Hapa
ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako leo Ijumaa Februari
03,2017 kumefanyika Kongamano la wafanyabiashara kutoka wilaya ya
Shinyanga lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na
Kilimo(TCCIA) kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro.
Kongamano
hilo lililokutanisha wafanyabishara kutoka Shinyanga Mjini na Vijijini
na nje ya mkoa wa Shinyanga lililenga la kuibua na kujadili fursa za
uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga na kujadili changamoto
zinazowakabili wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
Mwandishi wetu Kadama Malunde, ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kongamano hilo lililoanza majira ya saa 11:25 jioni na kumalizika saa 4:06 usiku…Tazama hapa chini
Kushoto
ni mgeni rasmi katika kongamano la wafanyabiashara ,Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara
Wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga,(TCCIA) Mchungaji Dr. Kulwa
Ezekiel Meshack wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga leo Ijumaa
Februari 3 2017
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Sekretariati wakiwa ukumbini
Afisa
Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira aliyemwakilisha katibu
tawala wa wilaya hiyo akitambulisha viongozi wa serikali waliohudhuria
kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara
Mkurugenzi
wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia
wafanyabiashara,kulia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes
Machiya
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga
Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack akizungumza wa kufungua kongamano
hilo ambapo alisema wameamua kukutana ili kujadili fursa mbalimbali za
uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga
Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack alitumia fursa hiyo kumpongeza rais
John Pombe Magufuli kwa kuhimiza uchumi wa viwanda na kuahidi kuwa
wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga wapo tayari kumuunga mkono
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga
Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack pia aliiomba serikali kupunguza
rundo la kodi kwawafanyabiashara kwani kodi hioz zinawakatisha tamaa
kuendelea kufanya biashara
Meneja wa Benki ya Maendeleo -TIB Kanda ya ziwa Zacharia Kicharo akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Meneja Miradi kutoka Tanzania Local Enterprise Development (TLED) Stanley Magese akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Mwalimu
wa walipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa
Shinyanga Anthony Faustine akitoa mada kuhusu ulipaji kodi
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwahutubia wafanyabiashara
wilaya ya Shinyanga waliohudhuria kongamano hilo ambapo aliwaasa
kujitokeza kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda kwani
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli
inataka watanzania kuwekeza katika viwanda
Mkuu
huyo wa wilaya Josephine Matiro alisema serikali ya wilaya ya Shinyanga
ipo tayari kushirikiana na wafanyabishara katika kukuza uchumi wa mkoa
wa Shinyanga
Matiro aliwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwaomba kuendelea kuwekeza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kushoto) akiteta jambo na
mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel
Meshack na katibu wa Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo
Mc Mama Sabuni anayeongoza Kongamano hilo akiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Wafanyabisahara wakiwa ukumbini.Kulia ni mkurugenzi wa Vigimark Hotel bi Victoria Majige
Tunafuatilia kinachoendelea
Kulia
ni Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo,kushoto ni Afisa
tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira wakifuatilia kinachoendelea
ukumbini
Meneja
wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui akitoa mada wakati wa
kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wafanyabiashara kujenga mazingira ya
kukopesheka,kuwa waaminifu na kulipa madeni yao kwa wakati kama
wanavyokubaliana na benki
Pamui
alitumia fursa hiyo kuwapongeza wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga
kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwataka kujenga utamaduni
wa kujitokeza katika vikao na mikutano mbalimbali ili kubadilishana
uzoefu na kupeana mbinu mpya za kufanya biashara.
Wafanyabiashara wakifuatilia yanaliyokuwa yanajiri ukumbini
Mkurugenzi
wa Vigimark Hotel iliyopo mjini Shinyanga Victoria Majige akizungumzia
changamoto ya ubovu wa barabara inayoelekea katika hoteli hiyo ambapo
aliiomba serikali kutengeneza barabara hiyo walau kwa kiwango cha
moramu
Mfanyabshara wa Uyoga wilayani Shinyanga Hamisa Nuhu akichangia hoja wakati wa kongamano hilo
Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akichangia hoja ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Katibu wa Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga Gregory Kigusi akichangia hoja ukumbini
Katibu
wa TCCIA Marcelina Saulo akielezea kuhusu namna wafanyabishara
wanavyokerwa na bei kubwa ya mabango ya matangazo na kuiomba serikali
kuangalia namna ya kupunguza gharama za matangazo kwani inawakatisha
tamaa wafanyabishara na kuamua kuondoa matangazo
Afisa
Biashara wa manispaa ya Shinyanga Sunday akieleza namna serikali
inavyofanya kuhakikisha kuwa gharama za matangazo inapungua
Mkuu
wa Polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akijitambulisha kwa
wafanyabishara ambapo alisema serikali itaendelea kuwalinda
wafanyabiashara katika kuuweka mji wa Shinyanga salama
MC Mama Sabuni akifanya yake ukumbini
Kamanda
wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akizungumza wakati kufunga
kongamano hilo ambapo aliwaomba wafanyabiashara kujitokeza kutoa taarifa
za watumishi ama idara yoyote inayowaomba rushwa katika biashara zao.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment