Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la
Bima la Taifa la Tanzania (NIC), Sam Kamanga akizungumza jambo kuhusiana
na bima ya majanga ,wilayani Kisarawe,Pwani
Picha na Mwamvua Mwinyi
………………
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SHIRIKA la bima la Taifa la Tanzania (NIC)
,limelenga kuanzisha bima ya kilimo mwaka huu ,ambayo itasaidia kuwapa
usingizi wakulima mbalimbali nchini, waweze kunufaika kwa kujikinga na
majanga .
Mkurugenzi mtendaji
wa NIC ,Sam Kamanga, aliweka bayana juu ya mpango huo ,wakati akitolea
ufafanuzi masuala ya bima za majanga, wilayani Kisarawe mkoani Pwani .
Alieleza ,wamelenga kuanzisha program hiyo wakati wa siku ya wakulima ,nanenane na sabasaba mwaka 2018.
“Katika program zetu
tunaianzisha program hii ya bima ya kilimo ,kusudi kumpa mkulima nafuu
,kwani ni asilimia 75 ya watanzania wananufaika na kilimo”
“Kukitokea majanga
wakulima hao huwa wakipoteza muelekeo ,tunataka kumpa usingizi mlaji
,hata akitokewa na janga shambani ama gari lake limeangukiwa na mti awe
anajua atakingwa na kulindwa na bima yake” alifafanua Kamanga.
Akielezea baadhi ya
gharama za kukata bima , Kamanga alisema nyumba ya yenye thamani ya
Tsh.mil 30 bima yake kwa mwaka haizidi 150,000 .#
” Bima zetu
zinaendana na uwiano na kutokana na gharama na thamani, mfano gari
uliyonunua kwa gharama ya Tsh.milioni 400 unakatiwa bima ya mil.13 “
“Ni gharama kidogo na
nafuu sana ,nikikupa hapa dada yangu 150,000 ambayo ni bima ya nyumba
ukienda salun unaweza kusema 150,000 haitoshi ,maana wengine mnanunua
wigi la milioni moja ,sasa kwanini usijikatie bima ya nyumba, kilimo ama
gari yako ??!alihoji Kamanga.
Aidha Kamanga
alieleza ,bado uelewa kwa wananchi haujawa mkubwa ,kwani wengi wao
wanajua bima hizo zinawahusu watu walio matajiri pekee.
Kwa mujibu wake , hakuna elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa bima ya majanga kama ilivyo bima ya afya.
Aliwataka wananchi ,kubadilika na kujiwekea utamaduni wa kujilinda na mali zao kabla ya hatari.
“Tatizo utamaduni
tuliojiwekea tunataka kusaidiana likitokea janga la moto, msiba ,wakati
inatakiwa kujiwekea mwenyewe pia kabla ya janga ama shida ,:;”Kizazi
kinachokuja inabidi tubadilike na utamaduni huu kama ilivyo kwa wenzetu
katika baadhi ya nchi” alisema.
Hata hivyo ,Kamanga alisema ,wamejiwekea kuwa karibu na wananchi kwenye changamoto zao za kijamii ikiwemo afya na elimu.
Alisema wameanza
kutekeleza katika mikoa ya Iringa, Mwanza, Sumbawanga na wilaya ya
Kisarawe -Pwani ikiwa ni miongozo ya utawala bora kwa kushiriki kutatua
changamoto ndani ya jamii.
No comments :
Post a Comment