Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wadau wa sanaa na
filamu (hawapo katika picha) wakati wa uzinduzi wa Multichoice Talent
Factory iliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice Afrika jana Jijini
Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji Multichoice
Afrika – Mashariki na Magharibi, Bw. Maharage Chande akieleza jambo
kuhusu mradi uliozinduliwa jana Jijini Dodoma na Kampuni ya Multichoice
Afrika ujulinano kama Multichoice Talent Factory wenye lengo la
kuwaendeleza kitaaluma vijana waliko katika tasnia ya filamu na sanaa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe(wa kwanza kulia), akiwa na Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson
Mwansasu (Katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Multichoice Africa –
Mashariki na Magharibi, Bw. Maharage Chande (kushoto) wakiangalia video
wakati wa ufunguzi wa Multichoice Talent Factory jana Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe( wa nne kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi wa Serikali pamoja na viongozi wa
Multichoice Tanzania, mara baada ya kuzindua mradi wa Multichoice Talent
Factory jana Jijini Dodoma.
Picha na Frank Mvungi-MAELEZO,Dodoma
……………..
Na Lorietha Laurence-WHUSM, Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa rai kwa Kampuni ya
Multichoice nchini kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia pamoja na vyuo vinavyotoa elimu ya sanaa ya filamu ili
kuhakikisha wanabadilishana ujuzi na
kuwa na miradi ya pamoja.
Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo jana
Jijini Dodoma wakati akizindua mradi wa kampuni hiyo utakaowapa fursa
ya kujiendeleza kitaaluma vijana wenye vipaji katika tasnia ya filamu
kwa kupata ufadhili wa mafunzo kwa muda wa mwaka mmoja katika chuo cha
sanaa Jijini Nairobi nchini Kenya.
“Napenda kuwapongeza Multichoice
kwa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanaleta maendeleo, huu
ni mwanzo mzuri wa kuboresha taaluma kwa vijana ambao asilimia kubwa
wamejiajiri katika sekta ya sanaa ikiwemo filamu” Dkt. Mwakyembe
Aidha,Dkt. Mwakyembe amewataka
vijana mabao wanakidhi vigezo kuhakikisha wanachangamkia fursa hiyo
adimu ili waweze kuongeza ujuzi na hivyo kuwa chachu ya maendeleo pale
wanaporudi nyumbani kwa kuwafundisha wengine ili elimu hiyo kuwafikia
vijana wengi zaidi.
Alizidi kufafanua kuwa ili kuwa na
maudhui mazuri yenye kuvutia, yanayokwenda na wakati huku yakizingatia
tamaduni za nchi yetu, ni lazima tuwe na wataalamu wetu wenyewe wa
kuzalisha kazi hizo za kisanii, kuanzia waigizaji, waandika hadithi,
waandaaji na wazalishaji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji
Multichoice Africa – Mashariki na Magharibi, Bw. Maharage Chande
ameeleza kuwa Multichoice Afrika imeanzisha Multichoice Talent Factory
inayolenga kuwapa vijana wenye vipaji fursa maalum ya kupata mafunzo
katika sekta ya filamu.
“Kwa kuanzia tutakua na vituo
vitatu vya mafunzo kimoja Afrika Magharibi, kingine Afrika Masharika na
Afrika Kusini, ambapo vinatarajiwa kuanza rasmi mnamo mwezi Oktoba
mwaka huu huku mchakato wa kupata wanafunzi utaanza mwezi Juni mwaka
huu” Bw. Chande
Adha Bw. Chande alisisitiza kuwa,
katika kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo kwa ufanisi watashirikiana
kwa karibu na wadau wa tasnia ya filamu hapa nchini katika mchakato
mzima wa kuweza kuwapata vijana watakaofuzu kujiunga na mafunzo hayo.
No comments :
Post a Comment