Monday, July 4, 2022

CHUO CHA VETA CHA MAFUNZO YA HOTELI NA UTALII WAJA NA UBUNIFU WA NDIZI KITASARA INAYOTUMIKA KATIKA UTIBU MAGONJWA

Mwanafunzi wa Chuo cha VETA cha Mafunzo ya

Hoteli na Utalii (VHTTI) kilichopo Njiro mkoani

Arusha Happiness Michael akiwa ameshika ndizi

Kitarasa ambayo ikichanganywa na mbaazi

inatengeza vyakula ambavyo vinatibu magongwa

mbalimbali yakiwemo ya sukari, pasha , kuongeza

kinga ya mwili pamoja na kuimarisha afya ya akili

kwa mtoto.Mwanfunzi huyo yuko kwenye banda la

VETA katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya

Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya

Sabasaba mkoani Dar es Salaam.

Happiness Michael ambaye ni mwanafunzi wa

Chuo cha VETA ch Mafunzo ya Hoteli na Utalii

kilichopo Njiro mkoani Arusha akionesha unga

unatokana na ndizi kitarasa ambayo inatumika

kutengeneza aina mbalimbali za vyakula.

Baadhi ya wanafunzi na walimu wa Chuo cha

VETA cha Mafunzo ya Hoteli na Utalii Njiro mkoani

Arusha wakiwa katika picha ya pamoja kwenye

kwenye banda la VETA.


 Na Said Mwishehe, Michuzi TVCHUO cha VETA cha Mafunzo ya Hoteli na Utalii(VHTTI) kilichopo Njiro mkoani Arushaambacho kinamilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)kimekuja na ubunifu wa mazao ya ndizi kitarasa na mbaazi kutengezavyakula ambavyo vinatumika kutengeneza vyakulaambavyo ni tiba ya kutibu magonjwa mbalimbaliyakiwemo ya kisukari na presha.Akizungumza kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa

ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya MwalimuNyerere maarufu Sabasaba Mwanafunzi

anayesomea katika

chuo hicho Happiness Michael

amesema kwa mwaka huu katika maonesho hayo


wamekuja na ubunifu wa mapishi kwa kutumia ndizi

kitarasa na mbaazi.

“Sisi na walimu wetu katika maonesho ya mwaka

huu tumekuja na ubunifu wa mazao ambayo ni ndizi

na mbaazi na ndizi , hii ndizi ambayo tumeileta hapa

iko tofauti na ndizi zingine, hivyo tumeamua

kuchagua ndizi Kitarasa na mbaazi ni kwasababu

mazao hayo yalikuwa hayapewi kipaumbele katika

mlo wa binadamu.

“Kwa hiyo sisi tumechukua hiyo fursa na tulilenga

kwa watu ambao hawatumii ngano kwa hiyo

tumetumia ndizi kitarasa pamoja na mbaazi

kutengeza baadhi ya vyakula ama vyakula vyote

vinavyokuwa vinatengenezwa na ngano, mfano

mkate , maandazi ,biskuti, keki na hiyo sio moja kwa

moja mtu anakula tu lakini anakuwa anapata

tiba.Mtu anapotumia ndizi kitarasa na mbaazi

anakuwa anatibu kisukari , presha, mwili wenye

kujaa mafuta na vile vile kwa wale


wanaosumbuliwa na tatizo la kinga za mwili

zinakuwa zinashuka.

“Na hata watoto zinakwenda kujenga afya ya akili,

ndizi ya kitasara yenyewe iko tofauti na ndizi

nyingine na yenyewe kinachoangaliwa ni ule

utomvu ambao ndio tiba yenyewe na ndio maana

tukaamua kuchagua ndizi kitarasa.Hata wanaotaka

kuacha kuvuta sigara ni vema wakatumia ndizi

kitarasa na mbaazi .

“Hii ndizi unaweza kutumia ikiwa mbivu, ikipikwa ,

na unga, lakini kwa sisi tulikuwa tunalenga kutumia

unga , hivyo tulikuwa tunachukua ndizi kitarasa

kisha tunamenya tunaanika na tukishaanika

tunakwenda kusaga na kupata unga kwa ajili ya

matumizi ya kutengeza vile vitafunwa.Hii ndizi na

tangu enzi na enzi na kule Kilimanjaro zamani

ilikuwa inatumika wakati wa njaa,”amesema.

Wakati huo huo, amesema chuo chao mbali ya kuja

na ubunifu wa mazao hayo ,wamekuw wakielezea

kozi ambazo zinafundishwa katika chuo chao


ambacho kipo kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota

tatu.Ametaja baadhi ya kozi ni uokaji mikate, keki

na mapishi ya vyakula, mapambo na upambaji wa

kumbi za starehe, mafunzo ya kompyuta na mbinu

za uandaaji Cocktail.

Kozi nyingine ni ya usafi wa majengo na maeneo ya

wazi, huduma kwa wateja , mbinu za ujasiriamali,

usimamizi wa shughuli za mapokezi na vyumba,

uhudumu na uuzaji wa chakula na vinywaji,

uaandaji na upishi wa chakula , utaalamu wa

uongozaji watalii pamoja na uandaaji na uendeshaji

wa safari za watalii.

No comments :

Post a Comment