Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la Bunge
katika maonyesho ya 45 ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es
Salaam, Julai 5, 2021
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Herman Berege
akifafanua jambo kuhusu historia ya Bunge mbele ya wageni mbalimbali
waliotembelea Banda la Bunge katika maonyesho ya 45 ya Sabasaba
yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, Julai 5, 2021
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Hamad Hassan Chande (kushoto) akipokea
zawadi kutoka kwa Afisa Habari Ofisi ya Bunge, Zuhura Mtatifikolo mara
baada ya kutembelea Banda la Bunge katika maonyesho ya 45 ya Sabasaba
yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, Julai 5, 2021
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
No comments :
Post a Comment