HUKUMU ya kesi ya Kikatiba namba 9
ya mwaka 2016 iliyofunguliwa mwaka jana na Kampuni ya Jamii Media
ikipinga baadhi ya vifungu vya sheria ya makosa ya mtandao kwa kile
kuingilia uhuru wa maoni na kujieleza wa wananchi imeshindwa kusoma huku
kukiwa hakuna sababu zilizotajwa.
Akizungumza leo eneo la Mahakama
Kuu, jijini Dar es Salaam Wakili wa Jamii Media, Benedict Ishebakaki
Alex alisema awali walipata wito wa mahakama kuwa hukumu ya kesi yao
ilikuwa isomwe leo lakini wamefika mahakamani na kutokuta taarifa zozote
za kusomwa kwa hukumu hiyo.
“..Kama mnavyojua leo tulikuwa
tumekuja kwa ajili ya hukumu ya kesi yetu iliyofunguliwa toka mwaka jana
mwezi wa tatu kutokana na rekodi za mahakama tuliambiwa tuje leo saa
sita mchana kuja kupokea hukumu kama mnavyojua majaji ambao walikuwa
wanasikiliza kesi yetu ni majaji watatu Mh. Jaji Koroso, Mh. Jaji
Khalfan na Mh. Jaji Kitusi lakini tumefuatilia leo hapa pamoja na
mawakili wa serikali, lakini tulikuwa tunajua jaji Koroso hayupo kuna
taarifa kuwa amehamishwa…lakini tulikuwa tunajua labda kuna rekodo
yoyote kuwa labda amemwachia faili nani au hukumu itasomwa lini
tena…tunaona makarani wanasema hawana taarifa zozote juu ya hukumu hiyo.
Wakili huyo alisema yeye pamoja
na mawakili wa Serikali wataendelea kufuatilia kujua hukumu hiyo itasoma
lini ili waweze kuipokea.
Kwa upande wake Mwanaharakati wa
haki ya kupata habari nchini, Simon Mkina, akizungumzia kadhia ya hukumu
hiyo kutoonekana, amesema inashangaza kuona mahakama hiyohiyo iliyotoa
tarehe ya kutolewa hukumu, watendaji wake wanatupiana mpira kuhusu
ilipo.
mdau wa masuala ya habari nje ya Mahakama kuu jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment