
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim
Mgandilwa akiambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya
Ruangwa Leo tarehe 28/01/2020 ameshiriki katika tukio la
kuokoa watu
walioishi katika miti kwa siku tano bila ya kupata chakula.
Watu watatu kutoka familia moja
wameishi juu ya mti tangu tarehe 24/1/2020 ambapo mvua kubwa ilianza
kunyesha iliopelekea kufurika kwa maji kutokea mto mbwemkuru
Akizungumza Mara baada ya kuwaokoa
watu hao mkuu wa wilaya ya Ruangwa amewashukuru wananchi kwa kuendelea
kujitoa katika kuwatafuta watu hao hadi kuwapata wakiwa juu ya miti,huku
wakiwa hai.
Mkuu wa wilaya amesema huu ni mfano wa kuigwa na jamii kwa kuwa na umoja wakati wa matatizo.
Mwisho mkuu wa wilaya ya Ruangwa
ameendelea kuwaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuendelea kuchukua
tahadhari na waangalifu katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha
No comments :
Post a Comment