Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanaounda Utatu wa Asasi ya
Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama uliofanyika mjini Windhoek,
Namibia tarehe 16 Agosti 2018.
Kutoka
kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda wakifuatilia
mkutano.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano
huu pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC
utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018.
Mkutano huu umehusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wanaounda Utatu huo ambao ni Mheshimiwa João Manuel
Gonçalves Lourenço, Rais wa Angola na Mwenyekiti wa sasa wa SADC
organ; Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu, Rais wa Jamhuri ya Zambia na
Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye
ni Mwenyekiti wa SADC Organ aliyemaliza muda wake.
Mkutano
huu umejadili taarifa ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda
kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita wa Agosti 2017 hadi Agosti 2018.
Agenda
nyingine zilizojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na; taarifa ya
utekelezaji wa maazimio ya SADC kuhusu kuimarisha hali ya siasa, ulinzi
na usalama katika falme ya lesotho, hali ya siasa na usalama katika
jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),hali ya siasa na usalama nchini
Madagasca,hali ya kidemokrasia katika kanda na taarifa ya uchaguzi mkuu
kwa nchi wanachama ambao ni Madagasca, DRC na Eswatini.
vilevile
mkutano huu umejadili kuhusiana na ujenzi wa sanamu ya Mwalimu Julius
Nyerere iliyopendekezwa kujengwa katika jengo la Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia pamoja na majukumu
ambayo serikali ya Tanzania imepewa katika kusimamia zoezi hilo
linakamailika kwa wakati. |
No comments :
Post a Comment