Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisuru imeelezwa kuwa, mazungumzo ya makubaliano (Plea
bargaining) ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili... Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth yanasuburi Muongozo wa
Mkurugenzi mpya wa Mashtaka (DPP).
Wakili
wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon ameeleza hayo leo Juni 3, 2021
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa
ajili ya kutajwa na kujua hatma ya mazungumzo hayo na upelelezi
ulipofikia.
"Mheshimwa
Hakimu, kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado na pia
mazunguzo ya kumaliza kesi dhidi ya mshtakiwa Seth yanaendelea pale
yalipoishia, Qtunasuburi muongozo kutoka kwa DPP mpya aliyeteuliwa hivi
karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan ili tuweze kuwakilisha hapa mahakamani.
Awali
Seth na Makandege waliwasilisha ombi kwa DPP wakionesha nia yao ya
kutaka maliza kesi kwa kukiri makosa yao lakini, Mei 6, 2021 Wakili
Makandege aliondoa nia yake ya kufanya makubaliano na DPP akieleza
kwamba mazungumzo hayo hayana afya na yamechukua muda mrefu kukamilika.
Mbali na Seth washtakiwa wengine Katika kesi hiyo ni mfanyabiashara James Rugemalira na wakili Joseph Makandege
Rugemarila,
ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na
Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, wanadaiwa kutenda makosa
hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na
India.
Washtakiwa
wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha, miongoni
mwa mashtaka hayo yapo ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu,
kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani
22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Washtakiwa
wanadaiwa kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam
walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mwanasheria Makandege, anakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 980,000.

No comments :
Post a Comment