Saturday, August 18, 2018

SERIKALI KUHAMIA DODOMA: KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU (BUNGE) MAIMUNA TARISHI APOKEA VIFAA VYA OFISINI

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi. Maimuna Tarishi (katikati), akizungumza wakati wa hafla fupi ya ya kupokea vifaa vya Ofisi hiyo vilivyowasili Jijini Dodoma kutoka Dar es Salaam mapema leo Ijumaa Agosti 17, 2018

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi. Maimuna Tarishi (kushoto) akieleza jambo na mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma leo Agosti 17, 2018 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya Ofisi hiyo vilivyowasili kutoka Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nigel Msangi akionesha sehemu ya vifaa vya Ofisi hiyo vilivyowasili Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha zoezi la Ofisi hiyo  kuhamia Dodoma.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi.  Maimuna Tarishi akikagua sehemu ya vifaa vya Ofisi hiyo  vilivyowasili kutoka Jijini Dar es Salaam leo Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi la Serikali kuhamia Dodoma.

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi.  Maimuna Tarishi akikagua sehemu ya vifaa vya Ofisi hiyo  vilivyowasili kutoka Jijini Dar es Salaam leo Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi la Serikali kuhamia Dodoma.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Agustino Tendwa akisisitiza jambo kwa  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi.  Maimuna Tarishi wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya Ofisi hiyo kutoka Jijini Dar es Salaam leo Jijini Dodoma.

Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack  Bandwe akieleza  hatua zilizofikiwa katika kuhakikisha kuwa watumishi wote wa Serikali wanahamia Dodoma wakiwemo wa Taasisi za Serikali na Mihimili yote.
   Sehemu ya vifaa vya Ofisi ya Waziri Mkuu vikishushwa katika moja ya magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali kuhamia Dodoma.

  Sehemu ya vifaa vya Ofisi ya Waziri Mkuu kama vinavyoonekana katika picha mara baada yakufikishwa Jijini Dodoma na gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vikitokea Jijini Dar es Salaam.



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi.  Maimuna Tarishi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ofisi hiyo na kikosi kazi cha kitaifa cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kupokea sehemu ya vifaa vya Ofisi ya Waziri mkuu iliyofanyika katika Ofisi hizo.(PICHA ZOTE NA FRANK MVUNGI- MAELEZO)

No comments :

Post a Comment