Kushoto ni Daktari Bingwa wa
Upasuaji wa Watoto, Profesa Zakaria Habib kutoka Falme za Kiarabu akiwa
na timu ya watalaam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimuandaa mtoto
mwenye umri wa miaka minane kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa hatua ya
pili ya kushushwa kokwa kwenye korodani .
Madaktari wakifanya upasuaji wa njia ya matundu madogo kwa mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo
Madaktari wakifanya upasuaji wa njia ya matundu madogo kwa mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo
…………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) leo imehitimisha zoezi la upasuaji mkubwa kwa njia ya matundu
madogo kwa watoto ambao ulianza jumatatu wiki hii .
Upasuaji huo umefanywa na
Madaktari Bingwa wa Muhimbili waliobebea katika upasuaji wa
watoto kwa
kushirikiana na mtaalam kutoka Hospitali ya King Faisal ya nchini Saudia
Arabia Profesa Zakaria Habib .
Akizungumzia kuhusu upasuaji huo
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Zaitun Bokhary amesema upasuaji huo umekua na mafanikio makubwa na
kwamba watoto wote waliofanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri.
‘’ Tunamshukuru Mungu hadi leo
tunapohitimisha zoezi hili watoto waliofanyiwa upasuaji huo wanaendelea
vizuri na tayari wameanza kula pamoja na mazoezi ‘ ‘ amesema Dk.
Bokhary.
Tangu kuanza kwa upasuaji huo
Februari 20 mwaka huu kwa njia ya matundu madogo ( Laparoscopy
Surgery) jumla ya watoto sita wamefanyiwa upasuaji huo.
Upasuaji huo umehusisha upasuaji
wa nyama iliyojitokeza katika sehemu ya haja kubwa kwa watoto, upasuaji
wa kushusha kokwa katika korodani, upasuaji wa kushusha utumbo mkubwa
na kutengeneza njia ya haja kubwa kwa watoto ambao wamezaliwa bila kuwa
na njia ya haja kubwa, upasuaji wa kuondoa mfuko wa ziada kwenye koo kwa
watoto na upasuaji kwa watoto wadogo ambao hawana celi mbalimbali na
hivyo kushindwa kusukuma choo kwenye utumbo mkubwa
No comments :
Post a Comment