Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Dk.Philip Mpango (wa pili
kutoka kulia) akipita katika banda la Barrick wakati alipotembelea
maonesho ya Sabasaba.
Kampuni
ya madini ya Barrick, inashiriki katika maonesho ya 45 ya kimataifa ya
Biashara (SabaSaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam, ambapo banda
lake la maonesho linaendelea kutembelewa na viongozi mbalimbali wa
Serikali pamoja na wananchi ambao wanapata fursa ya kuelewa kwa undani
shughuli za kampuni hiyo.
Mbali
na ushiriki kampuni ya Barrick, pia imewezesha wajasiriamali kutoka
vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga, kwa
ajili ya kuonesha bidhaa zao kwa lengo la kupata masoko zaidi na kupata
maarifa kutoka kwa wajasiriamali wengine wanaoshiriki kwenye maonesho
hayo.
Barrick
imekuwa ikiwezesha wajasiriamali hao kwa kuwapatia elimu ya ukuzaji
biashara zao, na kwa wale wanaoshughulika na kilimo wamekuwa wakipatiwa
mbegu bora na mbolea.
Waziri
wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya
Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la
kampuni hiyo katika maonesho ya Sabasaba
Waziri
wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya
Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la
kampuni hiyo katika maonesho ya Sabasab
Waziri
wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya
Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la
kampuni hiyo katika maonesho ya Sabasaba
Wafanyakazi
wa Barrick katika banda la wajasiriamali kutoka Bulynhulu wanaoshiriki
maonesho ya biashara ya SabaSaba kwa ufadhili wa kampuni hiyo.
No comments :
Post a Comment