Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akifafanua jambo wakati
wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo
(Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering
Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction
Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini mkataba wa ujenzi
wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction
Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao (Katikati) wakisaini
mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo
(Interchange).Kushoto ni Meneja Mradi wa ujenzi huo Li Haiquan.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction
Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakibadilisha hati za
mikataba mara baada ya kusaini ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo
(Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo wakati wa
hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo
(Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering
Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Baadhi ya wawakilishi wa
Mkandarasi wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction
Cooperation kutoka China (CCECC) wakifuatilia hafla ya utiaji saini ya
ujenzi wa Ubungo interchange Jijin Dar es salaam.
………………………………………………………………
Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS), leo umetiliana saini na kampuni ya M/S China Civil
Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) mkataba wa
ujenzi wa barabara za Juu ‘Interchange’ katika makutano ya barabara ya
Sam Najoma na Mandela Ubungo jijini Dar es salaam.
Mkataba huo unamtaka Mkandarasi
kampuni ya CCECC kutoka China kuanza ujenzi huo mara moja na ujenzi huo
unatarajiwa kutumia takriban miezi 30 hadi kukamilika kwake.
Akizungumza mara baada ya kusaini
mkataba huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng.
Patrick Mfugale amesema zaidi ya shilingi Bilioni 177.4 zinatarajiwa
kutumika katika ujenzi huo utakaowekewa jiwe la msingi mwezi machi mwaka
huu.
“Hakikisheni mnaanza ujenzi mara
moja kwani Serikali imeshakamilisha taratibu zote na tayari kiasi cha
shilingi bilioni 2.1 kimelipwa kwa ajili ya fidia kwa wananchi
walioguswa na mradi huo”. Amesema Eng. Mfugale.
Ujenzi wa Ubungo interchange
unajengwa kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia ambapo Serikali kwa
upande wake imeshalipa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 2.1
“Zaidi ya magari 65,000 yanapita
kila siku katika katika makutano ya barabara za morogoro,Mandela na sam
nujoma eneo la Ubungo hali inayosababisha msongamano katika barabara ya
Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia jijini Dar es salaam hivyo
ufanisi wa mradi huo utahuisha hali ya usafirishaji katika jiji la Dar
es salaam na kuchochea ukuaji wa uchumi” amesisitiza Eng. Mfugale.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CCECC Bw, Jiang Yigao amemhakikishia Eng. Mfugale
kuwa wataanza maandalizi ya ujenzi huo mara moja na watafanya kazi hiyo
kwa wakati
No comments :
Post a Comment