Meneja wa Wakala
wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana, akifafanua jambo
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa pili
kulia), na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka (kulia), kuhusu
hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kitengo cha mizani iliyopo eneo la
Makambako mkoani humo.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa pili kushoto)
akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe
Mhandisi Yusuph Mazana (wa tatu kushoto), wakati akikagua nguzo ya daraja la
mto Halali katika barabara ya Nyigo-Igawa yenye urefu wa KM 64.6 wilaya ya
Wanging'ombe, mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher
Ole-Sendeka, akisikiliza.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa kwanza) na Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka, wakitoka kukagua kingo za daraja la
mto Halali lililopo katika barabara ya Nyigo-Igawa yenye urefu wa KM 64.6
wilaya ya Wanging'ombe, mkoani humo.
Kaimu Mhandisi
Mkazi kutoka kampuni ya LEA JV South Asia, Manish Kumar (kushoto), akimuonesha ramani
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), wakati akikagua ujenzi wa barabara ya
Nyigo-Igawa yenye urefu wa KM 64.6 kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe. Wa pili
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka akifuatilia.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akisalimiana na mkazi
wa kijiji cha Ilembula wilaya ya Wanging'ombe Bi. Hadija Samuli, wakati
alipokuwa akikagua barabara ya Nyigo-Igawa yenye urefu wa KM 64.6 inayojengwa
kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe.
Muonekano wa
sehemu ya barabara ya Nyigo-Igawa KM 64.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami,
mkoani Njombe. Mradi wa ujenzi huo utakamilika mwezi Disemba mwaka huu na
utagharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 103.(PICHA NA WUUM)
No comments :
Post a Comment