Na Mahmoud Ahmad Arusha
AFISA
mstaafu wa jeshi la kikoloni,King Africa Rifles,(K.A.R) Capten mstaaf,
David Nickol (96) kutoka nchini Uingereza,ameweka shada la maua kwenye
mnara wa kumbu kumbu ya mashujaa wa vita vya Kagera, jijini
Arusha,kwenye hafla fupi iliyoshuhudiwa na Katibu tawala wa mkoa wa
Arusha, Richard Kwitega, na maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Ulinzi
la wananchi wa Tanzania.
Akizungumza
mara baada ya kuweka shada hilo la maua kwenye mnara huo uliopo kwenye
bustani ya mkuu wa mkoa wa Arusha ,Nickol,maarufu mwanickol, amesema
amekuwa akija nchini kutoka kwao Uingereza, kila mwaka kuja kuweka shada
la maua kwenye mnara huo ikiwa ni kumbukumbu na heshima kwa askari wa
Tanzania waliokufa wakiwa vitani.
Nickol ,amesema alikuwa ni mkuu wa wilaya za Arusha, na Singida, mara tu Tanganyika ilipopata Uhuru wake mwaka 1961kabla ya kustaafu na kurejea kwao na hivyo ana mapenzi makubwa na Tanzania.
Amesema wakati akiwa askari alishiriki vita ya pili ya dunia,ambapo alipigana kwenye nchi mbalimbali ikiwemo
nchini Burma, Ethiopia ,Madagascan a Somalia ambapo walipata mafanikio
makubwa nchini Somalia walipoweza kuwashinda Wataiano,baada ya kupigana
kwa muda wa miezi sita na kukamata mateka wengi.
Nickol,amesema
ni jambo la heshima kubwa kwake kuja nchini na kuweka maua kwenye mnara
wa askari waliokufa wakiwa vitani na anaishukuru serikali ya Tanzania.
Amesema hakuna nchini nyingine barani afrika anayoiheshimu kama Tanzania kwa kuwa ni nchi yenye Ukarimu,Ustaarabu na upendo ameahidi kuja nchini kila mwaka ili kudhuru mnara huo wa mashujaa na hiyo inatokana na kuthamini na kutambua umuhimu wa askari wa jeshi .
Nae Balozi wa Uingereza nchini, Richard Beatty Obe, amesema serikali yake itamwezesha Capten huyo msitaafu kila mwaka kuja nchini Tanzania kudhuru mnara huo wa kumbu kumbu ya mashujaa kuwekashada la maua .
Kwa
upande wake Katibu tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, amesema
hiyo ni heshima pekee kwa Tanzania, kutembelewa na afisa huyo mstaafu wa
cheo cha Kapten kutoka Uingereza na kutembelea mnara wa kumbu kumbu ya askari wa vita ya Kagera.
Amesema kuwa
afisa huyo raia wa Uingereza ana moyo wa kipekee na ni mfano wa kuigwa
kutokana na upendo wake alionao kwa Tanzania ,kufunga safari kutoka kwao
kuja nchini kwetu na hiyo ni heshima kubwa kwa nchi yetu.
No comments :
Post a Comment