
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imesema
jumla ya watoto 36,548 wamepatiwa huduma mbalimbali zikiwemo huduma
za kisaiklojia ,huduma za afya,huduma za elimu pamoja msaada wa kisheria
katika
kipindi cha Januari hadi Disemba mwaja Jana wakiwemo wa kiume
17,894 na wa kike 18,654 walitambuliwa ,kati ya hao jumla ya
watoto 1,178 [wa kiume 768 na wa kike 410] walipatiwa huduma
mbalimbali zikiwemo afya ,kisaklojia,kijamii na kuunganishwa na familia
zao na kupatiwa elimu ya ujasiriamali.
Hayo
yamebainishwa leo Januari 28,2020 bungeni jijini Dodoma na Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii ,jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.Faustine
Ndugulile wakati akijibu Swali la mbunge wa viti Maalum Sikudhani
Yasini Chikambo aliyehoji ,kumekuwa na wimbi kubwa la watoto
wanaoishi mtaani ,ambao wanaishi katika mazingira magumu ,je,serikali
ina mpango gani wa kuwasaidia watoto hao.
Katika Majibu
yake,Naibu wa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
,Dkt.Faustine Ndugulile amesema serikali inatekeleza Program ya
kuwaunganisha watoto na Familia na kuwatafutia malezi mbadala wale wasio
na familia katika mkoa wa Mwanza.
Aidha,Dokta
Ndugulile amesema Program hiyo ilianza kutumika mwezi Nov.2019 na
inatarajia kufika mikoa yote ambayo ina wimbi la watoto wanaoishi
mitaani huku pia akiikumbusha jamii kuwa jukumu la malezi,ulinzi na
matunzo ya watoto ni la familia na jamii kwa ujumla.
Katika hatua
nyingine Dokta Ndugulile amesema mamlaka za serikali za mitaa zinapaswa
kusimamia sheria ya motto Na.21 ya mwaka 2009 ili kuwajibika
wazazi kutekeleza majukumu yao badala ya kuwatelekeza watoto na
kuwaacha wakizurura mitaani.
No comments :
Post a Comment