Mashirika ya Habari
KATIBU
Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN) na
mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Kofi Annan (pichani)amefariki dunia leo Agosti 18,
2018 akiwa na umri wa miaka (80), wakfu wake umethibitisha.
Annan
ambaye amezaliwa nchini Ghana mwaka 1938 amehudumu kama Katibu Mkuu wa 7 wa
Umoja wa Mataifa (UN) kutoka mwaka 1997 hadi mwaka 2006 na alikuwa ni mmoja wa
zao la watumishi wa UN kufikia nafasi hiyo.
Alikuwa
mmoja wa wanakundi la Wazee wa Dunia (Kundi la Viongozi wa Dunia), lililojikita katika masuala ya
kutetea haki za binadamu tangu lilipoanzishwa mnamo mwaka 2007, na mwaka 2013
Annan alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa kundi hilo.
Wakfu
wa marehemu Kofi Anna, umethibitisha kutokea kwa kifo chake kwa masikitiko
makubwa kupitia ukurasa wake wa tweter.


No comments :
Post a Comment