Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe
akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bunge leo
Jijini Dodoma.
Kutoka
kushoto ni Naibu wa Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta
Nditiye na Naibu wa Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Elias Kwandikwa wakifuatilia Hotuba ya
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha
2019/2020 leo Bungeni Jijini Dodoma.Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula na
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (katikati)
wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mkoani Mwanza, Mhe. Charles
Kitwanga wakati wa Kikao cha 24 cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo Jijini
Dodoma.Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akiteta
jambo na Manaibu Waziri wake mara baada ya kumalisha kuwasilisha Hotuba
ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bunge leo Jijini Dodoma. Kutoa
kulia ni Naibu Waziri anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Elias Kwandikwa
na Naibu Waziri anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhadisi Atashasta Nditiye. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)
No comments :
Post a Comment