Monday, July 5, 2021

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) UNAENDELEA KUKUA KWA KASI: WAZIRI JENISTA MHAGAMA


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akifafanua jambo huku akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano, Bi. Laura Kunenge wakati Waziri alipotembelea banda la WCF kwenye maonesho ya 45 yab Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 5, 2021.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari huku akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kulia)

Mhe. Waziri Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, wakurugenzi na wafanyakazi wa Mfuko.
Waziri Mhagama akipokelewa na Mkurugezni Mkuu wa WCF, Dkt. Mduma wakati akiwasili kwenye banda la Mfuko huo.
Waziri Mhagama akisalimiana na Mkuu w aKitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge wakati akiwasili kwenye banda hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba huku baadhi wa wafanyakazi wa mfuko huo wakishuhudia, baada ya Bw. Mshomba kutembeela banda la WCF Julai 5, 2021. Itakumbukwa ya kuwa Bw. Mshomba ndiye alikuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Mfuko huo mara tu baada ya kuanzishwa mwaka 2015 hadi alipoteuliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan  mwaka huu 2021 kwenda NSSF.
Dkt. Mduma na Bw. Mshomba wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa WCF nje ya banda la mfuko huo Julai 5, 2021
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, dkt. John Mduma (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anselim Peter

 NA KHALFAN SAID, SABASABA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unaendelea kukua kwa kasi ambapo mwaka 2016 ulikuwa na thamani ya bilioni 65.7 na kwa sasa umefikia thamani ya bilioni 438.
Waziri aliyasema hayo Julai 5, 2021 wakati alipotembelea banda la WCF kwenye maonesho ya 45 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba ili kujionea jinsi wanachama wa Mfuko huo ambaom ni waajiri pamoja na wafanyakazi wakiwemo wananchi wanavyohudumiwa.
Mfuko wa WCF uko chini ya Ofisi ya Wazitri Mkuu.
“Tuko Vizuri hata kwenye mafao tumetoka kwenye malipo ya fidia kiasi cha shilingi bilioni 1.5 na sasa malipo ya fidia yamefikia hadi  shilingi bilioni 27,” alisema Waziri Mhagama.
Alisema lengo la uwepo wa Mfuko ni kuhakikisha wafanyakazi wanaoumia wakiwa kazini kwa vigezo na sheria inavyosema Serikali kupitia WCF iwalipe fidia au iwatibu na wakipona warejee kazini kuendelea na majukumu yao.
“Kubwa ni kuendelea kuimarisha mifumo na utoaji elimu kwa walengwa ili waajiri na wafanyakazi waujue Mfuko na majukumu yake……Sasa hivi tunasema tuko kwenye uchumi wa viwanda, viashiria vingi vya uwepo wa ajali kazini eneo moja ni kwenye sekta ya viwanda, usafirishaji  kwahiyo tunaposherehekea maonesho haya ya Sabasaba tuhakikishe Mfuko unatekeleza majukumu yake ipasavyo.” Alisema Waziri Mhagama.

No comments :

Post a Comment