Saturday, August 18, 2018

MWITA WAITARA ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA UKONGA KUPITIA CCM


  Mgombea ubunge Jimbo la Ukonga kwa yiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwita Waitara leo Agosti 17, 2018 amechukua fomu za kuwania kiti hicho kutoka kwa Msmsimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bw. Jumanne Shauri. Waitara amefuanhgua pazia  kwa wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani kufanya nhivyo. Pichani Waitara ambaye awali alikuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia chama kikuu cha upinzani CHADEMA, alikihama chaam hicho na hivyo kujivua ubunge kwa maelezo kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kuchoshwa na siasa mbovu za upinzani na ameona ni busara kuhamia CCM ili aweze kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika kujenga uchumi wan chi. Pichani Waitara (kushoto) akichukua fomu kutoka kwa Msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo, Jumanne Shauri, Dar es Salaam



No comments :

Post a Comment