Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia bonde la mtop
Msimbazi katika kata ya Vingunguti lilivyoharibika kwa shughuli za kila
siku za Wananchi ikiwemo kilimo cha mbogamboga na uchimbaji wa mchanga.
Waziri Mkamba yupo katika ziara kutembelea kata ya Vingunguti kukagua
athari za mazingira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mbunge wa
jimbo la Segerea Mh. Bonnah Klauwa wakiskiliza kero mbalimbali
zinazotolewa ana Wananchi wakati Mh. Waziri alipofanya ziara katika kata
ya Vingunguti kukagua athari mbalimbali za mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Wananchi
waliojikusanya kumsikiliza wakati wa ziara yake katika kata ya
Vingunguti katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipata maelezo, toka
kwa vijana wa kata ya Vingunguti juu ya utenegenezaji wa majiko ya mkaa
ambayo ni rafiki wa mazingira na ambayo hayatumii mkaa mwingi.
…………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka wachimbaji
mchanga na walimaji wa bustani katika bonde la mto msimbazi katika kata
vingunguti iliyopo katika Manispaa ya Ilala, kuondoka mara moja na
kuacha shughuli hizo. Ameyasema hayo alipokua katika ziara ya siku moja
ya kutembelea kata ya Vingunguti na kujionea athari mbalimbali za
kimazingira katika kata hiyo.
Wakiongea mbele ya Waziri
Makamba, Wananchi wamelalamika kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo
bonde hilo kuzidi kumong’onyoka na kusogelea makazi ya watu pamoja na
eneo la makaburi. Hivyo basi kusababisha nyumba zao kuanguka na makaburi
kumong’onyoka hali amabayo inahatrisha maisha yao na kuwafanya kuishi
kwa hofu.
Akijibu kero hiyo Waziri Makamba
aliwaambia kuwa atayafanyia kazi maombi yao na atakaa na viongozi wa
Manispaa na wa Ofisi yake ili kupata suluhu ya matatizo yao. Pamoja na
hayo alisema kuwa kwa hatua za awali anawataka wachimbaji na wakulima
wa bustani kuacha mara moja shughuli hizo wanazofanya katika maeneno ya
bonde hilo.
(habari na picha toka Kitengo caha mawasiliano Serikalini OMR)
No comments :
Post a Comment