Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MWALIMU wa Ujasiriamali katika Chuo cha VETA-
Karagwe mkoani Kagera Hamiss Jumanne amesema
kwamba chuo chao kimekuja na ubunifu wa
kutengeza Wine(Mvinyo) unatokana na tangawizi,
Mchaichai na Amdalasini ambayo ni tofauti kabisa
na aina nyingine za Wine zinazotengenezwa ndani
na nje ya Tanzania.
Akizungumza na Michuzi TV katika Banda la VETA
lililopo kwenye Maonesho ya 46 ya kimataifa ya
Biashara yanayoendelea viwanja vya Sabasaba
mkoani Dar es Salaam Mwalimu Jumanne amesema
katika maonesho hayo yenye ujumbe unaosema
Tanzania ni mahali sahihi kwa uwekezaji na masuala
ya biashara wao VETA –Karagwe wameamua kuja
na ubunifu wa kipee wa kutengeza Wine hiyo.
“Sisi VETA Karagwe tumekuja na kitu cha ubunifu
kabisa na cha kipekee utengenezaji wa Wine kwa
kutumia Mchaichai ,Amdalasini, Rozela pamoja na
Tangazi ,huu ni utofauti mkubwa sana na ubunifu
wa kipee ambao pia tumekuwa tukiwafundisha
wanafunzi wetu kuona thamani ya vituo vingine.
“Wamezoea Mchaichai na Amdalasini unatumika
kwenye chai tu lakini leo kwa ubunifu wetu uko
kwenye Wine , ukiweka Wine kwa namna hii
wanafunzi wakienda mtaani wataamua kujitegea
wenyewe kwasababu watakuwa wamepata maarifa
haya lakini itaongeza thamani na uchumi kwa
wananchi.
“Ule Mchaichai na tangawizi vitalimwa kwa wingi
sana ili waweze kuleta viwandani na viwandani
vingine vinaweza kukua, kumbuka wanafunzi hawa
ndio watakuwa wakurugenzi wa baadae.Kwa hiyo
Wine hii ni tofauti na Wine nyingine kwani tuna
fahamu zipo Wine zinazotengenezwa na Zabibu na
Rozela lakini VETA Karagwe tumekua na Wine
inayotokana na tangawizi, mchaichai na
amdalasini.”
Amesisitiza hivyo Wine hiyo ni ya upekee kabisa
unayoipata wilayani Karagwe Kagera na
inafahamika kwa jina la Kombucha na
mchanganyiko wake pamoja na mambo mengine
umekuwa unasaidia kusafisha na kuimarisha
mishipa, hivyo hata kwenye suala la tendo la ndio
linakuwa liko vizuri lakini hairuhusiwi kwa walio na
umri chini ya miaka 18.
Amefafanua kwa anayetaka Wine hiyo kwa sasa
wako Sabasaba na wanaohitaji wanakaribishwa
banda la VETA.“Lakini unaweza kupiga simu 0759
817029 ina maana ukiwasiliana na sisii basi
tunakuletea popote ulipo kwani Serikali yetu
imerahisisha masuala ya usafiri.
“Sisi kutoka Karagwe basi ikitoka kule asubuhi saa
nane usiku inakuwa imefika Dar es Salaam na Wine
itakuwa imekufikia.Watu wanavutiwa sana kwani
kila ambaye ananunua anarudi tena kutokana na ule
uasili uliomo kwenye Wine yetu.”
No comments :
Post a Comment