TAASISI ya Utafiti ya Uchumi na Jamii (ESRF)
imewakutanisha wasomi na wawakilishi wa taasisi za umma na kibinafsi
kuchambua bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Sekta ya Afya na
Viwanda ili kuona inavyoweza kutatua changamoto zinazokabili Sekta hizo
kwenye mdahalo uliokutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na
Binafsi na kufanyika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Akifungua
mdahalo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Tausi Kida
alisema, Taasisi yake imeona ni vema kuwakutanisha wadau kujadili bajeti
hiyo katika sekta ya Afya na Viwanda, kwa vile zinagusa uchumi wa
wananchi.
Akiwasilisha
mada juu ya bajeti ya Serikali 2016/2017na changamoto zinazoikabili
sekta ya Afya, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi
Shirikishi, Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja alisema,
ingawa bajeti iliyotengwa kwenye sekta ya Afya ni kubwa, lakini bado
kuna changamoto kadhaa kwa vile Wizara hiyo imepanuka kutokana na
kuhudumia maeneo mengi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi
Kida, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mdahalo uliolenga kujadili changamoto
zinazoikabili bajeti ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Afya na
Viwanda, kwenye makao makuu ya ESRF jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo
umewakutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi. (Picha
zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
Profesa
Mujinja alitolea mfano wa ununuzi wa madawa ambapo, zaidi ya asilimia
90 ya madawa yanayotumika huagizwa kutoka nje na hivyo fedha nyingi za
kigeni hutumika.
Katika
majumuisho yake, Profesa Mujinja alisema, ni vema Serikali ielekeze
nguvu zake kwenye uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha madawa na vifaa
tiba hapa nchini ili kwenda sambamba na malengo ya taifa ya maendeleo
endelevu.
Akizungumzia
kuhusu changamoto za bajeti kwenye eneo la Viwanda, muwasilisha mada
Profesa Prosper H. Ngowi kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es
Salaam, alisema, fedha zilizotengwa kwenye Sekta ya Viwanda ni Shilingi
Bilioni 81, 871,992,000, ambapo asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya
kawaida na asilimia 49 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kwa
mtazamo wake, Profesa Ngowi alisema, mgawanyo huo ni mzuri na sio kwa
kiwango kikubwa kwani hakuna tofauti na bajeti ya mwaka 2015/2016, na
kuonyesha wasiwasi wake muda ambao Serikali inatoa fedha hizo kuhudumia
maeneo yaliyokusudiwa.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Cha
Muhimbili, Profesa Phares Mujinja, akitoa mada juu ya changamoto
zinazoikabili bajeti ya Serikali ya 2016/2017 kwenye Sekta ya Afya
wakati wa mdahalo huo.
“Bajeti
ya 2016/2017 ni Asilimia 70.3% ya ile ya 2015/2016 na kwamba wizara
hivi sasa ni kubwa kutokana na kuongezeka kwa sekta ya Uwekezaji.”
Alifafanua.
Wakichangia
mada hizo, wengi wa washiriki wameonyesha wasiwasi wao kuhusu
kufanikiwa kwa malengo ya serikali kwenye Sekta hizo kutokana na
muonekano wa bajeti yenyewe na mahitaji halisi ya sasa ya utoaji huduma
kwenye Sekta hizo ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa nchi
kumekuwepo kwa mtazamo kuwa biashara nchini zinaanguka kutokana na mkazo
wa kukusanya mapato.
Akifunga
mdahalo huo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Ujenzi wa Maendeleo
wa ESRF, Doris Likwelile, aliwashukuru washiriki kwa michango yao
mbalimbali na kwamba mawazo yao yatawezesha utayarishaji wa mtazamo wa
wadau kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 kwenye Sekta hizo
mbili za Afya na Viwanda.
WAZIRI MKUU: WAKURUGENZI WATAKAOTOA TAARIFA ZA UONGO KUONDOLEWA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitasita kuwaondoa katika
nyadhifa zao Wakurugenzi wote watakaoshiriki katika kutoa taarifa za
uongo kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo
yao.
“Serikali
inatoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo kuna
baadhi ya viongozi wamekuwa wakiandika taarifa za uongo kuwa mradi
umekamilika wakati haujajengwa, hivyo wakurugenzi watakaoshiriki kutoa
taarifa zisizokuwa sahihi wataondolewa,” alisema.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo jana jioni (Jumapili, Julai 31, 2016) wakati
akipokea taarifa ya mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili mkoani hapa
kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Alisema
alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakurugenzi katika halmashauri zote
nchini kuhakikisha wanatembelea miradi yote inayojengwa katika maeneo
yao ili kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama thamani yake inalingana na
kiasi cha fedha kilichotolewa.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Serikali aihitaji Halmashauri kutoa
ajira za mikataba kwenye kada zilizopo katika muundo wa ajira hivyo
ameziagiza halmashauri zote nchini kufanya mapitio ya watumishi wa
mikataba.
