Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (wanne kulia) katika picha
ya pamoja na Wanachama na Wajumbe wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa
Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association-Kinondoni)
baada ya kikao na wajumbe hao walitembelea ofisi za Bodi ya Filamu kuwatambulisha
viongozi wa chama hicho kwa uongozi wa Bodi ya Filamu hivi karibuni katika
Ofisi za Bodi ya Filamu Jijini Dar es salaam.
NA
MWANDISHI WETU
WASANII wa filamu na michezo ya kuigiza nchini wameaswa kujua thamani yao na kazi zao katika
kulinda maadili na utamaduni wa kitanzania ili kujijengea heshima mbele ya jamii
na wapenzi wa kazi zao.
Rai
hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce
Fissoo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba
wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association
- Kinondoni) walipotembelea na kufanya kikao katika Ofisi za Bodi ya Filamu Mtaa
wa Samora Jijini Dar es salaam.
Bibi.
Fissoo alisema baadhi ya wanatasnia ya filamu wanaonyesha mwenendo unaokinzana na
maisha na maadili ya kitanzania huku miongoni mwao wakifanya vitendo vinavyodhalilisha
utu na heshima hivyo kuitia doa tasnia nzima ya filamu na michezo ya kuigiza.
“Nawapongeza
Chama cha Waigizaji kwa kushirikiana na serikali katika kukemea wale wanachama wachache
wanao chafua taswira ya tasnia. Ni muhimu kuendelea kuongeza nguvu katika nidhamu,
matumizi ya lugha zenye staha, mavazi yanayoonyesha taswira chanya ya taifa letu;
hivyo endeleeni kuiunga mkono Serikali katika hatua inazozichukua” alisema Fissoo
Kwa
upande wake Msemaji wa Chama hicho Bw. Masoud Kaftany alisema lengo la kukutana
na Bodi ya Filamu Tanzania ni kuwatambulisha viongozi na kamati ya matukio,
maadili na mikataba kutoka kwenye chama cha Waigizaji Kinondoni kwa uongozi wa Bodi
ya Filamu kama njia mojawapo ya kuendeleza ushirikiano katika tasnia hiyo.
“Kamati
yetu inaundwa na wawakilishi 13 wakiongozwa na Mwenyekiti bwana Ahmad Hussein,
Katibu bwana Khalifan Ahmed na Msemaji bwana Masoud Kaftany na leo tumekuja Bodi
ya Filamu kujitambulisha na kujifunza Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotakiwa kufuatwa
ili zitusaidie katika utendaji wa kila siku wa kazi zetu” alisema Kaftany
Kwa
upande wake Mjumbe wa Kamati ya Chama hicho Bi. Vanitha Omari ameiomba Bodi ya
Filamu kutochoka kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu ili
waweze kupata uelewa stahiki katika tasnia kwa ujumla.
Chama
cha waigizaji wa filamu Mkoa wa Kinondoni ni miongoni mwa vyama vinavyounda
vyama vya waigizaji wa filamu taifa na ni chama ambacho kimekuwa mfano katika kutetea
maslahi na haki za wanachama wake.
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Kamati ya
Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania
Drama Film Actors Association-Kinondoni) wakifuatilia taarifa iliyokua
ikitolewa wakati wa kikao na Bodi ya Filamu kuwatambulisha viongozi hao hivi
karibuni katika Ofisi za Bodi ya Filamu Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Kamati ya
Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania
Drama Film Actors Association-Kinondoni) wakifuatilia taarifa iliyokua
ikitolewa wakati wa kikao na Bodi ya Filamu kuwatambulisha viongozi hao hivi
karibuni katika Ofisi za Bodi ya Filamu Jijini Dar es Salaam



No comments :
Post a Comment