
WAZIRI wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula akijibu maswali ya wabunge Bungeni Jijini Dodoma
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia NGOs Neema Lugangira akitoa Mchango wake kwenye
Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje
WAZIRI wa Mambo
ya Nje Balozi Liberata Mulamula amesema kabla ya mwaka huu kuisha Sera
ya Nje inayojumuisha Sera ya Diaspora itakuwa tayari na hiyo ni kwa
kutambua umuhimu wa ...diaspora katika kuchangia maendeleo na masuala ya
diaspora yanapewa kipaumbele.
Ameyasema hayo
Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu kuhusu Ushauri aliotoa Mbunge wa
Viti Maalumu kupitia NGOs Neema Lugangira katika Mchango wake kwenye
Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje alipoitaka Serikali itunge Sera ya
Diaspora ambayi ni Sera hiyo ni muhimu na kwa sababu jambo hilo haliwezi
kuendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje pekee kwa sababu linahusu Sekta
nyingi.
“Mh Spika
ningependa kugusia suala la diaspora hili jambo lilishawai kujadiliwa
sana na tulishapiga hatua ambapo diaspora hao mikutano mbalimbali
ilifanyika nje ya nchi na walishiriki hata kutoa maoni kwenye katiba
mpya ambayo inapendekezwa sasa nimefurahi kwenye Hotuba, Mhe Waziri
amewagusia suala la diaspora na hata kwenye mapendezo ya kamati nao
wameguaisia suala la diaspora” Alisema
Mbunge Lugangira
aliendelea kusema kwamba lile zoezi la ziara nyingi nje ya nchi
zilizokusanya maoni ya diaspora na hadi kuwashirikisha diaspora kwenye
huo mchakato Katiba mpya inayopendekezwa yalipelekea hayo kuanzishwa kwa
Idara ya Diaspora ndani ya Wizara na Mambo ya Nje ambapo kulikuwa na
Mkurugenzi kwenye jukumu la kufanya coordination na ufuatiliaji.
Aliendelea kusema
kwamba hivi sasa imeonekana kama jambo hilo limerudi nyuma kwa sababu
hivi sasa kuna Sheria ambazo zinamzuia Mtanzania anayeishi Nje ya Nchi
kumiliki ardhi lakini pia zipo Sheria ambazo zinamnyima haki ya kurithi
mali za wazazi wake kwa sababu Sheria zimeweka hicho kizuizi na kwa
msingi huo anapendekeza Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi iandae Sera ya
Diaspora.
Alisema kwa
sababu nchi nyengine wanatumia diaspora kuendeleza uchumi na uwekezaji
hivyo Serikali itunge Sera ya Diaspora na Sera hiyo ni muhimu kwa sababu
nasi pia Tanzania tutaweza kutumia diaspora kuchangia kukuza uchumi wa
nchi yetu ambayo ni nchi yao pia.
“Mh Spika Mbunge
mwenzangu ametoa mfano wa India lakini naomba nilitolee ufafanuzi.
Nchini India walichofanya wamewapa Wahindi wanaoishi Nje ya India kitu
kinachoitwa Pasipoti ya People’s of India Origin (PIO) ambayo PIO hiyo
inamruhusu mwenye pasipoti ya PIO kuingia India na kutoka muda wowote
bila Viza, in mruhusu kuwekeza kwenye hiyo nchi na kufanya kazi kwenye
Sekta zote kasoro Sekta ya Ulinzi na Usalama” Alisema Mbunge Neema
Lugangira
Alisema pia
“Jambo lingine ambao Wahindi wenye Pasipoti ya PIO ambalo hawatakiwi
kufanya ni kujishughulisha na masuala ya kisiasa na kupiga kura hivyo
mantiki hiyo Mhe Spika napendekeza na sisi kama Tanzania tufike huko na
hatuwezi kwenda huko bila kuwa na Sera ya Diapsora na Sheria ambayo
itaelekeza ni namna gani tutatoa fursa kwa diaspora.
“Katika jambo
hili naomba tusichanganye mambo mawili ya diaspora na uraia pacha hilo
la uraia pacha tumelijadili na limeoneka lina ugumu hivyo lisituchukulie
muda lakini la diaspora lipo ndani ya uwezo wetu na hata sasa hivi
diaspora wananunua viwanja wanawekeza na wanafanya hivyo kutumia kwa
kutumia njia zisizo rasmi kwa kutumia ndugu jamaa na marafiki
“Alisisitiza Mbunge Neema Lugangira
Alisema hivyo
wanachotakiwa kufanya ni Wizara ya Mambo ya Nje iwe na Sera ya Diaspora
ili kuweka suala hilo rasmi na kupitia Sera hiyo Nchi itaweza kujua kuna
diaspora wangapi na mchango wao katika ukuaji wa uchumi ni upi.
“Kwa kumalizia
naomba Mhe Waziri atapokuja kuhitimisha atuambie na atupe Msimamo wa
Serikali wa kuja na Sera ya Diaspora ambayo itawezesha Watanzania
wanaoishi Nje ya Nchi kuchangia kwenye maendeleo ya nchi na kutoa
rasimali fedha amboyo tunaihitaji kwenye uwekezaji ”Alisema Mbunge Neema
Awali wakati
anaanza Mchango wake Mbunge Neema Lugangira alisema “Nampongeza sana Mhe
Rais Samia Suluhu kwa ziara aliyoifanya nchini Kenya ambayo imeleta
matokeo makubwa sana katika diplomasia ya uchumi inayohitajika nchini na
kama unavyofahamu wiki hii Kenya na Tanzania wamekubaliana kuondoa Tozi
za biashara 30 na kuna mchakato wa kuondoka Tozo 34 na hayo ni matokeo
ya jitihada kubwa za Mhe Rais lakini pia nimpongeze Mhe Waziri wa
Viwanda na Baishara kwa kufanikisha jambo hilo”.
Mbunge Neema
Lugangira alisisitiza kwamba Mtazamo wa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan
kuhusu Kenya kwamba sio adui wetu uungwe mkono kwani Kenya ni mshindani
mwenzetu, wanatupa changamoto, tusiwaogope kutokana na kwamba tunaweza
kushindana nao na kuwakabili.
“Niungane na
Wabunge wenzangu ambao wametoa pongeza kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan
kuhusu kutengeneza safu mpya kwenye Wizara ya Mambo ya Nje iliyojaa
wabobezi kwenye fani ya diplomasia ikiongozwa na Waziri Balozi mwanamama
Liberata Mulamula, Naibu Waziri Mbaruku, Katibu Mkuu Balozi Sokoine,
Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Rajabu na Chief Protocol Balozi Mndolwa
ambao tunaimani nao kubwa sana na sasa tunaona diplomasia nchini inapaa”
Alisema Mbunge Lugangira

No comments :
Post a Comment