Katibu Mtendaji
wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Prof. Charles Kihampa akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Tume hiyo
katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, mkutano huo ulifanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es
Salaam Januari 28, 2020.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo
Vikuu Nchini (TCU), Prof. Charles Kihampa akizungumza na Waandishi wa
Habari (pichani), kuhusu mafanikio ya Tume hiyo katika miaka minne ya
Serikali ya Awamu ya Tano, mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam Januari 28,
2020.
(Picha na Idara Habari-MAELEZO).
………………
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
TUME ya Vyuo
Vikuu Tanzania (TCU) katika kipindi cha mwezi Novemba 2015 hadi Novemba
2019 imefanya uhakiki na utambuzi wa uhalali wa vyeti 8328 vya
wahitimu
waliotunukiwa tuzo zao na vyuo vikuu vilivyo nje ya Tanzania.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa vyombo vya habari leo Jumanne (Januari
28, 2020) Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles
Kihampa alisema kutokana na kuimarika kwa mifumo ya kieletroniki, TCU
imefanikiwa kupunguza muda wa uhakiki na utambuzi wa vyeti hivyo kutoka
siku 14 za awali hadi siku tatu.
Prof. Kihampa
alisema TCU imeimairisha mifumo yake ya kielektroniki ambayo imeongeza
ufanisi katika utendaji kazi kwa kuboresha huduma inazotoa kwa wateja na
wadau wake kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma kwa wateja.
‘’Katika kipindi
hiki, zaidi ya maombi 1,077 ya hati ya kutokuwa na pingamizi kwa
wanaotaka kwenda kusoma elimu ya juu nje ya nchi, yamewasilishwa TCU na
kushughulikiwa na mfumo huu ni muhimu kwani unawapa fursa wananchi
kufahamu uhalali wa programu wanazokwenda kusoma, hivyo kuwaepusha
kupoteza rasilimali fedha za kusoma katika vyuo visivyotambulika’’
alisema Prof. Kihampa.
Aidha Prof.
Kihampa alisema kupitia miongozo yake TCU imeweza kusajili Wakala tatu
zinazodahili wanafunzi wanaotaka kusoma elimu ya juu nje ya Tanzania, na
kuzitaja wakala hizo ni pamoja na Global Education Link Ltd, DARWIN
Education Agency Ltd na Yahoma Educational Ltd, pamoja na kupokea maombi
ya wakala nyingine 7 zinazosubiri taratibu za usajili.
Prof. Kihampa
alisema kwa mujibu muongozo huo, wakala wote hutakiwa kuwa na mikataba
maalum baina yao na vyuo vilivyopo nje pamoja na Cheti maalum (NOC), na
hivyo kuwataka wakala wote waliokidhi vigezo hivyo kutuma maombi yao TCU
na kukamilisha usajili kwa wakati.
Katika hatua,
nyingine Prof. Kihampa alisema katika kusimamia ubora wa elimu
inayotolewa na vyuo vikuu nchini, kati ya kipindi cha mwezi Oktoba 2016
hadi Januari 2017, TCU ilifanya ukaguzi maalum wa kitaaluma kwa taasisi
64 za vyuo vikuu, vyuo vikuu vishiriki na vituo vya vyuo vikuu ili
kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango vya kitaifa, kikanda na
kimataifa.
‘’Matokeo ya
ukaguzi yalibainisha kasoro mbalimbali katika uendeshaji wa vyuo vikuu
nchini, vyuo 45 vilikutwa na kasoro ndogondogo, vilipewa ushauri na
viliweza kurekebisha katika kipindi kifupi vikaendelea na utoaji wa
elimu ya juu na vyuo 19 vilikutwa na kasoro kubwa, vilipewa ushauri na
muda wa mrekebisho’’ alisema Prof. Kihampa.
Kwa mujibu wa
Prof. Kihampa alisema hadi sasa vyuo vikuu 9 kati ya 19 vilivyositishwa
udahili vimefanya marekebisho makubwa na vimeruhusiwa kudahili na
kuendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya programu za masomo, na kuvitaja
vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania
(UAUT), Chuo Kikuu cha Teofila Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu Kishiriki cha
Askofu Mkuu Mihayo Tabora (AMUCTA), Chuo Kikuu Kishirishi cha Marian
(MARUCo).
Anavitaja vyuo
vingine ni Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Nchini Tanzania (KIUT),
Chuo Kikuu Kishiriki cha Kikristo cha Tiba Kilimanjaro (KCMUCo), Chuo
Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stephano- Moshi (SMMUCo) na Chuo Kikuu
Kishiriki cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Mt. Fransisko (SFUCHAS).
Anaongeza kuwa
mifumo ya ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara imefanya vyuo kufanya
maboresho makubwa katika miundombinu ya kufundisha na kujifunzia ikiwa
na pamoja na ujenzi wa maabara za kisasa, mifumo ya mawasiliano ya
kielektroniki, madarasa na kuongeza idadi ya viongozi na wahadhiri wenye
sifa.
