Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
(kulia) akiwa na Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kushoto),
katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
(kushoto) akipokea zawadi ya Ngao kutoka kwa Balozi wa Kuwait hapa
nchini Jasem Al-Najem (kulia), katika ofisi za Wizara ya Madini jijini
Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem
Al-Najem (kulia) akimweleza Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto)
kuhusu alama mbalimbali zilizo katika Ngao kutoka nchini Kuwait, mara
alipomtembelea katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.
…………..
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Jasem
Al Najem tarehe 24 Novemba, 2017.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi
za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumza masula
mbalimbali kuhusu uendelezaji wa Sekta ya Madini nchini.
Waziri Kairuki amesema kuwa
mazungumzo yake na Balozi wa Kuwait yamelenga katika suala la uwekezaji
kwenye Sekta ya Madini ambapo ameikaribisha nchi hiyo kuja kuwekeza
nchini ili kuendeleza Sekta husika.
Aidha, ameongeza kuwa, katika kikao
hicho wamezungumzia suala la kuwajengea uwezo Wataalam wa Madini nchini
ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Vilevile wamejadiliana suala la
kubadilisha uzoefu kati ya Kuwait na Tanzania lengo likiwa ni
kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inachangia ipasavyo katika uchumi wa
nchi husika.
No comments :
Post a Comment