Mkurugenzi
wa Mawasiliano kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata
Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Udhamini wa Mashindano ya
Kilimanjaro International Marathon katika Ofisi za Kampuni hiyo zilizoko
Blue Rock jijini Arusha.
………….
Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
Kampuni
ya Simu za mkononi ya TIGO imejipanga kunogesha mashindano ya
Kilimanjaro International Marathon kupitia udhamini mnono ya mashindano
hayo kwa upande wa kilomita 21 ambapo licha ya udhamini huo
watahakikisha huduma zote muhimu za kifedha zinapatikana katika
mashindano hayo.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini,George Lugata
amesema kuwa zaidi ya nchi 45 zinatarajia kushiriki katika mashindano
hayo ya kimataifa yanayotarajia kufanyika Februari 26 mwaka huu mjini
Moshi mkoa wa Kilimanjaro.
George
alisema kuwa kampuni ya Tigo imejipanga kuhakikisha kuwa huduma za Tigo
Pesa zinapatikana kwa kipindi chote kwani wameongeza idadi kubwa ya
mawakala wataotoa huduma hizo.
“Ni
vyema tukatambua kuwa wateja kutoka mitandao yote nchini wanaweza pia
kulipia huduma na bidhaa kutoka katika maduka ya wafanyabiashara wowote
jijini Moshi kwenye mabango yaliyoandikwa Lipa kwa Tigopesa” Alisema
George
Alisema
kuwa katika kipindi chote hicho watatoa huduma zenye ubora wa hali ya
juu ili kuhakikisha kuwa wa Washiriki na Watakaohudhuria wanafurahia
huduma hizo.
Mkurugenzi
huyo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kushiriki
mbio hizo zenye hadhi kubwa kitaifa na kimataifa .
No comments :
Post a Comment