“Tumeruhusu
kuajiri kwa mikataba walimu wa masomo ya sayansi kwa kipindi cha miaka
miwili tena kwa waliostaafu. Kuna kada zilizoko katika muundo wa ajira
hizo hatuhitaji watumishi wa mikataba wakiwemo madereva msiwatumikishe
kwa mikataba watakosa stahili zao,” alisema.
Akizungumzia
suala la watumishi hewa mkoani Morogoro Waziri Mkuu alisema ni vema
wakaendelea kufanya uchunguzi na ifikapo mwisho wa mwezi huu wawe
wamekamilisha taarifa na kuanza kuchukua hatua kwa waliohusika kwa
waliohusika.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe katika taarifa
yake aliyoiwasilisha kwa Waziri Mkuu alisema mkoa unaendelea kutekeleza
agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuzitaka taasisi zote za Serikali
kufanya uhakiki wa mishahara hewa na malipo batili ya watumishi.
Alisema
mkoa umebaini watumishi hewa 315 ambao wameisababishia Serikali hasara
ya sh. bilioni 2.132 ambapo timu ya uhakiki bado inaendelea na zoezi
hilo na taarifa kamili itatolewa mara kazi hiyo itakapo kamilika.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, AGOSTI 01, 2016.
RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOHUTUBIA MKUTANO GEITA MJINI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
mamia ya wakazi wa Geita mjini mara baada ya kuwasili kutoka Kahama.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka
katika viwanja vya mikutano vya Geita mjini mara baada ya kuhutubia.
Wananchi wa Geita wakionesha furaha yao wakati Rais Dkt. Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano viwanjani hapo.
PICHA NA IKULU
TAASISI ZATAKIWA KUANZISHA MFUMO WA KUPIMANA
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa (Kulia)
wakati alipotembelea ofisini kwake kupata taarifa ya hali ya miundombinu
katika mkoa huo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa
Mbeya Eng. Paul Lyakurwa wakati alipokagua barabara ya Ikana-Makamba
–Chitete iliyopo mkoa wa Songwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua kituo cha kukuza mawimbi ampilification station kilichopo
miangalau mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Meneja wa kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL) Mkoa wa Katavi na Rukwa Bw. Peter Kaguru.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Stephen akitoa taarifa ya hali ya Miundombinu
katika mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa wakati alipomtembelea ofisini kwake.
MKUTANO WA LOWASSA NA WANAFUNZI MUHIMBILI WAZUILIWA
Na Dotto Mwaibale
……………………..
UONGOZI
wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia
mkutano uliokuwa ufanywe na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na Waziri
Mkuu wa zamani Edward Lowaasa.
Mkutano
huo ambao ulikuwa ufanyike na baadhi ya vijana wa kikristo ambao ni
wanafunzi wa chuo hicho ulikuwa pangwa kufanyika juzi chuoni hapo
kuanzia saa za mchana.
Akizungumza mtandao wa www. habari za jamii.com
mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema
maandalizi yote ya mkutano huo ambao ulikuwa baada ya ibada yalikuwa
yamekamilika.
“Tulifanya
taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo
ambao ulitukubalia na kumualika ndugu Lowassa lakini tumeshangazwa na
zuio lililotolewa na uongozi wa chuo” alisema mwanafunzi huyo.
Mwanafunzi
huyo alisema kuwa saa sita mchana wakati wakimsubiri mgeni rasmi Edward
Lowassa awasili mkuu wa chuo hicho na viongozi wengine waliwaita na
kuwaeleza kwamba mkutano huo umewekewa zuio kutoka juu hivyo
hautafanyika bila ya kutoa sababu .
Msemaji
wa Lowassa Abubakar Lihongo alisema wanafunzi hao baada ya kuzuiliwa
kufanya mkutano huo walimuomba radhi Lowassa na kumueleza watamualika
tena kipindi kingine wakiwa tayari.
“Mimi
naona zuio hilo linatokana na masuala ya kisiasa lakini kuna barua ya
wanafunzi hao ipo katika mitandao ya kijamii mkiipata mnaweza kupata
picha halisi” alisema Liongo.
No comments :
Post a Comment