Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu
wa familia iliyopata msiba huo katika kijiji cha Fumba Wilaya ya
Magharibi “B” Unguja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Dk. Abdalla Juma Mabodi Akisalimiana na baadhi ya wananchi na viongozi
mbali mbali walioudhuria katika msiba huo.
………………………………………………………………………….
Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM)Z
anzibar kimetoa mkono wa pole kwa familia iliyopata ajali ya kuungua
moto nyumba na kusababisha vifo vya watu wanne huko katika kijiji cha
Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi wakati wa kuifariji familia hiyo
amesema CCM Zanzibar imesikitishwa sana na tukio hilo kwani limegharimu
maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia.
Dk. Mabodi alisema kwa niaba ya
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatoa pole kwa
ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo na kuwasihi waendelee kuwa na...
moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha msiba huo.
“ Kupoteza watu Wanne katika
familia moja ni jambo zito linalotia huzuni lakini tuendelee kuwa
wavumilivu kwani Allah amewapenda zaidi na sisi tuliobaki tuendelee
kuwaombea dua ili wapate makaazi mema na kusamehewa madhambi yao”,
alitoa nasaha hizo kwa maskitiko makubwa Dk. Mabodi.”
Mapema Sheha wa Shehia ya Fumba,
Mohamed Suleiman alifafanua kuwa nyumba hiyo ilianza kuwaka moto majira
ya saa 6:15 usiku Oktoba 21 mwaka huu, ambapo wananchi mbali mbali
walianza juhudi za kuzima moto huo na kushindwa kuokoa watu waliokuwa
ndani kwani uliku ni mkubwa.
Suleiman alisema wakati juhudi za
kuzima moto huo zikiendelea waliwasiliana na Kikosi cha Zimamoto na
Uokozi Zanzibar ambacho kilifika na kusaidiana na wananchi hao ambapo
walizima moto huo na kukuta watu wanne tayari wamefariki dunia.
Akidhibitisha tukio tukio
hiloalisema chanzo cha moto huo ni hitilafu za umeme zilizoanzia katika
waya wa jokofu (Friji) lililokuwa likifanya kazi wakati wa usiku.
Kamanda Nassir aliwataja watu
waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Bahati Ali Ameir (40), Sinawema
Abdalla Ali, Hashim Abdalla Ali (6) na Latifa Mohamed Ali (8).
Alitoa wito kwa wananchi kujenga
utamaduni wa kuzima vifaa vya umeme wakati wa usiku ambavyo havina
umuhimu wa kutumiwa wakati huo ili kuepuka majanga yanayoweza
kuhatarisha maisha ya watu.
No comments :
Post a Comment