Hababuu
amesema mafunzo hayo yatawasaidia wadau wa madini kufanya kazi zao za
uchimbaji na ulipuaji kwa ubora, uhakika na usalama zaidi tofauti na
awali.
Amesema
mafunzo hayo yatahusisha mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya usalama,
utumiaji wa vifaa vya kisasa na utumiaji wa njia za uchimbaji wa kisasa
kutoka kwa wataalamu wa chuo cha DIT.
“Ni
fursa nzuri kwa wadau wa madini kushiriki mafunzo hayo ya wiki mbili
yatakayoanza Juni 7 hadi Juni 18 kuanzia saa tisa alasiri hadi saa moja
jioni,” amesema Hababuu.
Wakili
wa kampuni ya kisheria ya L & L Attorney @ law, Faisal Rukaka,
akizungumza na wachimbaji hao wa madini ya Tanzanite, amesema suala la
wadau wa madini ya Tanzanite kuwa na wanasheria halikwepeki.
Rukaka
amesema wachimbaji wanapaswa kushirikiana na serikali na wao wanasheria
ili kujengewa uwezo wa masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kupata
vibali mbalimbali.
Amesema
serikali ni mlezi wao wadau wa madini ila wanapaswa kuwa na wanasheria
watakaoweza kuwapa elimu ikiwemo ya uchimbaji, kodi, leseni na mambo
mbalimbali.
Amesema
kutokujua sheria siyo utetezi wa kufanya kosa hivyo kupitia wanasheria
wanaweza kushirikiana na wahusika wa fani husika ikiwemo wanasheria ili
kuendeleza kazi zao kwa mapana zaidi.
“Kunakuwepo
na makosa madogo madogo ambayo wangekuwa na wanasheria wangeweza
kunufaika juu ya masuala ya kisheria na shughuli zao kwenda vizuri
inavyopaswa,” amesema Rukaka.

No comments :
Post a Comment