Meneja Bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo
Myonga (kushoto) na Meneja Uhusino wa Kampuni ya kutengeneza simu ya
Tecno Eric Mkomoya, wakionyesha simu janja za kisasa na za gharama nafuu
aina ya Tecno Spark 3 na Tecno Spark 3 Pro zilizozindliwa jana jijini
Dar es Salaam.
Mwandishi
wa Habari kutoka Radio Times FM ya jijini Dar es Salaam Abdala Ally,
akiwa katika picha ya pamoja na Meneja bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo
Myonga (kushoto) na Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile
Tanzania Eric Mkomoya (kulia) muda mfupi baada ya kuibuka mshindi katika
droo iliyochezeshwa kwa waandishi wa habari ambapo alifanikiwa
kujishindia simu mpya ya kisasa ya Tecno Spark Pro iliyozinduliwa jana
jijini Dar es Salaam.
Meneja Bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo
Myonga (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa zimu janja mpya za kisasa na za gharama nafuu aina
ya Tecno Spark 3 na Tecno Spark Pro jijini Dar es Salaam jan. Kulia ni
Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile Tanzania Eric
Mkomoya.
Afisa
mauzo kutoka kampuni ya tecno Mobile Tanzania Neema Khamis (kushoto)
akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu mpya aina ya
Tecno Spark Pro iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo Myonga (kushoto) na Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile Tanzania Eric Mkomoya.
…………………
Na MWANDISHI WETU
Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana
na TECNO leo wamezindua simu janja mpya aina ya
TECNO Spark 3 na TECNO
Spark 3 Pro zenye ubora wa hali ya juu na ukubwa wa inchi 6.2
itakayomwezesha wateja kuweza kufanya matumizi bora ya simu janja kwa
bei nafuu kabisa.
Wateja watakaonunua simu hizi pia
wataweza kufurahia huduma ya mtandao wenye kasi kutoka Tigo pamoja na
kifurushi cha GB 96 bure watakachoweza kutumia kwa mwaka mzima.
Akizungumza wakati uzinduzi wa
simu hizo, Meneja Bidhaa za Simu kutoka Tigo, Mkumbo Myonga, alisema
Tigo inashirikiana na TECNO Mobile kuleta aina mbili za simu janja za
TECNO Spark 3 katika soko la Tanzania ili kuwafanya wateja wake
wafurahie maisha ya kidijitali.
“Moja kati ya simu tunazozindua
leo hii ina mfumo wa intanet wa 3G ambayo ni TECNO Spark 3. Simu hii
inapatikana kwa bei ya Shilingi 280,000 tu na ya pili yenye mfumo wa
intanet ya 4G inaitwa Spark 3 Pro, ikiwa inapatikana kwa Shilingi
333,000 tu. Simu zote hizi zinapatikana katika maduka yetu yote ya Tigo
nchi nzima,” alisema Myonga.
Lengo la Tigo ni kuhamasisha
maisha ya kidijitali katika jamii ya Kitanzania. Hii ndio sababu
iliyowafanya kushirikiana na TECNO Mobile ili kuweza kuongeza idadi ya
watumiaji wa simu janja na wa intanet katika soko la hapa nchini.
Kampuni hii ya mawasiliano inaamini kuwa kushirikiana na watengenezaji
wa simu ni mkakati unaoakisi lengo la kuwapatia Watanzania simu bora na
za bei nafuu.
Wakati huo huo, Meneja Mahusiano
wa TECNO Mobile, Eric Mkomoya, alisema, “Ushirikiano wetu na Tigo
umeleta mageuzi makubwa katika sekta ya mawasiliano ya kidijitali nchini
Tanzania. Pamoja, tumeweza kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za
mkononi nchini kwa kuwapatia simu janja za kisasa na kwa bei nafuu.
Kwahiyo, tunaamini ya kwamba simu hizi za TECNO Spark 3 ambazo
tunazizindua hii leo zitaweza kutoa kiwango bora cha utumiaji kwa wateja
wetu.”
Kwa maelezo ya Mkomoya, simu janja
hizi pia zinakuja na kamera ya kiwango cha juu kabisa ambayo itawezesha
wateja wanaopenda picha kuweza kupiga picha na video zenye mvuto na
ubora wa juu.
Simu ya TECNO Spark 3 inafanya
kazi katika kiwango cha 3G intanet, ina kamera ya kisasa ya Mega Pixel
13, uwezo wa GB 16 ya RAM, na skrini ya nchini 6.2. Kifaa hiki pia
kinaendeshwa kwa mfumo wa Android 9.0.
Kwa upande mwingine, simu ya TECNO
Spark 3 Pro inafanya kazi katika kiwango cha 4G LTE ya intanet, ina
kamera ya kisasa ya Mega Pixel 13, uwezo wa GB 32 ya Rom na GB 2 ya RAM,
pamoja na na skrini ya nchini 6.2.
Simu hizi zinakuja na waranti ya miezi 13.
No comments :
Post a Comment