Kamanda wa Polisi
Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna akitoa taarifa kwa waandishi wa habari
kuhusu kukamatwa kwa watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha
wahamiaji haramu 21 .(picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
JESHI la polisi
mkoani Pwani ,linawashikilia wahamiaji haramu 21 ,raia wa Ethiopia kwa
kosa la kuingia nchini bila kibali ikiwa ni kinyume na sheria .
Aidha limewakamata
watanzania wawili waliokuwa wakiwasaidia kuingia nchini wahamiaji hao
ambapo pia inausaka mtandao unaojihusisha na biashara hiyo.
Akielezea kuhusiana
tukio hilo ,kamanda wa polisi Mkoani Pwani ,(ACP) Jonathan Shanna
alisema ,octoba 20 usiku , eneo la Ruvu darajani wilaya ya kipolisi
Mlandizi askari wakiwa doria waliwakamata Yabata Shaban (30) mkazi wa
Bagamoyo na Mohammed Ayub (20) mkazi wa Bunju wakiwasafirisha wahamiaji
hao.
Alisema watuhumiwa walikuwa wakiwasafirisha raia hao kwa... kutumia usafiri wa gari aina ya Noah yenye namba za usajili T.209 DEW .
“Walikuwa wakitokea Ethiopia kwenda Afrika ya Kusini ,” Waliingia nchini kwa usafiri wa majahazi wilayani Bagamoyo .
Kamanda Shanna
alielezea ,Bagamoyo ndio lango kuu lina bandari bubu kama 17 ,ambazo
baadhi ya watanzania wanazitumia vibaya kupitisha magendo na kufanya
biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu .
Alibainisha kwamba ,watataifisha mali zote za watu wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.
Kamanda Shanna aliwatahadhalisha ,wale wanaotoa vyombo vyao vya
majini na nchi kavu kusafirisha wahamiaji wanaoingia nchini pasipo
kufuata sheria za nchi kwani navyo vitataifishwa .
Alisema Jeshi la
polisi mkoani humo, linaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote ili
kubaini mtandao wao na wale wanaowasaidia kuingia nchini .
Kamanda huyo
,alisema kuwa wahamiaji hao watafikishwa idara ya uhamiaji kwa hatua
nyingine za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani .
Ni siku chache
zimepita waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba alipotembelea magereza
ya Kigongoni -Bagamoyo,mkoani hapo na kukutana na wimbi la wahamiaji
haramu gerezani ambao wengi wao wanasubiria kumaliza kifungo chao na
kupelekwa makwao kwa gharama za serikali .
Kutokana na hilo
alisema hakuna sababu ya serikali kuendelea kutumia mamilioni ya fedha
za walipa kodi kuwahudumia wahamiaji haramu wanaoingia kiholela bila
kufuata taratibu .
Nchemba alieleza, badala yake wajihudumie ama wahudumiwe na nchi zao ili kuliondolea mzigo Taifa.
No comments :
Post a Comment