Wednesday, December 1, 2021

ONGEZEKO LA WATU LIMECHOCHEA MABADILIKO SEKTA YA AFYA- MUHAS

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili MUHAS Prof Andrea Pembe akizungumza na wanataaluma mbalimbali wakati wa Kongamano la Miaka 60 ya Uhuru kuzungumzia mabadiliko ya sekta ya afya ilipokua na ilipo kwa sasa.
Wanataaluma mbalimbali wakifuatilia Kongamano hilo
*Asilimia 40 wanaishi mijini

*magonjwa yasiyo ya kuambukiza na mlipuko yashika kasi

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Ongezeko la watu nchini na kufikia Asilimia 40 ya watanzania wanaishi mjini  imepelekea mabadiliko mbalimbali ikiwemo kutoka magonjwa ya kuambikizwa hadi magonjwa ya mlipuko.

Hayo yamesemwa leo wakati wa Kongamano la miaka 60 ya Uhuru katika Sekta Afya yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam yakiendeshwa na Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kongamano hilo, Makamu Mkuu wa Chuo cha Muhas Prof Andrea Pembe amesema, ongezeko la watu limepelekea mabadiliko katika kada ya afya ambapo kabla na baada ya uhuru kulikua na magonjwa ya kuambukiza ila kwa sasa kumekuwa na magonjwa mengi ya mlipuko na yasiyoambukiza.

“Dhima ya kongamano hili ni kuangalia namna mabadiliko ya magonjwa na namna sekta ya afya ilivyojipanga kukabiliana nayo ndani ya miaka 60 ya uhuru,” amesema

“Wakat wa uhuru watu walikua milion 9 na sasa hv ni takribani milion 60 na asilimia kubwa ya watanzania wanaishi mjini hali hiyo imepelekea mabadiliko mbalimbali ikiwemo chakula, Wingi wa watu na aina ya maisha yameleta yamesababisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko na yasiyo ya kuambukiza kama Shinikizo la damu, Kisukari na hata magonjwa kama Uviko 19,” 

Prof Pembe amesema, sekta ya afya imejipanga kukabiliana na magonjwa hayo kwa kuchanganua changamoto na namna ya kukabiliana nayo kiutafiti na kimatibabu na kuyafuatilia kwa umakini zaidi ili yafanyiwe kazi  na kuchukuliwa hatua.

Amesema, magonjwa ya mlipuko yanatofautiana na yanasambaa kwa kasi sana na ametoa ushauri kwa watanzania kuendelea kuchukua tahadhari juu ya Uviko 19 na kuwataka waendelee kuchanja ili kujiweka salama zaidi.

Akizungumzia upande wa Kada ya Sekta ya Afya na watoa huduma- Prof Pembe amesema Ndan ya miaka 60 sekta ya afya imekwenda mbali sana na kuna Vyuo vikuu vishiriki 10 vinayotoa wataalam wa afya sekta.Amesema, changamoto iliyopo ni Upungufu wa wataalamu wa afya ambapo jumla ya wataalamu 10,000 wanahitimu katika ngazi mbalimbali na hiyo imetokana na kuongezeka kwa hospital, vituo vya afya na hata hospitali za watu binafsi ukilinganisha na wakati nchi inapata Uhuru kulikua na hospitali 30.

Aidha, Prof Pembe amesema ndani ya miaka 60 ya Uhuru ni asilimia 20-28 sekta ya afya imeboresha na kufanya mabadiliko ya wakianzisha vitengo maalum vinavyotoa huduma za kibobezi, huduma maalu za kimatibabu na upatikanaji wa vifaa tiba.

Kwa sasa Tanzania  imekuwa inatoa huduma muhimu ambazo awali zilikya hazipatikani ndani ya nchi ikiwemo Matibabu ya Figo, Moyo, Ini na uanzishwaji wa kitengo maalumu cha Mifupa MOI.

No comments :

Post a Comment