora wa kimaisha kwa ujumla kupitia huduma za TADB.
“Nawasihi kutotumia pesa hizi kinyume na malengo yaliyokusudiwa, kwani kwa kufanya hivyo, siyo tuu tunaiua Benki yetu bali pia tunajimaliza wenyewe kiuchumi. Wito wangu kwenu ni kujipanga kwa dhati ili kuweza kutimiza malengo makuu ya mikopo hii ambayo ni kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini,” aliongeza.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ilizinduliwa Rasmi na Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima nchini, mnamo tarehe 8 Agosti 2015 mjini Lindi. Uanzishwaji wa Benki hii ni utekelezaji wa malengo ya muda mrefu ya Serikali, katika kuitikia wito wa wananchi na wadau wengine wa maendeleo ili Tanzania iweze kupiga hatua endelevu

Droo ya nne ya promosheni ya “Jaza Mafuta na Ushinde” ya GAPCO yafanyika jijini Dar es Salaam

Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (katikati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya nne ya promosheni ya “Jaza Mafuta na Ushinde” inayowawezesha wateja wake kujipatia lita 40 za mafuta kwa kila mshindi wa droo hiyo kila wiki. Kulia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, na kushoto ni Meneja wa Fedha wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania, Michael Chobu.

Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde afanya ziara makao makuu ya Tigo leo


Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  akizungumza na wafanyakazi wa tigo baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijtonyama  jijini Dar es laam 
Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari na wafanyakazi wa tigo   baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijitonyama Dar es laam 
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez , akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika mkutano alioshiriki pia Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  baada ya kufanya ziara katika makao  makuu ya Tigo Kijtonyama  jijini Dar es laam
……………………………………………………………………………………………………………………
Tigo Tanzania leo imepokea kwa furaha ugeni wa ghafla wa Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Kijitonyana jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mavunde ambaye alikuwa ameongozana na waandishi wa habari na maofisa kutoka ofisi za uhamiaji alitinga ofisini hapo mnamo saa nne asubuhi ya Jumatano ya tarehe 30 Desemba na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni ya Tigo.
Bwana Gutierrez alimtembeza Naibu Waziri kwenye idara mbalimbali za kampuni hiyo huku akitambulisha huduma zinazotolewa na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na Mhe. Waziri.
Kampuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa, kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.
Bwana Gutierrez alisema kampuni ya Tigo imefurahishwa mno na ugeni huo huku akiongeza kuwa ugeni huo unadhihirisha kwamba serikali imeonesha kwamba inajali huduma zinazotolewa na mashirika ya sekta binafsi.
Bwana Gutierrez alisema “Tutaendelea kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko lukuki kwenye maisha ya watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Tigo imejikita kwenye kupanua wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye uhakika”.
Kuhusu kuitembelea Tigo, Mh. Mavunde alisema: “leo tumetembelea kampuni ya Tigo, kwa ajili ya kujitosheleza vipi kampuni hii inajali waajiri wake, na katika ziara hii tumebaini mambo kadha ambayo tungependa kampuni ya Tigo, ivifanyie kazi kwa mfano kwenye maswala ya afya na usalama, na pia tungependa kuona mikataba baina ya Tigo na watoa huduma wake, pia serikali ya awamu ya tano, ipo makini kuhakikisha sheria inafuatwa ili tuwe na jamii inayozingatia sheria”

JK,WAZIRI LWENGE WAKAGUA MITAMBO YA MAJI WAMI,CHALINZE

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.
Rais Jakaya Kikwete na Lwenge wakiangalia mitambo ya kusafisha maji
Wakiwa katika picha ya pamoja
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete , akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge (kushoto kwake) wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akionesha kitu walipotembelea mitambo ya maji Wami
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge katika mitambo hiyo.

