……………………………………………………………………………………………………………
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mamlaka ya
mawasiliano nchini TCRA Kanda ya kaskazini imewataka mafundi wa vifaa
vya kieletroniki ikiwemo simu za mkononi kuwa kwenye mfumo wa umoja kwa
kuanzisha vikundi vyao kwa Kanda au mkoa.
Kwa muktadha huo
kuanzia mwezi julai mwaka huu hakuna fundu ambaye atafanyakazi kama
hajasomo wala kusajiliwa hivyo ni muhimu kwenu kujiunga kwenye kikundi
ili kupatiwa elimu.
Kauli hiyo imetolewa
na Mwanasheria wa mamlaka hiyo Kant Mosha wakati wa mkutano wa mafundi
wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa
mkoa wa Arusha ambapo aliwataka kuacha kutokuwa na usajili wa kikundi
ndio suluhisho.
Alisema kuwa mafundi
simu ni kada ambayo ilikuwa imesahauliwa hapo awali lakini kupitia
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais dkt.John Magufuli imeamua
kuwatambua hivyo kuungana ni sehemu ya kufanikiwa kwa malengo yenu.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa chama cha mafundi simu Kanda ya ziwa Maguwa Manyanda
amewataka kutambua kwamba mafundi simu ni wathamani kwani jamii
inwategemea na wanachangia mapato ya serikali hivyo busara ni kuona
umoja ndio suluhisho la changamoto zao.
Alisema kuwa mafunzo
hayo yataondoa changamoto na kuwafanya kuwa huru katika shughuli zao za
kila siku hivyo umoja ni nguzo ya kuwafikisha kuweza kushirikiana na
serikali katika masuala mbalimbali ikiwemo vyombo vya Dola.
Alieleza kuwa
kufanikiwa ili kila moja aweze kutenda kazi zake ni muhimu Sana
wakajiunga na umoja ili kuondoa changamoto zao ambazo zimekuwa
zikiwafanya kujikuta wakikumbana na jeshi la polisi.
Nae Mwenyekiti wa
umoja wa mafundi simu Kanda ya kaskazini Nasri Mshana Mtengeti alisema
kuwa wamefirahi Sana kupata elimu hiyo ya umoja ambayo itawasaidia
kuondokana na changamoto hivyo tuhamasishane kujiunga na umoja huu.
Awali akitoa mafunzo
kwenye mkutano huo mratibu wa vikundi hivyo kutoka mamlaka ya
mawasiliano mhandisi Kadaya Buluhye aliwataka mafundi hao kufanyakazi
kwenye umoja kwa lengo la kupata elimu na usajili.
Alisema kuwa jeshi la
polisi linafanyakazi ya kulinda usalama na Mali za raia Ila umoja wenu
utasaidia kufanya kazi kwa karibu na jeshi hilo na kuondoa changamoto
zenu ambazo mmekuwa mkikumbana nazo kama mafundi.

No comments :
Post a Comment