Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo mipya ya kuchambua pamba
inayofungwa katika kiwanda cha Manonga wilayani Igunga akiwa katika
ziara ya kikazi mkoa wa Tabora Agosti 16, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
Tabora, Aggrey Mwanri.
NA
OWM, IGUNGA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi
wa vyama ushirika wawatumikie wanachama wao ipasavyo na wasidhani hiyo ni
sehemu ya ‘kupiga dili’.
Amesema Serikali itawachukulia hatua kali
viongozi wote wa vyama vya ushirika watakaobainika kuhujumu wanaushirika, hivyo
amewataka wafanye kazi kwa uaminifu.
Aliyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Agosti 16,
2018) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye kijiji cha Chomachankola.
Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa
chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Tabora cha Igembensabo cha kuhakikisha
wanasaidia wakulima katika kujiunga na huduma ya bima ya afya.
Alisema tayari Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NIHF) umeanzisha huduma kwa ajili ya wanachama wa vyama vya ushirika ambao
wanatakiwa kuchangia sh. 75,000 kwa mwaka.
Waziri Mkuu alisema wanachama hao wakijiunga na
NIHF watapata fursa ya kutibiwa bure wao, wenza wao na watoto wanne kwenye
hospitali mbalimbali nchini ikiwemo ya Muhimbili.
Pia aliwahamasisha wananchi wa wilaya hiyo
wajiunge na Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ili waweze kuwa na uhakika wa kupata
matibabu wao pamoja na familia zao kwenye hospitali zilizoko ndani ya mkoa
Tabora bure.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wakulima wa zao la pamba
wajiandae kwa kupanua mashamba yao katika msimu ujao wa kilimo kutokana na
uwepo ya masoko ya uhakika.
Waziri Mkuu alisema kwa sasa kuna viwanda vingi
vya kuchambua pamba ambavyo vimeanza uzalishaji na baadhi ya wamiliki wake
wamelalamikia upungufu wa malighafi.
Pia Waziri Mkuu aliwataka vijana waache tabia ya
kukaa vijiweni na kucheza ‘pool’ badala yake wajishughulishe na kilimo cha zao
la pamba ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo inaposimikwa mitambo mipya ya
kuchambua pamba katika kiwanda cha Manonga wilayani Igunga wakati
alipokitembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa
Tabora, Agosti 16, 2018. Kiwanda hicho ambacho kilisimamisha uzalishaji
miaka 25 iliyopita kimefufuliwa na wamiliki wake , Chama Kikuu cha
Ushirika cha mkoa wa Tabora, Igembensabo na Kampuni ya M/S Rajani Metals
and Machinery kutokana na hamasa kubwa ya uchumi wa viwanda inayofanywa
na serikali.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga wilayani Igunga wakichapa
kazi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokitembelea kiwanda hicho
akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora, Agosti 16, 2018. Kwanda
hicho ambacho kilisimamisha uzalishaji miaka 25 iliyopita kimefufuliwa
na wamiliki wake , Chama Kikuu cha Ushirika cha mkoa wa Tabora,
Igembensabo na Kampuni ya M/S Rajani Metals and Machinery kutokana na
hamasa kubwa ya uchumi wa viwanda inayofanywa na Serikali.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga wilayani Igunga wakichapa
kazi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokitembelea kiwanda hicho
akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora, Agosti 16, 2018. Kwanda
hicho ambacho kilisimamisha uzalishaji miaka 25 iliyopita kimefufuliwa
na wamiliki wake , Chama Kikuu cha Ushirika cha mkoa wa Tabora,
Igembensabo na Kampuni ya M/S Rajani Metals and Machinery kutokana na
hamasa kubwa ya uchumi wa viwanda inayofanywa na Serikali.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha
Chomachankola wilayani Igunga akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa
Tabora, Agosti 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments :
Post a Comment