RAIS MAGUFULI ATANGAZA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

GUL1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakisikiliza kwa makini.
GUL2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonesha orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakishuhudia.
GUL3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonesha orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakishuhudia
GUL4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Mara baada ya kumkabidhi orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliwateua leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha zote na IKULU
………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
 1. Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi – Ombeni Sefue
 1. Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo
 1. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro
 1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu – Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu – Elimu)
 1. Ofisi ya Makamu wa Rais
            Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
            Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)
 1. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu – Sera)
 1. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu – Kilimo)
Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
Dkt. Budeba (Katibu Mkuu – Uvuvi)
 1. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu – Ujenzi)
Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu – Uchukuzi)
Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu – Mawasiliano)
Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)
 1. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)
Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)
 1. Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)
Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)
 1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu – Viwanda)
Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu – Biashara na Uwekezaji)
Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)
 1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)
Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)
 1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu – Afya)
Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu – Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)

Mhe. Kairuki aendelea na ziara katika taasisi zilizo chini ya ofisi yake kuhimiza uwajibikaji

UT3
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
UT1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
UT2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
UT4
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitazama nyaraka inayoandaliwa kutunzwa katika nakala laini (soft copy) alipoitembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mapema leo.
UT5
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akitazama moja ya kifaa cha kutunzia kumbukumbu  alipoitembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mapema leo.

WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA MAOFISA BIASHARA MANISPAA DODOMA

????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na  Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.
Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.
Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
Katika uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha  Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.
Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.
Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Imetolewa na:
Rebecca Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais – TAMISEMI
30 Desemba, 2015

Watakaofanya fujo mkesha wa mwaka mpya kukiona

4 (1)
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha wananchi kutokufanya fujo wakati wa  mkesha wa mwaka mpya kwa kuweka mikakati mikali kwa watakaokaidi amri hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amepiga marufuku uchomaji wa matairi ya gari,  upigaji baruti, risasi za moto na fataki ambazo zaweza kusababisha madhara wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
“ Ni baraka zaidi kusherekea sherehe kama hizi kifamilia na sio vizuri kuingia mwaka mpya ukiwa mahabusu, huo ni mkosi” Alisema Kamishna Kova.
Kamishna Suleiman Kova aliongeza kuwa watashirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jeshi la Zimamoto, kampuni binafsi za ulinzi, vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na kutumia ndege za Polisi kufanya doria ili kuhakikisha kuwa wanailinda amani na kudhibiti aina yoyote ya uhalifu utakaojitokeza.
Aidha Kamishna Kova amesisitiza kuwa vituo vyote vya polisi vitakuwa wazi masaa 24 ili kuwawezesha wananchi kutoa taarifa haraka pindi wanapopata matatizo au wanapoona dalili zozote za uvunjifu wa amani pia amehakikisha kuwa fukwe zote za bahari na maeneo  yote yenye mikusanyiko yatalindwa.
Katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka wa 2015 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limetoa rai kwa wananchi kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa haraka pindi waonapo dalili za uvunjifu wa amani.

WAZIRI WA AFYA ,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AFANYA ZIARA BOHARI YA DAWA (MSD)

UY1
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Prof.Idris Mtulia
UY2
Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo
UY3
Waziri huyo akiendelea na ukaguzi wa maghala hayo ,kulia ni Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja na kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya Bohari hiyo
UY4
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiangalia dawa zilizowekwa nembo ya serikali (GoT) ambayo itasaidia udhibiti wa upotevu wa dawa nchini
UY6
Mkurugenzi wa MSD Bwanakunu akieleza dira,malengo na majukumu ya Bohari hiyo
UY8
Waziri huyo akionesha kopo la dawa la Bohari ya dawa
UY9
Waziri Ummy akimuonesha ukurasa wa ugawaji fedha za bohari  Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya dawa Prof.Idris Mtuliya(Picha zote kwa Niaba ya Wizara ya Afya)
…………………………………………………………………………………
 Waziri wa Afya , Maendeleoya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Waziri huyo ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD.
Mbali na hilo, waziri huyo wa Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya Hospitali, vituo vya Afya na zahanati kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisistiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.
Katika hatua nyingine ameishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.
Waziri huyo ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake na watendaji wengine alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa ya Makao Makuu, jengo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimenti ya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na mengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na Mwanza.
Waziri Ummy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia