Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiongea
na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk pamoja na watumishi wa Wizara
wakati alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa
ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es
salaam.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na watumishi wa Wizara wakati
alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya
Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Geoffrey Mwambe (Mb) akipokea
nakala ya Jarida la Diplomasia linalochapishwa na Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara katika
Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam
Na Mwandishi wetu, Dar
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameitaka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa
kushirikiana na Balozi za Tanzania kuainisha na kutangaza fursa
mbalimbali zilizopo nchini hususani biashara na uwekezaji.
Dkt.
Mpango ametoa maelekezo hayo alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
Dar es salaam. Mara baada ya kuwasili katika banda la Wizara, Dkt.
Mpango amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
“Naipongeza
Wizara kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuimarisha mahusiano ya
kidiplomasia ……..lakini pia Wizara iendelee kuzishirikisha Balozi zetu
katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini, na Balozi hizo
ziainishe fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nchi za uwakilishi kwa
ajili ya Watanzania,” Amesema Dkt. Mpango
Pamoja
na mambo mengine, Dkt. Mpango ameielekeza Wizara ya Maambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kuboresha majukumu ya Wizara
ikiwa ni pamoja na balozi za Tanzania na Taasisi zake.
No comments :
Post a Comment