
Dar es Salaam, Novemba 24, 2017:
Serikali inautaarifu umma kuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
ataungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za
kuapishwa Mhe. Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa kipindi
cha awamu ya pili.
Mhe. Kenyatta ataapishwa siku ya
Jumanne, Novemba 28, 2017, jijini Nairobi, baada ya ushindi alioupata
katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo.
Imetolewa na:
Dkt. Hassan Abbasi
No comments :
Post a Comment