Mhe.
Mhandisi Stella Manyanya Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji
akifuatilia Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara,
Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea.
Mkutano
huu ulilenga kujadili na kutolea ufumbuzi masuala mbalimbali yakiwemo
ya kiforodha, ambayo yamekuwa kikwazo katika ufanyaji wa biashara za
kuvuka mipaka katika Jumuiya.
Mkutano huu uliofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018 na kuhudhuriwa na nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifikia tamati tarehe 30 Mei, 2018 jijini Arusha.
 |
Prof.
Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Kisekta la
Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliofanyika jijini
Arusha.
 |
| Kutoka
kushoto ni Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Prof.
Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa
Biashara, Viwanda na Uwekezaji, na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa
Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji wakifuatilia mkutano |
|
|
No comments :
Post a Comment