Monday, July 5, 2021

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MAONESHO YA 45 YA SABASABA (PICHA)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipata maelezo kutika kwa Mkuu wa Jeshi la kujenga taifa Brig Jenerali Rajabu Mabele wakati alipotembelea katika Banda hilo la Jeshi la Kujenga Taifa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea zawadi ya begi kwa ajili yake (picha namba 3) na kwaajili ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan( Picha namba 2) wakati alipokuwa akizindua maonesho hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na mjasiriamali Bi Aziza Saidi anayefanya biashara ya tiba mbadala. wakati alipotembelea banda maalum la wafanyabiashara wadogo( Machinga). Makamu wa Rais ameagiza Bi Aziza kusaidiwa haraka katika biashara yake hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akitembelea mabanda mbalimbali kujionea bidhaa zilizopo kwenye maonesho ya sabasaba ya mwaka 2021 wakati alipofika kuzindua maonesho hayo.

 

No comments :

Post a Comment