TCU YAFANYA UHAKIKI NA UTAMBUZI WA VYETI 8328 VYA WAHITIMU WA VYUO VYA NJE
Katibu Mtendaji
wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Prof. Charles Kihampa akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Tume hiyo
katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, mkutano huo ulifanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es
Salaam Januari 28, 2020.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo
Vikuu Nchini (TCU), Prof. Charles Kihampa akizungumza na Waandishi wa
Habari (pichani), kuhusu mafanikio ya Tume hiyo katika miaka minne ya
Serikali ya Awamu ya Tano, mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam Januari 28,
2020.
(Picha na Idara Habari-MAELEZO).
………………
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
TUME ya Vyuo
Vikuu Tanzania (TCU) katika kipindi cha mwezi Novemba 2015 hadi Novemba
2019 imefanya uhakiki na utambuzi wa uhalali wa vyeti 8328 vya wahitimu
waliotunukiwa tuzo zao na vyuo vikuu vilivyo nje ya Tanzania.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa vyombo vya habari leo Jumanne (Januari
28, 2020) Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles
Kihampa alisema kutokana na kuimarika kwa mifumo ya kieletroniki, TCU
imefanikiwa kupunguza muda wa uhakiki na utambuzi wa vyeti hivyo kutoka
siku 14 za awali hadi siku tatu.
Prof. Kihampa
alisema TCU imeimairisha mifumo yake ya kielektroniki ambayo imeongeza
ufanisi katika utendaji kazi kwa kuboresha huduma inazotoa kwa wateja na
wadau wake kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma kwa wateja.
‘’Katika kipindi
hiki, zaidi ya maombi 1,077 ya hati ya kutokuwa na pingamizi kwa
wanaotaka kwenda kusoma elimu ya juu nje ya nchi, yamewasilishwa TCU na
kushughulikiwa na mfumo huu ni muhimu kwani unawapa fursa wananchi
kufahamu uhalali wa programu wanazokwenda kusoma, hivyo kuwaepusha
kupoteza rasilimali fedha za kusoma katika vyuo visivyotambulika’’
alisema Prof. Kihampa.
Aidha Prof.
Kihampa alisema kupitia miongozo yake TCU imeweza kusajili Wakala tatu
zinazodahili wanafunzi wanaotaka kusoma elimu ya juu nje ya Tanzania, na
kuzitaja wakala hizo ni pamoja na Global Education Link Ltd, DARWIN
Education Agency Ltd na Yahoma Educational Ltd, pamoja na kupokea maombi
ya wakala nyingine 7 zinazosubiri taratibu za usajili.
Prof. Kihampa
alisema kwa mujibu muongozo huo, wakala wote hutakiwa kuwa na mikataba
maalum baina yao na vyuo vilivyopo nje pamoja na Cheti maalum (NOC), na
hivyo kuwataka wakala wote waliokidhi vigezo hivyo kutuma maombi yao TCU
na kukamilisha usajili kwa wakati.
Katika hatua,
nyingine Prof. Kihampa alisema katika kusimamia ubora wa elimu
inayotolewa na vyuo vikuu nchini, kati ya kipindi cha mwezi Oktoba 2016
hadi Januari 2017, TCU ilifanya ukaguzi maalum wa kitaaluma kwa taasisi
64 za vyuo vikuu, vyuo vikuu vishiriki na vituo vya vyuo vikuu ili
kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango vya kitaifa, kikanda na
kimataifa.
‘’Matokeo ya
ukaguzi yalibainisha kasoro mbalimbali katika uendeshaji wa vyuo vikuu
nchini, vyuo 45 vilikutwa na kasoro ndogondogo, vilipewa ushauri na
viliweza kurekebisha katika kipindi kifupi vikaendelea na utoaji wa
elimu ya juu na vyuo 19 vilikutwa na kasoro kubwa, vilipewa ushauri na
muda wa mrekebisho’’ alisema Prof. Kihampa.
Kwa mujibu wa
Prof. Kihampa alisema hadi sasa vyuo vikuu 9 kati ya 19 vilivyositishwa
udahili vimefanya marekebisho makubwa na vimeruhusiwa kudahili na
kuendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya programu za masomo, na kuvitaja
vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania
(UAUT), Chuo Kikuu cha Teofila Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu Kishiriki cha
Askofu Mkuu Mihayo Tabora (AMUCTA), Chuo Kikuu Kishirishi cha Marian
(MARUCo).
Anavitaja vyuo
vingine ni Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Nchini Tanzania (KIUT),
Chuo Kikuu Kishiriki cha Kikristo cha Tiba Kilimanjaro (KCMUCo), Chuo
Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stephano- Moshi (SMMUCo) na Chuo Kikuu
Kishiriki cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Mt. Fransisko (SFUCHAS).
Anaongeza kuwa
mifumo ya ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara imefanya vyuo kufanya
maboresho makubwa katika miundombinu ya kufundisha na kujifunzia ikiwa
na pamoja na ujenzi wa maabara za kisasa, mifumo ya mawasiliano ya
kielektroniki, madarasa na kuongeza idadi ya viongozi na wahadhiri wenye
sifa.
No comments :
Post a Comment