HakiPensheni
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)
Sabra Issa Machano akizungumza na vyombo habari siku ya
uzinduzi rasmi wa sherehe za kutimiza miaka 20 kwa Mfuko wa ZSSF tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1998 pamoja na juu ya mkutano mkuu wa wadau
utakaofanyika Agosti 20, 2018.
Na
Christian Gaya, majira Ijumaa, 17 Agosti 2018
Njia
mojawapo ya wadau wa mifuko ya hifadhi ya jamii ni kufuatilia na kujua utendaji
wa mifuko hii inayosimamiwa na bodi za wadhamini kwa njia ya mikutano mikuu
inayofanyika kila mwaka. Ambapo wadau kama vile wanachama ambao ndio
wachangiaji na waaajiri...
ambao mara nyingi ndio waliodhaminiwa au wakala wa
kuhakikisha ya kuwa wanashirikiana na mifuko hii kama vile kusimamia ukataji na
kupeleka michango kwenye mifuko ya hifadhi na kuhakikisha ya kuwa wanatunza
kumbukumbu za wafanyakazi wao,
Kwa
mfano, mfuko wa hifadhi ya jamii ya Zanzibar (ZSSF) umeshaanza
kusherehekea miaka 20 tangia kuanzishwa kwake mwaka 1998 na kilele chake
kitakuwa ni kumalizia kufanya mkutano mkuu wake wa NNE wa wanachama wa mfuko na
wadau mbalimbali wa sekta ya hifadhi ya jamii utakaofanyika tarehe 20 Agosti
2018 kwa ajili ya kutathmini juu ya mafanikio na changamoto za
mfuko ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Idd.
Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar ulianzishwa chini ya kifungu cha sheria Namba 2
ya mwaka 1998 na baadaye ilirekebishwa chini ya kifungu cha Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar, Sheria Namba 9 ya mwaka 2002 na Sheria Namba 2 ya mwaka 2005.
Kabla ya kifungu cha Sheria na uanzishwaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar, kulikuwa hakuna rasmi mpango wa kinga ya hifadhi ya jamii katika nchi
ya Zanzibar
Hiki ni
kipengele mojawapo muhimu cha kuzingatia utaratibu na kanuni za utawala bora
hivyo tunaamini ya kuwa mfuko wa ZSSF utaendelea kujenga imani zaidi wakati wa
mkutano mkuu kwa wanachama na wadau kwa kuwahakikishia ya kuwa mfuko
unaendeshwa na kuongozwa na utawala bora na kwa ufanisi wa hali ya juu zaidi
kwa kuendesha mkutano kwa njia ya ukweli na uwazi
Kuna haja
ya uongozi wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa wazi kama kigezo muhimu cha
utawala bora kuthibitisha pale uamuzi unapofanywa kwa kuzingatia masilahi ya
mfuko kwanza na siyo masilahi binafsi ya viongozi.
Tunaamini
ya kuwa mfuko huu wa ZSSF unazingatia kanuni za uongozi bora na ndiyo maana kwa kufanya hivyo kumekuwa na uwezekano mkubwa kwa mfuko kuwa na utendaji mzuri
unaofikia malengo na kukidhi matarajio ya wanachama wake na familia zao.
ZSSF hivyo
tumieni nafasi hii ya mkutano mkuu wa
wadau kwa kuhamasisha kuanza kupanua
wigo zaidi wa hifadhi ya jamii kwa kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa
wanachama, wadau na kwa umma wa Tanzania kwa ujumla kwa njia ya kujenga
ushirikiano kati ya wadau ili kuhamasisha wananchi kujiunga na mifuko ya huu wa
ZSSF wa hifadhi ya jamii nchini.
Watanzania
wengine tumieni fursa hii ya wiki ya mkutano mkuu kwa wanachama na wadau nchini
kujifunza na kujielemisha juu ya uhai, utendaji, afya na ustawi wa mfuko wa
ZSSF juu ya taarifa zinazohusiana na hesabu, taarifa za ukaguzi wa mahesabu, na
taarifa za bodi ya wadhamini wa mifuko na kujua nafasi na uwezo wa mfuko
kifedha kwa njia ya magazeti, redio, luninga, blog na njia zingine za mitandao
kwani pensheni ni haki yako
ZSSF
kwa kutimiza Miaka 20 imekuwa ya mafanikio makubwa ambapo Mfuko umeweza
kutimiza majukumu yake ya kulipa mafao bila kulazimika kukopa au kuuza
rasilimali zake; kufanya shughuli zake kwa asilimia 70 kwa kutumia
teknohama iliyobuniwa na wafanyakazi wa
ndani, pamoja na hayo ZSSF imekuwa ikishiriki kwenye miradi mbalimbali ya
uwekezaji yenye manufaa kwa Taifa kiuchumi na kwa kimaendeleo ya kijamii, kwa
kupunguza umasikini kama siyo kuondoa umasikini kwa wanachama na wastaafu wake.
Christian
Gaya ni mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni Tanzania, mshauri na mtaalamu wa
masuala ya pensheni. Kwa maelezo zaidi: gayagmc@yahoo.com unaweza kutembelea www.hakipensheni
monitor online na hakipensheni blog
Simu +255 655 13 13 41 info@hakipensheni.co.tz
No comments :
Post a Comment