Kaimu mkurugenzi wa shirika la wanawake katika Sheria na
Maendeleo Afrika (WiLDAF),Anna Kulaya,akiongea wakati wa mkutano na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kampeni hizo
Afisa Mawasiliano kutoka TBL,Amanda Walter akiongea wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kihusu kampeni hizo
Baadhi
ya wadau wa Masuala ya kupambana na vitendo dhidi ya ukatili katika
picha wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya wadau wa masuala ya kupambana na vitendo dhidi ya ukatili wa
kijinsia katika picha ya pamoja baada ya kufanya mkutano wa waandishi wa
habari
……………………………………………………………………….
Kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia inayoshirikisha wadau mbalimbali wanaopinga vitendo hivyo inazinduliwa nchini
kesho jijini Dar es Salaam ambapo Makamu wa Rais,Mh.Samia Suluhu
Hassan, anatarajia kupokea maandamano ya wadau hao ambayo yataanzia
katika viwanja vya shule ya msingi ya Muhimbili na kuishia katika
viwanja vya leaders.
Kampeni
hizo ambazo hufanyika duniani kote kwa hapa nchini zinaratibiwa na
Shirika lisilo la kiserikali la wanawake katika sheria na Maendeleo
Afrika (WiLDAF) kwa kushirikiana na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa
Kijinsia (MKUKI) ,Wadau wa Maendeleo na Asasi za Kiraia
Mwaka
huu kampuni ya Tanzania Breweries Limited,TBL chini ya kampuni mama ya
ABINBEV imejitosa katika kampeni hizo ambazo itasambaza jumbe mbalimbali
za kuelimisha jamii kupitia kampeni yake ya #NO EXCUSE!!! ACHA SABABU,
BADILIKA inayoenda sambamba na kampeni yake ya kuelimisha jamii juu ya
Unywaji wa kistaarabu.
No comments :
Post a Comment