Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia mbele)
akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kalemie, Kongo kwa ajili ya
kushiriki mkutano wa kubadilishana data na uzoefu kuhusu mafuta katika
Tanganyika uliofanyika hivi karibuni nchini Kongo. Nchi nyingine
zilizoshiriki ni pamoja na Burundi, Kongo na Zambia. Wengine kutoka
kushoto ni Gavana wa Jimbo la Tanganyika – Kongo, Richard Ngoy
Kitangala, Waziri wa Migodi na Madini Nchini Zambia, Chris Yaluma na
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime
Ngoi-Mukena Lusa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (kushoto) na Gavana wa Jimbo la Tanganyika – Kongo, Richard
Ngoy Kitangala (kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime
Ngoi-Mukena Lusa (hayupo pichani) katika mkutano huo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria,
Wizara ya Nishati na Madini, Anna Ngowi (kushoto) pamoja na wataalam
wengine kutoka Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zinawasilishwa katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (katikati) akiweka mchanga kwenye jiwe la msingi kuashiria
uzinduzi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi katika mji wa
Kalemie. Kulia kwake ni Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia
ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo ( wa pili kutoka kushoto, mbele) pamoja na viongozi wengine
wakishikana mikono kama ishara ya umoja mara baada ya kuzindua ujenzi
wa Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi katika mji wa Kalemie hivi karibuni .
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo ( wa tatu kutoka kushoto mbele) na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri
ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa ( wa sita kutoka
kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wengine mara
baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi katika
mji wa Kalemie hivi karibuni .
Mtaalam kutoka Idara ya Nishati,
Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Athur Lyatuu (kushoto)
akibadilishana mawazo na mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.
No comments :
Post a Comment