Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani
Monduli katika mkutano wa hadhara wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoani Arusha yenye
lengo la kutatua changamoto za uhalifu.
Na
Jeshi la Polisi
MKUU
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ametoa onyo kali kwa majambazi na
wahalifu wengine hususani wanaotumia silaha za moto kuacha mara moja kabla ya
kukutana na moto mkali wa Jeshi la Polisi ambapo pia ametoa wito kwa wazazi
kuwakanya watoto wao kujihusisha na vitendo hivyo.
IGP
Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na Wakazi wa Mto wa Mbu Tarafa ya
Manyara Wilayani Monduli Mkoani Arusha wakati wa Ziara yake mkoani humo yenye
lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema
hivi sasa ujambazi wa kutumia silaha umepungua kwa kiasi kikubwa na baadhi ya
matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza yanaendelea kudhibitiwa na Jeshi la
Polisi.
“Nawasihi
wanaofikiria kuendelea kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo vya utumiaji wa
silaha na kuua watu waache mara moja kwa kuwa wakikutana na moto wa Jeshi la
Polisi wasije wakajilaumu mana kwa sasa moto wetu ni mkali hivyo nawashauri
wazazi wakanye watoto wao” Alisema Sirro.
Aidha
amewataka Wakazi wa Mto wa mbu Wilayani Monduli kuendelea na shughuli zao kama
kawaida kwa kuwa usalama umeimarishwa katika kupambana na wahalifu waliokuwa
wakifanya vitendo vya kuwaua watu hususani wanawake ambapo katika kipindi cha
hivi karibuni kuliripotiwa matukio kadhaa ambayo yalileta wasiwasi katika eneo
hilo muhimu kwa utalii.
Amewataka
Viongozi wa Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa suala zima la ulinzi na usalama
linatiliwa mkazo ili kuhakikisha hakuna mhalifu katika maeneo yao na wageni
wanapoingia wachukue taarifa zao mapema.
Kwa
Upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Bi. Kuluthum Hassan alisema
Wahalifu wanaouza bangi, pombe ya gongo na dawa za kulevya wanaendelea
kuwafichua ili wafikishwe katika vyombo vya dola na hivi sasa wanaendelea na mipango
ya ujenzi wa kituo kikubwa cha Polisi kitakachoendana na hadhi ya eneo hilo.
Nao
wananchi mbalilmbali wa Mto wa mbu wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa
kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama wakati wote hususani kipindi hiki
cha watalii wengi katika maeneo hayo na wameahidi kuchangia ujenzi wa kituo cha
Polisi ili kuboresha usalama katika eneo hilo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Wakazi wa Kata ya Mto
wa Mbu Wilayani Monduli wakati alipokwenda kuzungumza nao wakati wa Ziara
yakeya kikazi Mkoa wa Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamis Issah na RPC Arusha Kamishna
Msaidizi Mwandamizi Ramadhan Nganzi wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoa wa
Kilimanjaro na Arusha.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro pamoja na Afisa Mtendaji wa Kata ya
Mto wa Mbu Wilayani Monduli Bi Kuluthum Hassan wakikagua eneo la Polisi linalotarajiwa
kujengwa kituo cha Polisi wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha yenye
lengo la kutatua changamoto za uhalifu. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha SACP Ramadhan Nga’nzi
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya
Karatu Bi. Theresia Mhongo wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha yenye
lengo la kutatua changamoto za uhalifu
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa waliopo Shule
ya Polisi Moshi zamani CCP wakati wa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa
mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua gwaride baada ya kuwasili
Shule ya Polisi Moshi zamani CCP kwa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa
mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho.(PICHA NA JESHI LA POLISI).
No comments :
Post a Comment